Umewahi kukutana na tukio hil: Uchumba kutaka kuvunjika, ilikuwaje na mliokoaje ili usivunjike?

Umewahi kukutana na tukio hil: Uchumba kutaka kuvunjika, ilikuwaje na mliokoaje ili usivunjike?

Duh aiseee soon wakataa ndoa watasajili mwanachama mpya. Jamaa hakutakiwa kusamehe bila kufahamu yanayoendelea kati ya binti na ex wake
Kwa mujibu wa maelezo hakuwa ex..alikuwa mpenzi msaidizi
 
Screenshot_20230502-231451_Quora.jpg
kampe hongera wifi yako
 
Usimuoe huyo mwanamke utakuja kujuta ndg hataachana na huyo bwana kamwe wataaakuwa wanaiba
Sasa lazimisha uone yatakayokukuta
 
Sisi tulivunja uchumba wa kaka yetu wifi mtarajiwa alikua hatupigii simu.
 
Hivi Kuna wanaume wanaoa hawajui kuwa wanawake hao wanaoa wanatamaniwa Kama walivyowatamani na wao. Ama yeye muoaji hajawahi tiaaa nje huko kabla ya kuoa?

Hakuna ukamilifu yaani wewe una weakness Ila unataka mwenzako awe perfect
 
Jamaa Yako ni fala sana,...huyo mwanamke siyo wa kuoa milele ila kama haamini aoe.
 
Ilikuwa mwaka jana mwezi wa 5.

Binti mmoja karibu na home alichumbiwa na kijana mmoja aliyekuwa mpenziwe kwa miaka 2 hivi.
Baada ya kulipa mahari taratibu za ndoa zikaanza, sasa siku moja walikuwa maeneo ya makumbusho walikuwa wanafanya shopping ya mahitaji yao nafikili ilikuwa kwa ajili ya maandalizi ya ndoa.

Walifika kwenye duka moja kijana akamwambia binti simama hapa ngoja niingine kwenye hili duka niulize kitu flani baada ya kuingia kwenye duka, Kukawa na mabinti wawili nje ya duka wakakutana na mkewe mtarajiwa huku jamaa anawaangalia. Kwa mshangao mkewe mtarajiwa akashituka, kwa mshangao kuwaona wale mabinti wawili kwa furaha kubwa sana mpaka mabinti nao wale walifurahi sana.

Mabinti wawili wakapiga sauti wifi wifi wifi Habari tumekuona siku sana na kukumbatiana kabisa na mke mtarajiwa nae kwa furaha sana aliwakumbatia. Na mabinti wawili wakawa wanamlalamika siku hizi huji hata home kujakututembelea bwana hata mama anakuulizia.

Jamaa yake akawa anaangalia mchezo na wale mabinti wawili hawajui, huku jamaa anasikia kila kitu. Mabinti wawili wakamwambika kuwa kaka anakuzingumzia sana home maana naona mnakutana mara kadhaa, Kaka yetu anasema sana home. Baadae mke mtarajiwa alijishitukia coz jamaa alikuwa anamcheki na kusikia kila kitu.

Baada ya tukio lile pale jioni ukaibuka ugomvi mkubwa tuu kati ya binti na jamaa, Mume mtarajiwa akafikisha mpaka home nia ni kuvunja uchumba , huku dada kilio kwao wakawa wanamuuliza shida ni nini alisimulia kila kitu kwao walimshangaa sana. Mshenga ikabindi awasiliana na wakwe watarajiwa kuwa muoaji anataka kuvunja uchumba ila ni vyema tukutane tusuruhishe. Wakakubaliana kusuruhisha tulio lile.

Ila waliamua Kuwaita wale mabinti wawili nyumbani kwao, mabinti wale pasipo kujua wameitiwa nini si wakaja bhana. Wakakuta tu kuna kikao na binti machozi kama yote. Waliongea na kuwaambia wale mabinti kuwa huyu sio wifi yenu na iwe mwisho leo kumtafuta na kumuita wifi na hata mama yenu mkamwambie huko.
Ila baadae waliamua kimpigia simu na jamaa kumueleza. Baadae mabinti waliomba msahama na kuondoka.

Wakayamaliza kihivyo. Kama wewe umewahi kutana na tukio kama hilo umlilisiruhisha kivipi.

KARIBUNI.
Ilikuwa Mwaka Jana Feb. 2022 Kuna Rafiki yangu (MSUKUMA) alikutana na Tukio moja la kimahusiano. Alikuwa na Wapenzi wawili.

Tuseme kwamba Binti mmoja anakaa Mtaa A(ambaye ni MHEHE kikabila) na mwingine anakaa Mtaa B(ambaye ni MBENA kikabila)

Mpenzi wa Mtaa A akawa amemtolea POSA kwa ajiri ya kumuoa.

Mpenzi wa Mtaa B kumbe alikuwa kashatoka naye akamtia MIMBA.

Kijana akajawa na Mawazo yupi aoe na yupi asioe. Kumbuka Mpenzi wa Mtaa A ametolewa Posa na Mpenzi wa Mtaa B ana ujauzito.

Ikabidii ashirikishe wazee wake na watu wa Busara. Akashauriwa AOE binti aliyempatia UJAUZITO. Hadi sasa ameshaoa huyo binti na tayari wana mtoto wa Kiume.

Kijana alienda kwao na Mpenzi wa Mtaa A akaomba msamaha sana, akatoa na FAINI ya LAKI SITA (600,000) kama kutoa mkosi kwenye ile Familia.

Familia ya Mpenzi wa Mtaa A wanamchukia hadi wa Leo huyo Kijana.

Wazazi wa Binti wa Mtaa A walimuomba huyo kijana amuoe binti yao hivyo hivyo kijana akakataa sababu Dini ya kikiristo hairuhusu kuoa wake wawili.

Hadi wa leo Mpenzi wa mtaa A hajaolewa.

Ungelikuwa ni wewe umeombwa ushauri na huyo kijana, kijana ungelimshauri vipi hapo ?
 
Back
Top Bottom