mikatabafeki
JF-Expert Member
- Dec 29, 2010
- 12,770
- 4,656
Ahahahahahaah!! Pole sana..dah mmi siku hiyo mitaa ya tabata relini sina hili wala lile coz ni karibu na home nikatoka tu kunyoosha miguu nikashangaa wamenivice wakanisachi hawakukuta hata sh 5 si wakaanza kunipiga eti kwanni hautembei na hela nikitaka kujibu kibaao
Hawa jamaa wana roho za kikatili, wanaweza kuua au kuacha mtu na majeraha kisa simu au hereni.tandika sokoni najiendea zangu job. ili naingia kwa daladala tu nikahis kuvutwa chini kumbe chaliii zshakwapua simu. aaah wapi sikukubali nikageuka kama umeme nikamkwida shati.. natetemeka mwili mzima. looh nikawa napaza sauti wee kuona noma akanipa simu huku ananchimba biti. si mekupa simu sasa kelele za nini. looh hata ile gari sikupanda tena nkahamia ingine.

siku nyingine ndani ya gari tuko kwenye foleni. namwona mtu kwa side mirror nkajua anapita. loooh ile gari imesogea kidogo yani heren zilivuliwa kama kafinya tu. na simu kwapu. hawa watu loooo siwapendi kama nini.
Ahahahahaah!! Eti kama movie vile.....Ilikuwa mida ya saa 3 asubuhi pale relini karibia na kurasini beach, yaani kama movie vile kisimu changu kikakwapuliwa alafu mwenzangu akapokonywa pochi! We acha tu ndugu, nikimkuta kibaka anapigwa wala simuonei huruma kabisa!
Dah pole sana nahisi ulipata kipigo cha hatari.Ila last year, May.

Huku Keko Mwanga, kuna sehemu inaitwa Danger na Nyingine n Walunguli. Nilikuwa napta mitaa mitaa ya Danger nikatoa kisimu changu cha torch, mshkaj mmoja akanisogelea akaniambia maliza kuongea utoe lain yako utugee simu yetu. Nilipuuzia, nlhs utan. Baada ya kumalza kuongea nkarudsha simu yangu mfukon.

Kilichontokea had leo sina hamu ya kupta maeneo yao.

Wale sio BINADAMU

dah mmi siku hiyo mitaa ya tabata relini sina hili wala lile coz ni karibu na home nikatoka tu kunyoosha miguu nikashangaa wamenivice wakanisachi hawakukuta hata sh 5 si wakaanza kunipiga eti kwanni hautembei na hela nikitaka kujibu kibaao
Pole sana.....hawa vibaka si wa kuhurumiwa hata kidogo!Visa vingine hadi vinachekesha kwa masikitiko. Kweli tatizo la vibaka ni kubwa sana Nchi hii karibu kila sehemu isipokua labda Makete tu maana huko kuna imani za kishirikina balaa. Nasikia ukidondosha hela yako kesho utaikuta palepale hamna atakaegusa. Natamani hiyo teknolojia yao wangeiweka kwenye vitabu itusaidie na sie wa maeneo mengine.

Mie nimeondokewa na Mjomba wangu mwaka huu mwanzoni huko mbeya, alikua nyumbani kwake na mkewe majira ya saa 2 usiku maeneo ya airport akapata msg ya ugonjwa toka nyumbani kwa mama yake, hakuwa na credit kwy simu akatoka kwenda dukani kununua vocha umbali kama wa dkk 5 hivi. Akiwa anaweka vocha pale dukan kumbe vibaka walikua pembeni wanamuangalia, alipotoka tu kwenda home, kuna kijinjia chenye giza wakamvamia wakitaka simu, alikua na ubavu sasa katika vurugu ile walipoona wanazidiwa wakamzushia mwizi wa simu kamkaba mtu. Basi raia walitoka kwa wingi wakampiga sana mmoja wao akawasihi wammulike coz alikua kesha anguka chini na kapoteza faham, ndipo wakagundua ni jirani na wakati wananchi wanaingilia kati vibaka walichomoka mmoja baada ya mwingine. Alichukuliwa kwenda police ili apelekwe hosptali lakini alipofika police ali fariki bila hata kutoa kauli yeyote. Ina niuma mpaka leo hii.

Poleni wote mliokumbwa na maswahibu ya hawa vibaka.
Kweli ganja mbaya, wakiwa wengi namna hiyo hata kujitetea huwezi!

GANJA LINAWAONGOZA,KAMA LEO NIMESKIA RWDION KUWA JANA USIKU KUNA GUEST IMEVAMIWA NA VIBAKA KAMA 30 WATU WAMEJERUHIWA NAWAMEPORWA NA WENGINE WAMELAZWA HOSP YA MWANANYAMALA