Umewahi kulia kisa kusemwa na mkeo/mpenzio?

Umewahi kulia kisa kusemwa na mkeo/mpenzio?

Hizi post za wala urojo zinachekesha [emoji23][emoji23].

Yaani wewe ni kichwa cha familia alafu uanze kutoa machozi, duuh.

Kumbuka wewe ndio wakuilinda familia yako mkuu, wewe ndio nguzo yao na tegemeo lao, hata jambazi akiingia ndani wewe ndio uwe mtata hapo sio kujificha nyuma yao.

Mwanaume halii mbele ya mke wake mkuu, ni udhaifu, acha umama.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi mwenyewe nimetoka kulia [emoji24][emoji24][emoji24]sasa hivi baada tu ya kuniambia eti ananipenda sana. Jana pia nililia [emoji24][emoji24][emoji24]baada ya kuniambia eti ameniota usiku.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hapana sio itashusha uanaume wako . tena unaweza ukasemwa kwa busara ukalia haswa. Ukaona mke anavyokujali hataki upotee

Hii iliwahi tokea once kwa mume wangu kuna kosa alikua anafanya si vyema kuanika hapa nikamfahamisha kwa mara ya kwanza akaachana nayo. Kama unavyojua shetani nae hapumziki akarudia nikamuonya nakuonesh kuchukizwa haswa na kumweleza kabisa ikitokea tena jua basi huu utakua mwisho wetu , ikajirudia tena ile siku nilikasirika sana huku machozi yananitoka kwa hasira niliswali rakaa mbili kumtaka Mola wangu msaada, sikuwahi kuona majuto yale aliyojutia aliamka na kupiga magoti na kuniomba msamaha kisha akaenda kuswali rakaa mbili akaja akaomba msamaha tena na vilio ikawa anaswali rakaa mbili kwa mola wake kisha anakuja kulia nami nimsaamehe. Toka sike ile hakuwahi kurudia namshukuru Mungu nae anashukuru kua tunasaidian ktk kuamrishana mema na kukatazana mema


Ila kiubinadamu nilitamani nipate kivideo cha vile alivokua analia na kuomba msamaha maana ni mbabe noma kwa hyo kumbananisha pale ilikua shangwe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nini kulia watu mpka wanazimia hasa mpenzi wako mwwnyewe akiwa mzaramo
 
Back
Top Bottom