Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Kwa wiki tatu na siku tano mashambulizi yaliendelea bila kukoma. Sehemu aliyokuwa amekaa Banzar iligeuka matope kutokana na damu na wanajeshi kupita walipokuwa wanaenda juu ya ukuta au walipokuwa wanajikokota kushuka. Kila siku maiti za wavamizi zilijazana nje ya ukuta. Usiku, wenzao walizitoa na kwenda kuzizika. Kwenye siku ya tano ya wiki ya nne vita iliendelea usiku kucha bila kukoma. Kulipopambazuka vumbi lililotimuliwa na adui aliyekuwa anaondoka lilionekana.

Walinzi wa kuta za jiji walipiga kelele kwa shangwe. Wanajeshi waliokuwa ndani nao wakapiga kelele, na raia vilevile. Jiji zima likashangilia.

Watu walitoka majumbani mwao na mitaa ikajaa umati wa watu. Wasiwasi uliowajaa kwa wiki kadhaa ukageuka nyimbo za furaha. Kutoka kwenye mnara wa hekalu la Beli moto wa ushindi uliwashwa. Moshi ulipanda juu kupeleka taarifa hadi sehemu za mbali.

Kwa mara nyingine kuta za Babiloni zilikuwa zimemzuia adui mwenye nguvu. Adui aliyepanga kupora hazina yake, kutesa na kufanya watu wake kuwa watumwa.

Jiji la Babaliloni lilidumu karne na karne kwa sababu lilikuwa na ulinzi thabiti. Gharama ya kutojilinda ilikuwa ni kubwa sana kwake.

Kuta za Babiloni zilikuwa ni mfano bora juu ya tamaa ya mwanadamu ya kujilinda. Hii ni tamaa ya asili ya mwanadamu. Tamaa ina nguvu leo kama ilivyokuwa enzi za kale. Tofauti ni kuwa leo tuna njia bora za kuitimiza.

Leo tuna kuta zisizopenywa za bima, akaunti za akiba na miradi mingi salama tunayoweza kuwekeza. Leo tunaweza kujilinda dhidi ya majanga yasiyotarajiwa, yanayoweza kuingia katika nyumba zetu na kuweka makazi.

Gharama ya kutokuwa na ulinzi wa kutosha ni kubwa sana.

Mwisho wa sura ya saba.
Asante!! Naendelea kupata madini!
 
MUUZA NGAMIA WA BABILONI

kadri mtu anavyopatwa na njaa ndivyo akili yake inavyofanya kazi zaidi. Pia ndivyo uwezo wake wa kunusa harufu ya chakula unavyoongezeka.

Hivyo ndiyo ilivyokuwa kwa Tarkad mwana wa Azure. Kwa siku mbili alikuwa hajatia kitu chochote mdomoni zaidi ya tini mbili ndogo alizokuwa ameiba bustanini. Lakini kabla hajachuma tini nyingi zaidi alitokea mwanamke mwenye hasira na kumfukuza hadi mtaani. Sauti yake kali bado ilikuwa inasikika masikioni mwa Tarkad alipokuwa anatembea sokoni. Ndiyo iliyomzuia kudokoa matunda yaliyokuwa yanauzwa kwenye vikapu sokoni.

Kabla ya leo alikuwa hajawahi kufikiria ni chakula kiasi gani huletwa kwenye masoko ya Babiloni na jinsi kilivyo na harufu nzuri. Kutoka sokoni akaingia hotelini na kuanza kutembea tembea karibu na ukumbi wa kulia chakula. Aliwaza kuwa pengine hapa anaweza kuonana na mtu anayemfahamu ili akope pesa kidogo. Bila kuwa na pesa alijua kuwa hatakiwi pale.

Akiwa bado amezama kwenye mawazo akajikuta anagongana uso kwa uso na mtu ambaye hakupenda kabisa kukutana naye, alikutana na mtu mrefu na mkakamavu, Dabasir, muuza ngamia. Katika jamaa zake wote ambao amewahi kukopa pesa ndogondogo Dabasir ndiye alimfanya ajihidi vibaya sana baada ya kudhindwa kulipa.

Dabasir alipomuona Tarkad uso wake ukakunjuka kwa furaha. "Ha! Ni wewe Tarkad! Nimekuwa nakutafuta unilipe zile sarafu mbili nilizokukopesha mwezi uliopita, na kile kipande cha pesa nilichokukopesha kabla ya hapo. Bora tumekutana, nina shida nazo leo, unasemaje?"

