Umewahi kujiuliza kwanini viwanda havitengenezi bidhaa za kudumu? Yani mfano zitengenezwe tairi za magari zisizoisha.

Umewahi kujiuliza kwanini viwanda havitengenezi bidhaa za kudumu? Yani mfano zitengenezwe tairi za magari zisizoisha.

youngkato

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
3,319
Reaction score
3,097
Umewahi kujiuliza kwanini viwanda havitengenezi Product za kudumu? Yani mfano zitengenezwe tairi za magari zisizoisha.

Dawa ya meno inayozuia kabisa meno yasiharibike.
Kiwanda cha nguo zisizochuja kabisa?

Huo uwezo wanao ila hawawezi kufanya hivyo...! Kwanini?

Mwaka jana nilikutana na jamaa mmoja Mentor mzoefu sana wa online! Akaniuliza Hiyo huduma yako una uhakika mteja akiinunua atarudi tena? Au ndo mmemalizana biashara imeishia hapo?

Mwanzoni sikuelewa ila baada ya muda nikagundua. Ni gharama sana kumpata mteja mmoja.

Sasa umetumia gharama kubwa au nguvu kubwa kumtafuta huyo mteja Ila, Akishanunua hauna kazi naye tena (huko ni kupoteza rasilimali)

Umewahi kujiuliza kitu gani kinawekwa kwenye soda au bia ili mtu awe addicted aendelee kunywa kila siku?

✅Hizi ni njia ambazo unatakiwa kuzitumia ili kumfanya mteja wako arudi kila siku

1. Toa huduma ambazo mteja wako anazihitaji kwenye hiyo kazi yake

Mfano huduma za Victoria Agency

Mfanyabiashara hata aende wapi nina uhakika atahitaji hizi huduma

Nilisikia interview moja ya @moodewji anasema

Anatengeneza bidhaa ambazo
Mtanzania akiamka asubuhi.

Atapiga mswaki, atatumia kiberiti, atapanda boda, atakula, atatumia mafuta, yani mpaka anaenda kulala anatumia bidhaa za mo tu.

Je biashara yako inamfanya mteja arudi?

Kumfanya mteja arudi sio tu kutoa huduma nzuri. Ni kumfanya akichukua huduma moja, kesho achukue huduma nyingine.

Kwa kutoa Offer tofauti tofauti, huduma tofauti, katika package moja.

Mfano mwingine ni kwanini mitandao ya simu, hawatoi kifurushi cha lifetime, au mwaka mzima?

Najua jibu unalo

They need your money

Wanataka kesho uje na pesa nyingine.

Sasa kwanini wewe kwenye duka lako la nguo unauza nguo tu, Unasahau huyo mteja anahitaji huduma nyingine.

Mfano mwingine ni kwanini wanaotengeneza dawa ya mbu ya kuchoma haiui mbu inawafanya wazimie badae wanaamka.

Au ya kupuliza haikai muda mrefu?

Lengo kubwa ni urudi kununua dawa yao.

Angalia mahitaji ya mteja wako, kaba kila angle.

Kuna njia nyingi za kufanya katika biashara yako ili kumfanya mteja wako arudi kila siku.

Mteja anapatikana kwa gharama. Ni lazima ufanye akae na wewe.

Kama hujui ufanyeje au uongeze nini kumrudisha mteja wako

Karibu ofisini
 
Back
Top Bottom