Umewahi kushuhudia hii?

Umewahi kushuhudia hii?

dorcas1234

Senior Member
Joined
Mar 13, 2012
Posts
116
Reaction score
34
Habari wana jamvi,
naomba kuuliza,hivi siku hivi bado kuna ile hali ya kuweka pingamizi kanisani kwa ajili kijana/mwanadada wasioane?
Nilichoshuhudia wiki mbili zilizopita ndicho kilichonisukuma kuleta hoja hapa jamvini.Kuna harusi moja nilishuhudia eneo fulani sitalitaja hapa,sasa wakati tuko kanisani na mwanadada anataka kula kiapo cha ndoa, kwanza ilisikika ninong'ono kama vile kunajambo mara ikasikika sauti ya mtu akisema "NAWEKA PINGAMIZI" kila mtu akageuka tukamuona nikijana mmoja ameshikilia karatasi mkononi mfano wa cheti cha ndoa,akafika hadi madhabahuni,hapo kanisa liko kimya kutaka kujua nini kinafuata kama ni ndoa basi au la!,cha kushangaza Mchungaji akauliza,(jamani haya yametokea kweli) ilikuwa kama mchezo wa kuigiza.
Mchungaji akamuuliza,jamaa unasemaje? jamaa akajibu huyu ni mke wangu na cheti cha ndoa yetu hiki hapa nilioana naye mwaka 1999 ndoa ya kiislamu.....haya mazungumzo wakati yanaendelea kanisa lilikuwa kimya na tulikuwa tunasikia hasa sisi tuliokuwa mbele.Mchungaji akauliza ulikuwa unakaanae sikuzote au akasema tulitengana mwaka 2002,Mchungaji akasema sasa hii ndoa imetangazwa wiki 3 ulikuwa wapi kuleta pingamizi? jamaa akajibu nilikuwa Dodoma kikazi,Mchungaji akasema pingamizi lako limechelewa na kwanini usimtafute mke wako miaka yote uje leo,Mchungajia akaita walinzi wakamtoa nje na Mchungaji akaendelea kufingisha ndoa.
SWALI langu mimi ni hivi,kwanza nilishangaa kwa nini Mchungaji aliamua kuendelea na kufungisha hiyo ndoa Wana jamvi hapo sio kuwa Mchungaji alikosea? au kwa wale wanaojua sheria ,hii imekaaje kwa wakristo wa Kiluther? au je pingamizi ni kwa siku zile za matangazo ya ndoa? na siku ya tukio huruhusiwi kuweka pingamiz? KAMA KUNA YEYOYE ANAYEJUA ZAIDI TUJUZANE
 
mmmh!hili limenizidi kimo kulianzisha,ngoja niwasubiri...
 
Tangazo la ndoa siku 21 ni matakwa ya sharia, so hata ufungie kwa DC lazima utangaze siku 21,na yeyote mwenye pingamizi anatakiwa apinge ndani ya hizo siku 21..............la sivyo hana chake, ndio maana siku hizi kwa kuepuka usumbufu watu hutangaza ndoa hata kabla ya miezi mitatu ili awe huru kwani pingamizi lipo valid ndani ya siku 21 za tangazo.Kama huyo binti aliolewa inatakiwa awe amepewa talaka kisheria na si vinginevyo au kama makubaliano ya ndoa ni mitala inabidi uwe mpole kwani ulikubali kwenye makubaliano ya mwanzo............so ni jukumu la mchungaji kusoma cheti na kumuuliza binti kama ana talaka,au ilikuwa ndoa ya mkataba,mitala nk
 
engeweka source ulipoitoa kwanza
halafu thread hizi zinawekwa mmu na sio love connects

halafu huyo mchungaji kapewa cheti cha kiislam kumbuka
na yeye ni mkristo
so go figure that
 
...halafu huyo mchungaji kapewa cheti cha kiislam kumbuka na yeye ni mkristo so go figure that
kuna kitu kimepanua wigo wangu wa kufikiri hili suala,kwamba ndoa ya kiislamu haitambuliwi kikristo na kinyume chake!!!!je ndoa ya kikatoliki na ile ya kisabato!!mchungaji wa kilutheri akipelekewa cheti cha ndoa cha kiangilikana...aisss hiii kitu nadhani bado ni mdogo kuielewa vyema!
 
