OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Miaka michache iliyopita nilipata kazi ya mkataba, nikawa nakunja milioni moja kwa mwezi, nikaona maisha si ndio haya. Bahati mbaya nikaangukia kwenye mikono ya watoto wa mjini, laki laki zilikuwa zinatoka kama vile njugu, mara ohoo nikasuke, mara nimeichoka hii Tecno nataka samsung, mara nikanunue nguo baby, yaani pesa nilikuwa nazitumbua tu, full kula bata na mademu plus mitoko, kwa mwezi nilikuwa naenda ATM hata mara 5 na nikifika nadraw kuanzia laki mbili.
Mwisho wa siku mkataba unakuja kuisha nkajikuta sina kitu, hakuna hatua niliyopiga, Mademu wote wakanitosa nikajikuta nipo zero akili za kichwa cha juu ndio zikarudi mpaka leo nikikumbuka huwa najiona mpumbavu kabisa.
Toa ushuhuda na wengine wajifunze!