Umewahi kuingizwa mjini?

Umewahi kuingizwa mjini?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Kisa cha jamaa yangu mmoja aliwahi kunihadithia miaka kadhaa iliyopita,

Katika pilika pilika za maisha alikuwa akiendesha baiskeli aina ya Phoenix akawa amepita njia moja hivi ambayo ina kauchochoro, alipita kwa sababu ilikuwa shortcut ya kwenda mjini,

Hakufika mbali mara akaona pesa zimefungwa na rubber band ikabidi ashuke faster ili aziwahi, mara akatokea jamaa akamwambia nimekuona inabidi tugawane pasu kwa pasu,

Jamaa akiwa bado ameshika zile pesa mara wakatokea vijana wengine wawili wakamvutia uchochoroni hapo akiwa amepigwa roba ya mbao yani hafurukuti.

Wale jamaa wakakomba kila kitu vikiwemo saa, simu, viatu nk bila kusahau baiskeli nayo ikaenda, wakamfunga jamaa mikono na miguu wakamjazia matambara mdomoni ili asipige kelele,

Alikuja kupata msaada baada ya masaa matatu kuna mama alikuwa akikusanya kuni ndipo akamuona na kumsaidia. Kumbe zile pesa zilikuwa mtega, hakika mjini shule.
 
Kuniingiza mjini siku hizi ni ngumu sana kwa sisi tulopitia mengi
 
Back
Top Bottom