Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Mkuu! Kuna roho nyingi sana unaziponya kwa kupitia kazi yako njema!! Hakika Mungu atakulipa mara dufu!! maana hakuna aliyemtumikia Mungu akabaki mikono mitupu!! hakuna aliyemtumikia Mungu akapata aibu! Mungu aukumbuke na uzao wako!!
 
Kimenifunza vingi sana hiki kitabu,Hongera mkuu kwa kazi ngumu uliyoifanya

Binafsi,hivi ni vitu nilivyojifunza katika sura zote hizo

1.Usiwe mtumwa wa pesa,ifanye pesa iwe mtumwa wako
-Asilimia 80 ya watu tumekua watumwa wa pesa bila kutambua,pesa inatutumikisha kila siku,inabidi kila siku tufanye kazi kuipata pesa ili watoto wale,chakula kipatikane,bundle liwepo,Tanesco,tuwahonge watoto wakali etc
Tunajikuta tupo kwenye duara(loop) la kuitumikia pesa kwa kufanya kazi ili tuwezo kutimiza mambo ya lazima pamoja na matamanio yetu mengine

Na siku ikipita bila kufanya kazi,pesa inatuadhibu kwa kutotimiza matumizi yetu(mambo ya lazima na matamanio yetu)

Kitabu kinatufunza kuondoa hii "mindset" ya kimasikini na kuifanya pesa iwe mtumwa wetu

Badala ya sisi kufanya kazi na kupata pesa itakayokidhii mahitaji yetu,basi itufanyie kazi ya kukidhii mahitaji yetu

Hapa kinatupa siri kuwa,masikini tunaamini sisi ndiyo tuna jukumu la kufanya kazi kwa bidii ili maisha yaende wakati "matajiri" pesa ndiyo inajukumu la kufanya kazi kwa bidii ili maisha yaendee

MATAJIRI HAWAFANYI KAZI,UKITAKA KUWA TAJIRI ACHA KUFANYA KAZI,AJIRI PESA IKUFANYIE KAZI

2.Funzo la pili nililojifunza hapa,ni jinsi ya kuajiri pesa
-Pesa sio ile tunayoipata baada ya kufanya kazi(iwe faida kwenye biashara au mshahara wa mwisho wa mwezi)
-Pesa ni kile tunachokitunza kwa kuweka akiba
-Kama unaingiza Tsh 10,000 kwa siku basi hakikisha unaweka akiba ya 1,000,yaani 1/10 ya kipato chako cha kila siku

Kama unategemea mshahara,labda wa Tsh 300,000 kwa mwezi,kwa siku unaingiza kiasi cha Tsh 300,000(mshahara wako)/30(idadi ya siku katika mwezi) ambayo ni sawa na Tsh 10,000 kwa siku
Hapa hakikisha matumizi yako kwa siku hayazidi Tsh 9000
Hapa utakua unaweza kuokoa Tsh 1,000 kila siku katika mshahara wako na kujikuta una akiba ya Tsh 30,000 kila mwezi(1000 * 30(idadi ya siku katika mwezi)

Fanya hivyo kwa kipindi cha mda maalum(napendekeza ndani ya kipindi cha mwaka mmoja au zaidi)

Kwa mwenye kipato cha 10,000 kwa siku,ndani ya mwaka mmoja atakua na akiba ya Tsh (10,000/10 * 366(idadi ya siku katika mwaka)
Sawa na Tsh 366,000 kwa mwaka

Kwa mwenye mshahara wa Tsh 300,000 mpaka mwisho wa mwezi atakua na Akiba ya Tsh 366,000 pia
(Hapo tumeona jinsi gani ya kuweka akiba kwa mfanyabiashara au mfanyakazi)
10% ya pato lako ni kiwango cha chini zaidi ya pato lako,unaweza kuiongeza kwa kupunguza matumizi yasio ya lazima (matamanio)

Kwa mfano kama mahitaji yako ya kila siku ni Tsh 9,000 na kipato chako kwa siku ni Tsh 10,000 hapa akiba yako kwa siku (10% ya pato lako) ni Tsh 1,000.unaweza kuiongeza kuiongeza kwa kuondoa matamanio kwenye matumizi yako ya kila siku

Hii ni kanuni rahisi,
Mahitaji ya kila siku = matumizi ya lazima kwa siku + matamanio ya siku