Tarkad akapatwa na kigugumizi na uso ukamuumuka. Kwa njaa yake hakuwa na ujasiri wa kubishana na Dabasir. Dabasir alikuwa ni mtu wa kuongea bila kumung'unya maneno.

"Samahani, samahani sana," alisema Tarkad kwa kubabaika na kinyonge. Hapa sina pesa ya kukulipa.'

"Basi kazitafute," akasema Dabasir kwa msisitizo. "Ina maana huwezi pata sarafu chache na kipande cha fedha ili kumlipa rafiki wa baba yako aliyekutendea wema ulipokuwa na shida?"
'"Nimeandamwa na bahati mbaya ndiyo maana nimeshindwa kukulipa."

"'Bahati mbaya! Unawezaje kuilaumu Miungu kwa uzembe wako mwenyewe? Bahati mbaya huwapata wale wanaofikiria kukopa kuliko kulipa. Hebu nifuate, maana nina njaa. Nataka kukusimulia kisa kimoja."

Tarkad alifadhaishwa na jinsi Dabasir alivyokuwa anaongea bila kumung'unya maneno lakini alimfuata na kufurahi kupata nafasi ya kuingia kwenye ukumbi wa chakula.
Walienda kwenye kona moja na kukaa kwenye zuria. Mmiliki wa hoteli ile, bwana Kauskori alipokuja huku akitabasamu Dabasir akamwambia. "We kenge mnene wa jangwani hebu niletee mguu mmoja wa mbuzi ulioiva vizuri na mkate pamoja na mbogamboga zote ulizonazo. Nina njaa sana. Usimsahau huyu rafiki yangu, mletee jagi la maji baridi maana joto ni kali sana leo.

Moyo wa Tarkad ukanyong'onyea. Yaani akae pale akinywa maji huku akimuangalia Dabasir akila mguu mzima wa mbuzi! Lakini hakusema kitu.
Dabasir hakuwa mtu wa kukaa kimya, alitabasamu na kuwapungia wateja wengine mikono. Karibu wote waliokuwemo mule alikuwa anajuana nao.

"Nimesikia habari fulani kutoka kwa msafiri mmoja aliyetoka Urfa hivi karibuni. Kanisimulia habari za tajiri mmoja ambaye alijenga nyumba, na kisha akakata mawe yaliyokuwa yanaangaza kama kioo na kuyaweka madirishani. Lakini mawe yale yalikuwa ya manjano na ukiangalia nje kupitia dirishani unaona dunia ikiwa na rangi tofauti kabisa.

Unasemaje kuhusu hili Tarkad, yaani dunia yote ionekane kwa rangi tofauti na ile ya asili?

"Sina la kusema," akajibu Tarkad huku mawazo yake yakiwa kwenye ule mguu wa mbuzi ulionona mbele ya Dabasir.

"Mimi nimeamini. Sababu mi mwenyewe nimewahi kuiona dunia ikiwa na rangi tofauti. Kisa nitakachokusimulia kinahusu jinsi nilivyoweza kuiona dunia kwa rangi yake halisi tena.

"Dabasir ana kisa anataka kusimulia." Alisema mtu mmoja aliyekuwa anakula pembeni yao akiwaambia wengine mule mgahawani huku akisogeza zuria lake. Wale wengine nao wakasogea na kutengeneza nusu duara. Walisogea na vyakula vyao, ni Tarkad pekee ndiye ambaye alikuwa hana chakula. Alitamani sana lakini Dabasir hakumkaribisha.
"Kisa ninachotaka kusimulia." Alianza kusema Dabasir huku akiendelea kula mguu wa mbuzi. "Kinahusiana na nilivyoanza maisha na jinsi nilivyokuja kuwa mfanyabiashara wa ngamia. Kuna mtu anajua kuwa zamani nilikuwa mtumwa huko Siria?"

Kusikia hivyo watu wote wakaanza kunong'ona kwa mshangao.