Tangazo la ndoa siku 21 ni matakwa ya sharia, so hata ufungie kwa DC lazima utangaze siku 21,na yeyote mwenye pingamizi anatakiwa apinge ndani ya hizo siku 21..............la sivyo hana chake, ...
kama ndoa hufungwa baada ya hizo siku 21 kwanini swali hilo huulizwa kama umesema zikishapita siku 21...hana chake!!
 
Kama siku ya harusi mtu hawezi kupinga, ni kwanini wachungaji huwa wanawauliza waumini kama kuna yeyote mwenye zuio la haki? Mimi nafikiri mchungaji alipaswa aahirishe ndoa hadi kwanza hayo mambo yawe resolved. maana tayari jamaa alieleza kwamba alikuwa mbali. So mchungaji hapa inaonekana alishiriki kwenye dhuluma za mke wa mtu. Kama huyu mke alikuwa tayari ameshatengana na huyu bwana si alipaswa awe na talaka? sasa kama hana talaka anawezaje kufunga ndoa nyingine? just curious
 
kama ndoa hufungwa baada ya hizo siku 21 kwanini swali hilo huulizwa kama umesema zikishapita siku 21...hana chake!!
huwa wanachemka wachungaji wengi siku hizi wana mbwembwe sana, me nilifunga ndoa 1964...........mambo hayakuwa hivi vijana wengi mnachanganya mambo........kinachotokea ni kwamba jambo la kupinga ndoa kanisani sio la kawaida watu wanapata taharuki, mchungaji mwenye busara yapaswa amwambie aende mahakamani kwani muda umepita .......''there is no ignorance of law'', mfano kwa kesi ya mirathi kama hujaleta madai ndani ya siku tisini kisheria tokea tangazo la mirathi kutangazwa unahitaji huruma ya wafiwa ili kupata chako...........otherwise......
 
kuna kitu kimepanua wigo wangu wa kufikiri hili suala,kwamba ndoa ya kiislamu haitambuliwi kikristo na kinyume chake!!!!je ndoa ya kikatoliki na ile ya kisabato!!mchungaji wa kilutheri akipelekewa cheti cha ndoa cha kiangilikana...aisss hiii kitu nadhani bado ni mdogo kuielewa vyema!


unaweza pinga mahakamani..
since ndoa zote zipo kimahakama

but ukienda kanisani hawakutambui
mfani yapo makanisa ya kilekole mtu akishaokoka tu
anatakiwa amlete mume/mke wake nae aokoke wafungishwe ndoa upya
vinginevyo anatafutiwa mchumba mwingine kanisani
 
Kama siku ya harusi mtu hawezi kupinga, ni kwanini wachungaji huwa wanawauliza waumini kama kuna yeyote mwenye zuio la haki? Mimi nafikiri mchungaji alipaswa aahirishe ndoa hadi kwanza hayo mambo yawe resolved. maana tayari jamaa alieleza kwamba alikuwa mbali. So mchungaji hapa inaonekana alishiriki kwenye dhuluma za mke wa mtu. Kama huyu mke alikuwa tayari ameshatengana na huyu bwana si alipaswa awe na talaka? sasa kama hana talaka anawezaje kufunga ndoa nyingine? just curious


Kwa kawaida ndoa za siku hizi huwa zinakuwa na maandalizi yanayochukua zaidi ya miezi minne, michango, harusi, nk. Kwani alisafiri muda wote huo? Na inawezekana kweli hizi habari alipata siku ya harusi tu?
Hapa issue ni kuwa jamaa alitaka kumharibia huyo dada!
 
Back
Top Bottom