Hyo story umetunga sasa swali wewe umepima? Au umewah pima?Mimi mara ya kwanza aseee nilikatiza jirani na Marie Stopes nikiwa na mishe Zangu tu,
Huku na kule ghafla mhudumu wa hapo kaniita ilikuwa nafikiri kipindi chao maana nilikuta maturubai nje? Na viti vingi vingi hivi,
Kaanza kunishawishi hapo weee na story nyingi! Dah! Nikaona isiwe ishu nikapewa kikaratasi nikaandikwa jina nikazama ndani,
Hapo roho haipo inadunda kama nini! Lakini mwisho wa siku nashukuru MUNGU nikakutwa fresh? JE wewe mwenzangu ilikuwaje? Hali yako siku hiyo sasa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji117]"kijana wewe si ndio wa kwanza nenda"Nilishaandika hiki kisa humuu si chini ya mara mbili, kuna watu wakiona watakumbuka uzi.
Mshkaji aliniamsha asubuhi subuhi (sijui usiku aliwaza nini) nimsindikize akapime pale temeke...
Nikamuuliza mzee kulikoni, akasema we twende mi najiamini sio kama wewe....
kufupisha
Sisi ndio wa kwanza pale, tulifika hata bado hawajafungua, mda wakufungua tukawa tumefika watu Saba , Kimbembe kilianza Pale nesi aliposema haya Aingie wa kwanza.....
Jamaa anasukuma wenzake kwenye bench, Anajitia kuchati, Akaambiwa na mzee mmoja
"kijana wewe si ndio wa kwanza nenda"
jamaa akasema
"Aaaah hamna shida mzee wangu yeyote naweza mpisha aende"
Hapa ndio watu wakaanza kusukumana kwenye benchi mpk wa mwisho akaanguka, akaamua kusepa..
Yule mzee nae amekua mkali..
" hapa tumepanga foleni, lazima tufuate utaratibu, wa kwanza ndio aende"
Kuna mmoja akajitosa akaenda,
Ile anamaliza nesi anafungua mlango..
jamaa yangu chiniii, akazima, tukampepea, Anaamka tukatulia kidogo baadae kusikia tena njoo, Akala mzinga tena...
Nesi akawa kama ame mind mbona watu hawaendi..
Hapa ndio mimi nikalazimia kwenda KUPIMA bila kutaka, ile natoka tuu ananiona..
akala mzinga wa tatu na wa mwisho...
Tulimbeba kwenye bajaji alienda zindukia hostel..
Cha kwanza kuuliza "mlinipima"?
Nikamwambia hapana, akasema mmekosea mngenipima.
Hakuna siku akili ilichakata na kutoa majibu kwa haraka kama wakati ule nasubiria majibu. Hivi viganja vya mikono vilikuwa vinatoa jasho bwana!
Baada ya kusubiria majibu nikaambiwa hongera! Kwa sasa ni mzima. Presha ikashuka, kisha nikamsimulia kilichonileta hasa ni kwa vile nimechera rafu halafu peku kwenye 18 na mtu ambaye nimesimuliwa kuwa ana ngoma, akaniuliza toka umecheza masaa 72 yamepita? Nikamjibu ni jana tu.
Akanielekeza taratibu za kufuata ili nipatiwe msaada. Nilipofika sehemu ya kupewa dawa, mhusika hakuwepo, nikaambiwa nije J3 na ukizingatia ile siku ilikuwa ijumaa. So nikisubiria hadi J3 manake masaa 72 yatakuwa yamepita na nitapata ngoma, nilihisi magoti laini kama mlenda aisee!
Yule mhudumu baada ya kuhangaika akapata vidonge vitatu na akanishauri ninywe ijumaa ile, jumamosi na jumapili kisha j3 nirudi kuchukua kikopo kizima cha vidonge 30.
To cut the story, nilimaliza vidonge 33 ila nasikia kuna watu hawamalizi vidonge 30 coz vinalewesha kwa siku za mwanzo, yule mwanamke alikuwa +ve