Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili upate huduma fulani?

Umewahi kulazimika kutoa rushwa ili upate huduma fulani?

  1. Naam, niliwapa Tanesco kufunga umeme
  2. Masoko ya Serikali kupata eneo ndani ya jengo
  3. City, taa ya gari niliyoiegesha ilining'inia, kusimama kuiweka sawa haooo.. Sio watu
  4. Hospitali za Serikali
  5. Halafu kuna haya madude mawili, yanaitwa polisi na mahakama. Bila rushwa hutoboi na jambo lako..
Hii ya TANESCO nimesikia watu wengi wanasema. Pole sana Mkuu
 
Ilinitokea nikiwa Kahama wakati natafuta Cheti cha Kuzaliwa.

Niliambiwa kwa utaratibu wa kawaida utachukua muda, lakini nikijiongeza itachukua siku 2.

Kwa kuwa ilikuwa ni dharura, ilibidi nitoe japo kidogo, kesho yake nikapata cheti changu.

Nasikia pia NIDA kuna urasimu mkubwa unaosababisha watu wengi waingie kwenye mtego wa kutoa rushwa.
 
Back
Top Bottom