Wahanga wengi wa manynyaso ya mabosi ni kwenye kampuni binafsi, biashara za watu binafsi, kuajiriwa kwa baadhi ya wahindi na wachina, n.k
mkasa wangu
kuna kipindi flani nikiwa mtaani baada ya kumaliza chuo nilipewa connection sehem ya kujishikiza kampuni binafsi mshahara laki 2, yani kulikuwa na huyo msimamizi wetu wa kazi (supervisor) ambae ni kero tupu, hakuweza kuona lolote zuri nalofanya hata nipige kazi kwa bidii namna gani.
alikuwa ana lugha kali sana lakini bado hakuwahi kuitumia kwangu maana nilifanya kazi kwa uadilifu, sasa kuna siku moja muda wa lunch nilichelewa kufika kazini kama kwa dakika 10 hivi, nilimkuta msimamizi akiwa ananisubiria mlangoni na amenipania si mchezo.
akaanza kunigombeza na kunitolea lugha chafu, alintukana tusi moja zito kidogo lililonifanya nimrudishie fadhila, nilimpiga bonge la kibao,, paaaaa!!! kimyaaaa, vimaneno maneno vyote vimemwishia!! muda huu wote niliwasha voice recorder ya kwenye simu yangu.
tuliitwa ofisini kwa bosi, yeye ndie alieanze kuongea basi akaanza kutia chumvi kwamba wala hakunitukana ila nimempiga, mimi mda wa kujitetea niliweka simu mezani nika play kilichorekodiwa ile lugha yake ya kunigombeza, tusi na kibao matata nilichomnasa.
Bosi alinionya kitu hicho nisurudie na kwamba siku nyingine nilalamike kwake.
yule msimamizi kwa ile lugha yake kali + tusi alisimamishwa kazi mwezi mzima, mimi nilifanya kazi mpaka nilpopokea mshahara wa mwezi huo nikandoka ili kuepusha makubwa ambayo yangetokea endapo angerudi, nilikuja kuambiwa kwamba alishushwa cheo.
kuna siku nikiwa kwenye gari yangu nilimuona, nilimpigia honi nikampungia mkono huku nikitabasamu