Umewahi kukutana na tukio hil: Uchumba kutaka kuvunjika, ilikuwaje na mliokoaje ili usivunjike?

Duh aiseee soon wakataa ndoa watasajili mwanachama mpya. Jamaa hakutakiwa kusamehe bila kufahamu yanayoendelea kati ya binti na ex wake
Kwa mujibu wa maelezo hakuwa ex..alikuwa mpenzi msaidizi
 
Usimuoe huyo mwanamke utakuja kujuta ndg hataachana na huyo bwana kamwe wataaakuwa wanaiba
Sasa lazimisha uone yatakayokukuta
 
Sisi tulivunja uchumba wa kaka yetu wifi mtarajiwa alikua hatupigii simu.
 
Hivi Kuna wanaume wanaoa hawajui kuwa wanawake hao wanaoa wanatamaniwa Kama walivyowatamani na wao. Ama yeye muoaji hajawahi tiaaa nje huko kabla ya kuoa?

Hakuna ukamilifu yaani wewe una weakness Ila unataka mwenzako awe perfect
 
Jamaa Yako ni fala sana,...huyo mwanamke siyo wa kuoa milele ila kama haamini aoe.
 
Ilikuwa Mwaka Jana Feb. 2022 Kuna Rafiki yangu (MSUKUMA) alikutana na Tukio moja la kimahusiano. Alikuwa na Wapenzi wawili.

Tuseme kwamba Binti mmoja anakaa Mtaa A(ambaye ni MHEHE kikabila) na mwingine anakaa Mtaa B(ambaye ni MBENA kikabila)

Mpenzi wa Mtaa A akawa amemtolea POSA kwa ajiri ya kumuoa.

Mpenzi wa Mtaa B kumbe alikuwa kashatoka naye akamtia MIMBA.

Kijana akajawa na Mawazo yupi aoe na yupi asioe. Kumbuka Mpenzi wa Mtaa A ametolewa Posa na Mpenzi wa Mtaa B ana ujauzito.

Ikabidii ashirikishe wazee wake na watu wa Busara. Akashauriwa AOE binti aliyempatia UJAUZITO. Hadi sasa ameshaoa huyo binti na tayari wana mtoto wa Kiume.

Kijana alienda kwao na Mpenzi wa Mtaa A akaomba msamaha sana, akatoa na FAINI ya LAKI SITA (600,000) kama kutoa mkosi kwenye ile Familia.

Familia ya Mpenzi wa Mtaa A wanamchukia hadi wa Leo huyo Kijana.

Wazazi wa Binti wa Mtaa A walimuomba huyo kijana amuoe binti yao hivyo hivyo kijana akakataa sababu Dini ya kikiristo hairuhusu kuoa wake wawili.

Hadi wa leo Mpenzi wa mtaa A hajaolewa.

Ungelikuwa ni wewe umeombwa ushauri na huyo kijana, kijana ungelimshauri vipi hapo ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…