mimi alishakuja getto nikasonga ugali akajifanya ugali haupandi nimnunulie chipsi si unajua masista duu nikaufinya peke yangu, nikamwambia hela niliyonayo haitoshi chips.
Akaniomba nauli nikampa 500 alikaa wiki moja hajanipigia simu na mimi nikamkaushia akaona nini sijui akaamua kwenda hewani. Siku nyingine akarudi getto tukapeana mambo
@maryketi
kuna kujikuta umechemsha siku ya kwanza bila hata kujua ni kwa nini.
Bora hata huyu alichemka kwa kukosa hela, wengine tukielezea yalotupata mtasema tulivuta bangi. Things happen, sijui for what reason.
kwa hyo mliiba sio?
SIMULIZI hii ni ya ukweli, ukizani uongo basi shauri yako; hususani wewe mwanaume mwenzangu upendae kujikweza mbele ya vidosho!!
In short ni kwamba, siku hizi nimechoka mbaya lakini enzi zile ilikuwa ni TOO MUCH!! Basi kipindi kile cha msoto wa kutisha, nikabahatika kukutana na msichana mmoja.. mzuri wa haja; mama Mnyamwezi, baba Masalia ya Waarabu! Hebu pata picha, huyo kinda linalotoka hapo litakuwaje!! Hata hivyo, yule shori hakuwa mwenyeji sana hapa Dar ni product ya Nzega, Tabora!
Basi bwana, tukaachiana contacts! Ikawa mara kwa mara tunawasiliana hadi penzi likachanua na kukomaa!!
Siku moja, nikiwa sina hili wala lile; binti wa watu akaenda hewani! Bila kutarajia, akaniambia anataka kuja ghetto! Kucheki saa, nikakuta inakaribia saa 11.30 jioni! NIKASHANGAA! Nikashangaa kwavile aliniambia anaishi Pugu wakati mimi naishi Temeke! Nikajiuliza, mida yenyewe ni jioni kabisa inayokaribia machweo na Pugu na Temeke ni mbali ile mbaya! Nikajiuliza kwao atarudi saa ngapi! Nilipomuuliza atarudi saa ngapi wakati mida imeenda sana, akajibu anakuja kulala kwangu!
Liudenda likanimwagika, na kijasho chembamba nacho kikanitiririka kidume cha watu! Nilipoingia mfukoni, nikajikuta nina buku unusu (TZS 1,500/=) pekee! Kwa mida ile, nisingeweza kufanya makaratee yoyote! Nilipoenda kwenye friji, nikakuta kumbe maharage yangu niliyopika mchana bado yapo! Kucheki kwenye kindoo change, nikakuta kuna mchele wa kutosha! Nikajua hapa anasa hamna lakini kulala njaa vile vile hakupo!
Kuona hivyo, nikaenda hewani, ile binti kupokea nikampa full data..!! Nikamwambia wazi, kwamba hapa nipo alosto ile mbaya kwahiyo kama ana mpango wa kuja akae akijua nini atakutana nacho! Nikamwambia wazi kwamba nilikuwa na buku unusu tu ambayo ndo bajeti yangu ya siku inayofuata!
Sina hakika kama alizani natania au vipi! Akajibu kwa kujiamini, kwamba POA TU! Kama masihara vile, binti akapanda daladala na akaniambia nimfuate TAZARA. Hivyo basi, ile kufika TAZARA tu, nikajikuta nimeshatumia TZS 300/- na hivyo kubakiwa na TZS 1,200/=! Muda kidogo, binti akafika! Kwa sababu ninazozijua mwenyewe, nikakata shauri la kupanda magari ya kwenda Posta badala ya kuchukua ya moja kwa moja! Ile kufika Posta, kidume nikajikuta nimebakiwa na TZS 600/- tu! Toka posta, tukachukua daladala za TMK ile kufika ghetto, sina hata thumuni .!!!
Kilichomtoa kwao, akakipata!
Siku ya pili akabaki ghetto hadi mchana! Ile anajiandaa kuondoka, nikajikooza na kujiweka sawa!! Huku nikiwa na macho makavu, nikamwambia:
Dont forget ile jana nilikuambia nilikuwa na 1,500/- tu ambayo ilikuwa ndo bajeti yangu ya leo! Hata hivyo, hivyo, ela yote iliishia kwenye nauli na hapa sina hata senti tano!