"Nilipokuwa kijana," akaendelea Dabasir baada ya kukata kipande kikubwa cha nyama. "Nilijifunza kazi ya baba yangu, kutengeneza matandiko ya farasi. Nilifanya kazi kwenye karakana yake na baada ya muda nikaoa. Sababu nilikuwa kijana na sikuwa na ujuzi mkubwa kipato changu kilikuwa kidogo, lakini kilitosha kumtunza mke wangu. Nilitamani vitu vizuri lakini sikuwa na jinsi ya kuvipata. Nikagundua kuwa wafanyabiashara walikuwa tayari kunikopesha nami niwalipe baadaye.

"Kutokana na kukosa uzoefu sikujua kuwa yule anayetumia kuliko pato lake anakuwa anapanda mbegu ya upepo wa matumizi yasiyo na lazima. Upepo ambao mavuno yake ni kimbunga cha matatizo na aibu. Nilizama kwenye matumizi kwa kukopa nguo nzuri na kumnunulia mke wangu vitu vya anasa. Nyumba yetu tukajaza vitu vya anasa. Tulikopa na kutumia kuliko uwezo wetu.

"Mwanzo niliweza kulipa bila tatizo lolote lakini siku zilivyoenda nikaona kuwa pato langu halitoshi kuishi na kulipa madeni. Wakopeshaji wakaanza kunifuatilia nilipe madeni na maisha yangu yakaanza kuwa machungu. Nilikopa kwa rafiki zangu lakini nao sikuweza kuwalipa. Maisha yakawa mabaya kabisa. Mke wangu akarudi kwao na mimi nikaamua kutoroka Babiloni na kwenda kuishi mji mwingine.
 
Kuwa mtumishi wa Mungu sio lazima uwe na kanisa Kama kina Masanja!! hata kwa kazi hii unayoifanya ni utumushi mkubwa sana!! Kwanza huhitaji sadaka Kama akina Masanja waganga njaa!! wewe unafanya utumishi ulioko moyoni mwako!! sio utumishi was kulazimisha Kama wafanyavyo wengine!!

Utumishi unatoka moyoni!! utumishi ni kipawa mtu anachopewa na Muumba wake!!
hapa sadaka naweza toa hata bila kuombwa, abirikiwe sana aliyeanzisha huu uzi wa simulizi hii
 
"Nikapata kazi kwenye msafara wa wafanyabiashara na nikafanya kwa miaka miwili. Maisha yalikuwa magumu na ya kutangatanga. Baaadaye nikaacha kazi na kujiunga na kundi la waporaji waliokuwa wakitangatanga jangwani kuvamia misafara isiyo na ulinzi. Kwa jinsi baba yangu alivyonilea sikupaswa kufanya matendo yale lakini sikuona aibu. Nilikuwa naiona dunia kupitia kioo chenye rangi, sikutambua jinsi nilivyokuwa nimepotea.

"Kwenye kazi yetu ya kwanza tulipata mafanikio. Tulipora dhahabu nyingi, hariri na vitu vingine vya thamani. Tulienda Ginir na kutapanya mali yetu yote.
"Mara ya pili bahati haikuwa upande wetu. Tulipokuwa tumepora ghafla tukaanza kushambuliwa na mikuki kutoka kwa watu wa chifu wa eneo lile. Misafara ilikuwa inamlipa chifu yule kwaajili ya ulinzi. Viongozi wetu wawili waliuwawa na tuliobaki tulichukuliwa hadi Damasko. Huko tulivuliwa nguo zetu na kuuzwa kama watumwa.

"Mimi nilinunuliwa na chifu mmoja wa jangwani kwa vipande viwili vya fedha. Nilinyolewa ywele na kupewa nguo ya kuziba uchi tu kama watumwa wengine. Kwasababu nilikuwa kijana nisiyejali niliona kama mchezo tu. Lakini hilo lilibadilika ghafla pale yule chifu alipo nipeleka kwa wake zake na kuwauliza iwapo wanahitaji towashi. Hapo ndipo nikagundua nipo kwenye hali mbaya.

"Kwa uoga mkubwa nilisimama huku wale wanawake wakinichunguza. Kichwani nikiwaza iwapo watanionea huruma. Alieanza kunikagua alikuwa ni mke mkubwa, Sira. Alinikagua bila kusema lolote, sikujua ameamua nini.

Wa pili kunikagua alikuwa mwanamke mzuri sana ambaye aliniangalia kwa dharau kama vile nilikuwa mnyoo tu. Wake zake wadogo wawili walinikagua kama vile nilikuwa kichekesho tu.

