Umewahi kula kitu gani ambacho hukuwahi kufikiria pale njaa ilipokukamata kisawa sawa

Umewahi kula kitu gani ambacho hukuwahi kufikiria pale njaa ilipokukamata kisawa sawa

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Nakumbuka kuna kipindi nlikuwa chuoni hela yangu ya matumizi kwa mwezi ndani ya siku 10 hivi, nlimpigia simu mhusika aliekuwa akinutumia pesa jibu nlilopewa ni "mbona mapema sana subiri mwisho wa mwezi".

Hapo tayari nlikuwa na madeni kadhaa yani kukopa ilikuwa tabu.

Basi ikifika mchana nlikuwa naenda sehemu flani nachuma mapera ndio nakula. kuna baadhi ya sehemu nilianza kufukuzwa wakidai namaliza sana mapera, kiukweli ilikuwa aibu.

Kama mnavyojua matunda yanasagika haraka sana njaa inakamata baada ta masaa machache hivyo inabidi uongezee mlo kidogo stable, jibu kikawa mihogo.

Kuna elf 10 nilipata basi ndio ikabidi niipigie bajeti, jioni ikifika nlikuwa natembea mwendo wa lisaa kwa mguu naenda mbali sana huko nikiwa na chupa yangu ya maji nliyochota bombani naenda kula mihogo ya 400, kesho yake ikifika mchana kama kawaida naenda kukwea mipera.

Changamoto kubwa ilikuwa siku nyingine pera likijikusanya na mihogo huko chooni ilikuwa ni shidaaah!!

Sitakuja sahau kile kipindi.
 
Nakumbuka niliwahi kufukua mbegu ya mahindi ardhini nikayala ikiwa mbichi sababu ya njaa kali niliyokuwa nayo. Njaa sio mchezo hadi magamba ya puani nilikuwa natoa nakula sababu ya njaa.
Mkuu hiyo sio njaa, hiyo ni SHIDA
 
Kipindi pia niko chuo pesa ilinikatia. Gheto kuna unga kidogo usiotosha ugali, sukari na gesi tu. Ilikua ni mwendo wa uji tu.

Sitasahau kile kipindi asiee na huo uji ni mara moko tu ili nisife njaa.
 
Aisee hatar sana, nilishawahi pigwa na njaa nikawa sitaki Tena kuoga kuogopa nikienda bafuni nitazimia.
 
Nimeandikaaaaa we, ila nikaamua kufuta. Kiufupi niliwahi kula mihogo ikiwa ndio chakula ambacho namudu bei yake pekee hadi ilifika hatua nikisikia harufu ya mihogo napata kichefuchefu. Dah! Bajeti kwa siku ni elfu moja, unaishi Buguruni Rozana unafanya kibarua Ubungo ambako kila siku uende na kurudi kwa mguu. Dah! Mungu anatutoa mbali.
 
Back
Top Bottom