Kwahiyo? Binti wa watu akaniuliza!
inabidi uniache angalau na buku!
Bibti yule alicheka hadi basi kasha akazama kwenye kipochi chake na kuniacha na gwala (5,000/=)! Kidume nikaua ndege wawili kwa kajiwe kamoja!!
Nilizani binti yule asingekuja tena; kumbe wapi!!
MWANAUME MWENZANGU vipi, yashawahi kukuta haya?! Kama hapana, je kama yangekukuta katika situation ambayo nilikuwa nayo ungefanya nini?! Ungeenda kukopa au ungejifanya umesafiri?! Au ungejifanya leo ghetto kuna mgeni kwahiyo aje siku nyingine?! Au na wewe ungeyafanya haya niliyofanya mimi?! Usisahau, hiyo ilikuwa ndo mara yetu ya kwanza kukutana faragha!
NAWE mdada, ungekuwa ndie wewe .nikakupa ukweli huo, ungekuja tu ghetto au ndo ungekuwa mwisho wa mchezo?!

wala, ni dalili mbaya mwanaume kuniomba hela siku ya kwanza, mbona yeye hakuleta shida zake kwako siku hiyo hiyo
alikuja kukutembelea kwa strehe zake na ndio maana akaja na nauli yake na pengine alikuja ameshiba kabisa, sasa wewe ukajua amekuja kukuchuna ndo maana ukajiwahi kumchuna kwani usingeomba hela siku isinge isha, mwanaume wa type yako sirudiii tena
alijua anakuja kukutembelea kwa starehe zake na ndio maana akaja na nauli yake ili asikupe mzigo,na pengine alikuja ameshiba kabisa hakuwana shida na huo msosi
hii hata kama ni changa la macho...bado imekaa vyema sana!...ila mkuu ni kwamba tumekariri sisi vidume siku zote ndo wakutoa huduma!...tunajikamua mpaka damu...tunaingia madeni sugu...kisa uonekane uko juu...hatujui WANAWAKE ni waelewa sana...hili ni bonge la PINDI yani!...BIG UP MAN...
BTW mikasa yangu ni midogo midogo tu!..
Mi nisingerudi. Lol
wewe ni jembe kaka, mimi ningeenda kukopa. ila usiniulize kwanini na wala usinilaumu
Usingerudi wapi Husninyo? Ungehamia ghetto moja kwa moja au baada ya kutoka ghetto usingekuja tena?
Mimi niliacha simu gesti, meneja aliniambia gest buku tatu mimi sikumuelewa kumbe ni kwa lisaa.
Bajeti yangu ilikua buku kumi na tano kila kitu.
Ilikua J'pili moja mtoto kanipigia simu anakuja getto. Siku hiyo ilikua noma maana mwenye nyumba anashinda nyumbani na kodi yake nshapitisha mwezi na nusu hivyo lazima angenikoromea.
Akili ya haraka haraka ilikuja niingie gest za uchochoroni. Saa saba na nusu hivi pale studio kituoni mtoto kashuka anaona tunaelekea kusiko.. kuniuliza kulikoni nikamwambia getto soo maji hamna alafu choo kinatoa harufu.
Tukafika hiyo gest kwa nje kuna mangi anakaanga chips kuku. Kuwa na uakika nikaenda kuuliza chumba nikaambiwa buku tatu ila nisubiri kidogo ataniita.
Wakati tunasuburi nikaagiza kuku chips 2 nikaona ngoja nipige na kamzika kadogo ka konyagi ili kuongeza kasi.
Mtoto alipiga soda yeye. Mangi kuleta bili nikakuta ninabakiwa na buku nne unusu, ambayo bado niliona nika vizuri kutokana na bei ya gest.
Meneja akanishtua tukaingia ndani... basi siku hiyo nilipiga gemu balaa. Tuliingia kwenye saa tisa tukatoka saa moja na nusu ivi
mtoto katangulia nje wakati mimi namalizana na meneja... mzee natoa buku tatu yangu jamaa aniambia bado buku 9..Du! alafu anaongea kwa nguvu na corido za gesti zilivyo na mwang'wi nikaona leo yamenikuta.
Nikamshtua mtoto nje vipi unapesa kidogo uniongezee... ananijibu hata nauli ya kurudi chuo ananitegemea, kidogo nianguke kwa presha.
