dorcas1234
Senior Member
- Mar 13, 2012
- 116
- 34
Habari wana jamvi,
naomba kuuliza,hivi siku hivi bado kuna ile hali ya kuweka pingamizi kanisani kwa ajili kijana/mwanadada wasioane?
Nilichoshuhudia wiki mbili zilizopita ndicho kilichonisukuma kuleta hoja hapa jamvini.Kuna harusi moja nilishuhudia eneo fulani sitalitaja hapa,sasa wakati tuko kanisani na mwanadada anataka kula kiapo cha ndoa, kwanza ilisikika ninong'ono kama vile kunajambo mara ikasikika sauti ya mtu akisema "NAWEKA PINGAMIZI" kila mtu akageuka tukamuona nikijana mmoja ameshikilia karatasi mkononi mfano wa cheti cha ndoa,akafika hadi madhabahuni,hapo kanisa liko kimya kutaka kujua nini kinafuata kama ni ndoa basi au la!,cha kushangaza Mchungaji akauliza,(jamani haya yametokea kweli) ilikuwa kama mchezo wa kuigiza.
Mchungaji akamuuliza,jamaa unasemaje? jamaa akajibu huyu ni mke wangu na cheti cha ndoa yetu hiki hapa nilioana naye mwaka 1999 ndoa ya kiislamu.....haya mazungumzo wakati yanaendelea kanisa lilikuwa kimya na tulikuwa tunasikia hasa sisi tuliokuwa mbele.Mchungaji akauliza ulikuwa unakaanae sikuzote au akasema tulitengana mwaka 2002,Mchungaji akasema sasa hii ndoa imetangazwa wiki 3 ulikuwa wapi kuleta pingamizi? jamaa akajibu nilikuwa Dodoma kikazi,Mchungaji akasema pingamizi lako limechelewa na kwanini usimtafute mke wako miaka yote uje leo,Mchungajia akaita walinzi wakamtoa nje na Mchungaji akaendelea kufingisha ndoa.
SWALI langu mimi ni hivi,kwanza nilishangaa kwa nini Mchungaji aliamua kuendelea na kufungisha hiyo ndoa Wana jamvi hapo sio kuwa Mchungaji alikosea? au kwa wale wanaojua sheria ,hii imekaaje kwa wakristo wa Kiluther? au je pingamizi ni kwa siku zile za matangazo ya ndoa? na siku ya tukio huruhusiwi kuweka pingamiz? KAMA KUNA YEYOYE ANAYEJUA ZAIDI TUJUZANE