Wanaume hawa jamani yaani nyie acheni tu. Nilikuwa na ex bf wangu tulipendana kweli, ikafika kipindi nikaenda kusoma nje ya nchi. Mara ya kwanza mawasiliano yalikuwa mazuri baada ya muda mwenzangu akaaza lawama, mara oh we umeenda huko najua utanipiga kibuti tu. Usipotuma sms siku moja mwenzangu anapata sababu, ohh hujatuma sms ushaamua kuniacha.
Ikafika kipindi akaacha kabisa mawasiliano, na mie nikaona isiwe shida nami nikachuna.
Mungu jalia nikamaliza masomo na kurudi home, baada ya kurudi tukaonana na kipindi hicho kumbe tayari alikuwa kaoa.
Tulivyoonana tu, mara tena akaanza kuleta za kuleta. Ohh unajua nisamehe mie bado nakupenda, naomba turudiane. Mie nikamwambia mbona umeoa? Akajibu nilioa kwa kuwa rafiki na ndugu walisema kwamba mwanamke akitoka nje ya nchi sio wa kumsubiria, eti anaweza kusubiri halafu mie nikamtosa. Nikamwambia usicheze na ndoa ilimradi ulioa we endelea na ndoa yako na tubaki marafiki tu.