Fasta fasta nikajifanya naongea na simu kumbe namfata mangi muuza chips barazani... nilikua nina Nokia kwa kipindi hicho ilikua ina thamani kama ya laki 2 unusu... nikatoa line yangu nikamwambia mangi anipe pesa.
Akasema hana shida ya simu ila kwa kunisaidia atanipa elfu thelathini kesho nimrudishie hamsini.
Basi nikavuta mkwanja nikalipa gest na mtoto nikamvutia buku kumi... akaniuliza hny umepata wa pesa.
Nikamwambia kuna jamaa nilimpigia alikua karibu ndo ameniletea.
Mpaka leo ni mke wangu na tuna watoto watatu hajawai kujuaga niliuza Nokia kwa elfu thelathini kulipia gest na nauli yake.
THIS IS TRUE STORY.
mimi na msela wangu,tulifika club tukakutana na mashori wawili tukanywesha,ilipofika mda wa kwenda kupanjuka wakatupeleka guest ambayo wamezoeleka,kufika wakaanza kutupiga mkwara eti wao ni ma afande tuwambie sisi ni wa wapi na tunafanya kazi gani. Tukawapoza na maneno matamu tukaigia room double beds.wakagoma kutoa mchezo eti tulale kwanza,walipopitiwa na usingizi wa pombe, tukajichukulia simu zao nne, ki ipod.na kusepa nazo.tukapanda magari ya kuja sirari border hii ilitokea kisii kenya.true story.cheza na mtz wewe.
Mimi niliacha simu gesti, meneja aliniambia gest buku tatu mimi sikumuelewa kumbe ni kwa lisaa.
Bajeti yangu ilikua buku kumi na tano kila kitu.
Ilikua J'pili moja mtoto kanipigia simu anakuja getto. Siku hiyo ilikua noma maana mwenye nyumba anashinda nyumbani na kodi yake nshapitisha mwezi na nusu hivyo lazima angenikoromea.
Akili ya haraka haraka ilikuja niingie gest za uchochoroni. Saa saba na nusu hivi pale studio kituoni mtoto kashuka anaona tunaelekea kusiko.. kuniuliza kulikoni nikamwambia getto soo maji hamna alafu choo kinatoa harufu.
Tukafika hiyo gest kwa nje kuna mangi anakaanga chips kuku. Kuwa na uakika nikaenda kuuliza chumba nikaambiwa buku tatu ila nisubiri kidogo ataniita.
Wakati tunasuburi nikaagiza kuku chips 2 nikaona ngoja nipige na kamzika kadogo ka konyagi ili kuongeza kasi.
Mtoto alipiga soda yeye. Mangi kuleta bili nikakuta ninabakiwa na buku nne unusu, ambayo bado niliona nika vizuri kutokana na bei ya gest.
Meneja akanishtua tukaingia ndani... basi siku hiyo nilipiga gemu balaa. Tuliingia kwenye saa tisa tukatoka saa moja na nusu ivi
mtoto katangulia nje wakati mimi namalizana na meneja... mzee natoa buku tatu yangu jamaa aniambia bado buku 9..Du! alafu anaongea kwa nguvu na corido za gesti zilivyo na mwang'wi nikaona leo yamenikuta.
Nikamshtua mtoto nje vipi unapesa kidogo uniongezee... ananijibu hata nauli ya kurudi chuo ananitegemea, kidogo nianguke kwa presha.
Fasta fasta nikajifanya naongea na simu kumbe namfata mangi muuza chips barazani... nilikua nina Nokia kwa kipindi hicho ilikua ina thamani kama ya laki 2 unusu... nikatoa line yangu nikamwambia mangi anipe pesa.
Akasema hana shida ya simu ila kwa kunisaidia atanipa elfu thelathini kesho nimrudishie hamsini.
Basi nikavuta mkwanja nikalipa gest na mtoto nikamvutia buku kumi... akaniuliza hny umepata wa pesa.
Nikamwambia kuna jamaa nilimpigia alikua karibu ndo ameniletea.
Mpaka leo ni mke wangu na tuna watoto watatu hajawai kujuaga niliuza Nokia kwa elfu thelathini kulipia gest na nauli yake.
THIS IS TRUE STORY.
sasa hapo ukaudhu uko wapi mkuu wangu?