Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili upate huduma fulani?

Hii ya TANESCO nimesikia watu wengi wanasema. Pole sana Mkuu
 
Ilinitokea nikiwa Kahama wakati natafuta Cheti cha Kuzaliwa.

Niliambiwa kwa utaratibu wa kawaida utachukua muda, lakini nikijiongeza itachukua siku 2.

Kwa kuwa ilikuwa ni dharura, ilibidi nitoe japo kidogo, kesho yake nikapata cheti changu.

Nasikia pia NIDA kuna urasimu mkubwa unaosababisha watu wengi waingie kwenye mtego wa kutoa rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…