Umewahi kupigwa roba mtaani? Weka kisa chako

Pole sana mkuu. Maisha yana mambo mengi. Tunamshukuru MUNGU, uhai na utu wako ulibaki salama.
Yaani acha tuu ndugu yangu sijui wangeniharibu utu wangu ingekuwaje,.maana wakati ule nilikuwa nikikumbuka lile tukio mwili mzima unasisimka nabaki kuweweseka tuu.. huyu YESU aliyeniokoa pale nitamtumikia milele 🙌
 
Yaani acha tuu ndugu yangu sijui wangeniharibu utu wangu ingekuwaje,.maana wakati ule nilikuwa nikikumbuka lile tukio mwili mzima unasisimka nabaki kuweweseka tuu.. huyu YESU aliyeniokoa pale nitamtumikia milele 🙌
Amina mtumishi. BWANA Yesu ni mwema sana.
 
Kuna jamaa humu alikabwa mpk wakabaji wakamkumbuka ati "huyu wa Jana!!" Wakamuacha akaenda..[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nmeikumbuka hiyo stori, nlichekaga sana
 
Unapenda kushika pumbu za wanaume wenzako utajageuzwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukatulingishia bwana!! Kumbe Ni we[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Lipia tangazo mkuu
 
Think like a thief act like a cop, utakua salama mitaani
 
Hawa waseng' huwa ni majasiri sana.Mwaka jana pale Zakhem Mbagala kama unaelekea kibonde Maji walinikabia mjeshi mmoja hivi,wakampora vyote na demu wake wakampoka.
Kumpoka ndio nini mkuu,au ulitaka kumaanisha kumbaka
 
Final ya uefa arsenal na Barcelona ni 2006. Acha uongo
 
Unaniua mbavu zangu😂😂😂
 
Yuko jamaa yangu toka Shy alikuja Dar kununua gari. Basi nikamtembeza show room kadhaa akachagua gari na kulipia. Sasa tukawa tunasubiri usajili na gari ifanyiwe service tayari kwa safari ya kurudi Shinyanga.
Sasa tuko pale Magomeni mapipa tunasubiri usajiliili jamaa aanze safari ya shy kesho Yake. Jamaa yangu akaamua aende kariakoo akanunue vijizawadi vya kupeleka Shy. Nikamwambia panda daladala yule mjinga akasema, Kariakoo si pale napaona, niharibu Mia nne ? Basi akaamua kutembea. Pale Jangwani mtakumbuka kulikua na viwanja vya mpira mbali na kile Cha YANGA. Basi baada ya kuvuka daraja jamaa akakatiza kwenye vile viwanja na wahuni walikua wanacheza mpira mida ya saa kumi na moja.
Sijui wahuni walimstukiaje jamaa yangu, maana walimpelekea mpira halafu wakaufuata Kama naye jamaa Ni mchezaji wa timu pinzani katika Ile hali walimuangusha Kama mwenzao tu huku wakiendelea kucheka.
Kuja kustuka kila mchezaji anaendelea na hamsini zake na kucheza mpira, jamaa yangu Yuko chini Hana hata Mia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…