Hakikisha, matamanio ya siku = 0
Hapa unaweza jikuta unatumia Tsh 7,000 badala ya Tsh 9,000 na akiba yako ikawa Tsh 2,000 (20% ya pato lako) badala ya Tsh 1,000(10% ya pato lako) hivyo kwa mwaka utakua na Tsh 732,000 badala ya Tsh 366,000
Hapa utaona kwa kuondoa matamanio yako(matumizi yasio ya lazima) unaweza ku "double" pato lako la mwaka

Nafikiri kanuni rahisi ni hii
Hapo utakua umepata mtumwa /mfanyakazi wako wa kwanza mwenye thamani ya Tsh 732,000 ndani ya kipindi cha mwaka mmoja tu

Hivi ndiyo jinsi ya kuajiri pesa,tunaajiri pesa kwa kuweka akiba

3.Funzo la tatu nililojifunza ni jinsi sasa ya kuipatia kazi ya kufanya pesa yetu tuliyo iajiri
Hapa tunakua na wazo lolote lile la biashara(kumbuka hii ni biashara ambayo hatutafanya sisi)
Lengo sio sisi kufanya kazi,tayari tuna mfanyakazi Mr Tsh 732,000 atakaye fanya hii kazi

Baada ya kupata wazo letu,tuseme labda (Mgahawa wa chakula cha asubuhi)
Tunatafuta watu wenye uzoefu na aina hii ya biashara ili kupata ushauri kutoka kwao,watu wenye uzoefu ni mara zote watu waliofanikiwa kwenye biashara husika

Baada ya kupata ushauri kutoka kwao,pia tunahakikisha tunatafuta wahudumu wenye uzoefu

Baada ya kupiga hesabu na kuhakikisha hatupo kwenye risk ya mpoteza mfanyakazi wetu Mr Tsh 732,000 hapa ndipo tunapo mtuma akafanye kazi
Kwa kila faida atakayo ingiza kwa siku,tunaitumia kuajiri pesa nyingine,nayo tutaipa kazi na chochote itakacho ingiza tutaitumia kuajir nyingine kwa hekima ile ile ya kwanza

4.Funzo la nne,ni kuwa na moyo wenye uthubutu wa kufanya jambo,kuwa na nia ya kweli,na tamaa ya mafanikio

5.Tuzione changamoto kama fursa(roho ya mtu huru),kuliko kuziona kama matatizo(roho ya mtumwa)

6.Tuzungukwe na marafiki waliofanikiwa na watakao weza kutupa ushauri

7.Tusijitese sana,kuna mda tukate kiu ya matamanio yetu,bila kuathiri kipato chetu

Hayo ni machache kati ya mengi niliyojifunza
 
The Richest man in Babylon is one good book that I would advise anyone to endorse himself/herself.The problem is that most of the time we study these books and add them to our book collection with little application.

Very true. We read some amazing books, with lots of knowledge.
The story ends up there. Literally we rarely take the lessons and apply anywhere in our lives.
Sometimes I think meditation can help us manage the transition between learning something and doing. I don't do meditation myself
 
Hayo maisha uliyoyapitia kuna watu wanayapitia sasa ivi unaposema hii comment

Wengine hawana access ya huu uzi wa Red Giant
Tujifunze kuwa walimu wa wenzetu,
I hope mkuu hutoruhusu hicho kipindi kijirudie
Naahidi kuwa mwalimu muzur kwa vijana!! maana vijana wengi wanajitoa uhai kwa mazira wanayopitia!!

Hawana pa kujifunza!! na Kuna watu wanauwezo wa kufundisha, lakini wanajiuliza "nitapata nn nikimfundisha" wengine wanasema " mtu mwenyewe hanihusu"
Kumbe tungeondoa ubinafisi Kama red giant tungeokoa roho nyingi sana!!
Mungu aendelee kutuinulia watu Kama red giant. Nisi pia tujifunze kushea vipawa vyetu na wengine!
 
Wacha nianze nimejiridhisha na comments za wadau
 
Hivi ukiwa unasoma kitabu chenye lugha ya kiingereza Pdf kuna uwezekano ukibadili kiwe lugha ya kiswahili maana huwa nachokaga kuaangalia maneno magumu kwenye dictionary mwisho simalizi kitabu
 
Amesema asilimia kumi ya kipato unaweka na asilimia tisini ndio unafanya matumizi .kanuni kuu hapa ni kusave hela kabla ya matumizi.
 
Sisi wa iphone mkuu tunaomba ufanyie mpango tupate hiyo app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…