Wacha kabisa hawa mafundi...
Wakati napauwa fundi alisema leta mbao kiasi flani nikaja na ileile idadi yake na mikaongeza hapo kidogo tena, fundi kapiga mbao plus na ile idadi yngu bado mbao zinahitajika kama PCs 15, kumuuliza anadai hajawahi fanya site kama hii adai hapo site kuna miujiza.
Nikaona huyu anacheza na akili yangu, nikampa option ya tufanyaje yeye bila kujua akasema tukaongeze mbao. Mbao ikaongezwa na mwendo ukaenda wa bati akaja na idadi yake na mwisho yakaongezwa 7 katika hiyo idadi yake. Twende kazi mwisho wa siku kuna gape tena kumuuliza anadai fundi aliyejenga sio mtu mzuri alikuwa anataka hiyo kazi iwe yake.
Kumuuliza suluhisho akasema twende dukani, tukaenda dukani akaja na idadi yake tena nikaongeza 5 kwenye yake na mwisho wasiku likabaki bati moja. Mbona mtu alilia mwisho wa siku anadai ela yake.
Nikamuuliza fundi hapo alikuwa nan kati ya mm na yeye, akasema yeye mkadiriaji wa material ni nani? Akasema yeye sasa nikamuuliza fundi akikosea kukadiri mara ya kwanza na mara ya pili hii hasara yakununua material ambayo unauziwa kwa retail na si wholesale nani anailipa, akasema ni mimi kwakuwa site ni yakwangu... Kilichofata aliondoka mweupe mfukoni atajua aliwalipaje vibarua wake izo ni additional cost ambayo yeye mwenyewe ndio alijitengenezea.