Umewahi kupata Madhara gani kwa kutumia Dawa ulizopewa Hospitali

Umewahi kupata Madhara gani kwa kutumia Dawa ulizopewa Hospitali

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Wadau, hebu tuelezane hapa kuhusu matumizi ya Dawa tunazopewa Hospitali. Kuna watu wamewahi pata madhara hasi baada ya kuanza kutumia dawa fulani wakitegemea kupata Tiba lakini badala yake zinapelekea Ugonjwa kuongezeka au kupata tatizo lingine zaidi
 
Duh kuna kitu kinaitwa aspirin junior au low aspirin wanapewaga wa mama wajawazito hata sana kiliniletea majonzi kwenye familia
 
Kwa upande wangu cijawai kupata madhara lakin nina ushuhuda maadhi ya watu nimeshawai kuwaona wakipata madhara
 
Wadau, hebu tuelezane hapa kuhusu matumizi ya Dawa tunazopewa Hospitali. Kuna watu wamewahi pata madhara hasi baada ya kuanza kutumia dawa fulani wakitegemea kupata Tiba lakini badala yake zinapelekea Ugonjwa kuongezeka au kupata tatizo lingine zaidi
Mm nasikitika sana. Na huwa ni maamuzi yangu naandikiwa dawa. Naamua kuzitupa nakunywa maji ya kutosha na mazoez mepesi na hupona. Labda tatizo serious nakunywa. Nadhani nimekwepa madhira mengi kwa kuepuka kunywa dawa ninazotilia shaka
 
Kuna binti alichanganya dawa kama 6, kuamka asubuhi hasikii...mpka leo kawa kiziwi!
 
Kuna mzee alikuwa anasema mazungu maongo tu wakimuandikia dawa mbili mara yatu yeye anakunywa moja mara tatu ( alishafariki).Bibi yangu alipata madhara ya kutokusikia alikunywa dawa ya malaria ilikuwa inaitwa kwinini.Alikuwa anadai anasikia kama wadudu wanapiga makelele masikioni.Kwa sasa ananafuu kidogo ila ndio upayuke haswaa.
 
Back
Top Bottom