Nilishaandika hiki kisa humuu si chini ya mara mbili, kuna watu wakiona watakumbuka uzi.
Mshkaji aliniamsha asubuhi subuhi (sijui usiku aliwaza nini) nimsindikize akapime pale temeke...
Nikamuuliza mzee kulikoni, akasema we twende mi najiamini sio kama wewe....
kufupisha
Sisi ndio wa kwanza pale, tulifika hata bado hawajafungua, mda wakufungua tukawa tumefika watu Saba , Kimbembe kilianza Pale nesi aliposema haya Aingie wa kwanza.....
Jamaa anasukuma wenzake kwenye bench, Anajitia kuchati, Akaambiwa na mzee mmoja
"kijana wewe si ndio wa kwanza nenda"
jamaa akasema
"Aaaah hamna shida mzee wangu yeyote naweza mpisha aende"
Hapa ndio watu wakaanza kusukumana kwenye benchi mpk wa mwisho akaanguka, akaamua kusepa..
Yule mzee nae amekua mkali..
" hapa tumepanga foleni, lazima tufuate utaratibu, wa kwanza ndio aende"
Kuna mmoja akajitosa akaenda,
Ile anamaliza nesi anafungua mlango..
jamaa yangu chiniii, akazima, tukampepea, Anaamka tukatulia kidogo baadae kusikia tena njoo, Akala mzinga tena...
Nesi akawa kama ame mind mbona watu hawaendi..
Hapa ndio mimi nikalazimia kwenda KUPIMA bila kutaka, ile natoka tuu ananiona..
akala mzinga wa tatu na wa mwisho...
Tulimbeba kwenye bajaji alienda zindukia hostel..
Cha kwanza kuuliza "mlinipima"?
Nikamwambia hapana, akasema mmekosea mngenipima.