Umewahi kuona umuhimu wa Himid Mao kwenye Timu ya Taifa?

Conclusion ya Wabongo watakuambia NDUMBA inatumika
 
Himid
Kwangu ni mchezaji mzuri sana aliyepitia ngazi zote za uchezaji, alianza kucheza Copa coca ya ile kwanza kisha achaguliwa kwenye kikosi kilichoenda Brazil na kubeba tuzo
Baada ya kurudi hapo akaendeleza kucheza timu za vijana za ngazi zote hadi timu ya Taifa uko pote alifanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji wanaoanza kwenye vikosi vya kwanza na kwa walimu tofauti tofauti
Azam fc washaletwa viungo wengi sana lakini himid aliweza kupata namba pia
Leo akijitokeza mtu na kunambia Himid hajui mpira nitamshangaa sana na kumuona yeye ndio hajui
Mana haiwezekani makocha zaisi ya 15 wote kumuamini na kunpanga tena wengine kutoka nje ya Nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Baba ake ana influence Hadi kwa Mapharaoh Tena timu 2?
Basi mzee Mkami ni noma sana
 
Wale wanaosema Ninja anabebwa na Baba ake watakuwa na chuki nae tu, kuna wachezaji wangapi wa zamani ambao Baba zao walikuwa wachezaji wazuri sana lakini wameshindwa kufanikiwa kwenye soka
Binafsi naamini Himid anasonga mbele kwa uwezo na nidhamu yake ya juu katika soka
Baba ake alikuwa Star wa Pamba ya Mwanza na Mtibwa alipoenda kumalizia soka lake
Himid ni star wa Azam na timu za Misr

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizo timu ambazo wewe unaziona ndogo, basi zinagombaniwa na wachezaji wa nchi nyingi za kiafrica wapate nafasi japo ya kusajiliwa...
Kumbuka ya kuwa ligi kuu ya Misri ni moja kati ya ligi bora tatu za Africa
Kwenye kupata team sio kupanga team.... Fuatilia team anazo chezea ni team ndogo angekua kua Bora si angechaguliwa na team kubwa.....

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fletcher sawa, ila J.s park umetudanganya
 
Egypt anacheza kitimu chenye hadhi kama Ndanda

Sent using Jamii Forums mobile app
Ligi daraja la pili kwa Mapharaoh ni Bora na Ina ushindani kuliko hii ya Bongo.
Timu ya daraja la kwanza huko Egypt inazifunga hizo timu zenu 2 za kariakoo home and away na timu ya mwisho huko kwenye Egypt Premier League ikija kucheza ligi ya bongo inachukua ubingwa fresh kabisa
 
Yanga waliwapiga Al Ahly waliokuwa mabingwa au umeanza kufuatilia mpira baada ya Covid 19 kuingia?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuna mtu ambaye huwa haoni shughuli anayofanya mtu kama casemiro pale madrid
Kante wote hao n wakata umeme na tunaona wanachofanya wakiwa uwanjani
 
Inonekana Himid Mao hatojua mpira mpaka akacheze Simba au Yanga!!

Himid nikiungo wa Shoka asiekua na marembo marembo mtibuaji japo simporaji mzuri wa mipira, ni direct player zaidi. Work rate yake ndio inayombeba, anajituma na asieonesha kuchoka.

Niaina ya wachezaji wa kiafrika kabisa, mgumu haswaa,ukakamavu na nguvu ya kushindana hua unawavutia makocha .

Najua siku akicheza Simba au Yanga atapewa sifa zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Himid Mao ni miongoni mwa wachezaji wachache ambao wamekulia katika misingi ya soka humo unamkuta Tom ulimwengu pia
Himid Mao ni kiungo ambae hutumiwa zaidi katika mechi znazohtajika kukaba zaidi kutokana na asili yake ya "upunda"alokua nao uwanjani
Ni wale middle wachache wanaocheza basic football haina mambo mengi ukiwa unacheza namna hii kibongobongo tunasema haujui mpira kundi hilo watakuwekea Tom Ulimwengu John bocco ajabu wakija makocha bongo wanaanza kuwaona hao wachezaji kabla ya wengne wote
Mashabiki wengi wa mpira bongo hatuuishi mpira watakwambia Beno Kakolanya ametimia zaid kulko Aishi wanajua GK ni kudaka tu mpira kama nyani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Himid Mao Mkami a.k.a Ninja ni miongoni mwa viungo wakabaji bora kabisaaaa Tanzania
Tena ni bab kubwaaaa, kiungo anaefika, na kucheza zile zoote ngumuuuu...
Basi tuu soka letu la kibongo liko kisengerenyumaaa
 
Ni kweli mkuu, ingekuwa issue ya kubebwa na dingi yake basi Haji Manara angefika mbali sana, lakini alishia kuwa mbeba jezi wa Kariakoo united.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…