Nilikaa nikisubiri hukumu yangu, ulionekana kama ni muda mrefu sana. Ilionekana kama wanawake wale wanategeana kutoa majibu.

Mwishowe Sira alisema "'Matowashi tunao wengi wa kutosha lakini hatuna watunza ngamia wa kutosha. Wachache tulionao hawaijui kazi yao vizuri. Hata leo ningependa kumtembelea mama yangu ambaye ni mgonjwa lakini sioni mtumwa wa kuongoza ngamia vizuri. Muulize huyu kama anaweza kuongoza ngamia.'

"Bwana wangu akaniuliza, ' unajua nini kuhusiana na ngamia?'
"Nilijikaza nisionyeshe furaha yangu, nikajibu. Naweza wafanya wapige magoti, naweza kuwapakia na naweza kuwaongoza kwenye safari ndefu bila kuchoka. Pia ikihitajika, naweza kurekebisha kamba za kuwafunga.

"'Huyu mtumwa anaonekana anauelewa. Kama unaona anafaa mchukue awe mtunza ngamia wako.'

"Hivyo nikawa mtumwa wa Sira na siku hiyohiyo niliongoza ngamia wake kwenda kumuona mama yake. Nilitumia muda huo kumshukuru kwa kuniokoa kutoka kuhasiwa. Nikamueleza kuwa mimi sikuzaliwa mtumwa bali ni mtoto wa mtu huru, mtengeneza matandiko huko Babiloni. Pia nikamsimulia hadithi ya maisha yangu. Majibu yake hayakuwa ya kufariji na yaliniacha na maswali mengi.

'''Unawezaje kujiita mtu huru iwapo udhaifu wako umekutumbukiza kwenye hali kama hii? Mtu kama akiwa na roho ya utumwa atakuwa mtumwa tu hata akizaliwa wapi na nani. Maji si hufuata mkondo?
Kama ana roho ya mtu huru, je hataheshimiwa katika jiji lake hata kama hana utajiri?
 
"Nilikuwa mtumwa kwa mwaka mmoja na niliishi na watumwa lakini sikuweza kuwa mmoja wao. Siku moja Sira aliniuliza, 'watumwa wengine wanachangamana pamoja na kufurahi kwanini wewe hukaa peke yako hemani?'

"Nafikiria ulichoniambia. Nafikiria iwapo nina roho ya utumwa. Siwezi kuchangamana nao hivyo nimeamua kukaa peke yangu.'

'''Hata mimi muda mwingi hukaa peke yangu,' aliniambia. Mahari yangu ilikuwa kubwa sana. Na bwana wangu alinioa sababu ya thamani yangu. Lakini hanitamani tena. Takwa kubwa la mwanamke ni kutamaniwa. Lakini sababu ya hilo na sababu ya kutopata mtoto imenibidi kujitenga. Ningekuwa mwanaume ningekubali kufa kuliko kuwa mtumwa lakini desturi yetu kwa mwanamke kuwa mtumwa ni jambo la kawaida.

'''Wewe kwani unanionaje' nilimuuliza. 'Je, nina roho ya mtu huru au roho ya mtumwa?'
'''Una mpango wa kulipa madeni unayodaiwa huko Babeli?' alinihoji.

'''Nina nia ya kulipa madeni yangu lakini sina jinsi,'

'''Kama miaka imepita na ulikuwa ukizurura tu bila kufanya jitihada yoyote kulipa madeni yako basi wewe ni mtumwa wa hali ya chini kabisa. Mtu anayejiheshimu lazima atalipa madeni yake.
'''Nitafanya nini kulipa madeni yangu na mimi ni mtumwa huku Siria?'

'''Endelea kuwa mtumwa ewe mtu dhaifu!'

'''Mimi siyo mtu dhaifu,' nilipinga vikali.

'''Thibitisha kama kweli wewe siyo dhaifu,'
'''Nitathibitishaje sasa?'
"Je mfalme wako wa Babeli hapigani na maadui kutoka kila upande akitumia kila njia na jeshi lake lote? Madeni yako ndiyo adui zako. Ndiyo yaliyokukimbiza kutoka Babiloni. Uliyaacha na yamekuwa na nguvu kukuzidi. Kama ungepambana nayo kiume ungeyashinda na ungekuwa mtu wa kuheshimika. Lakini hukuwa na moyo wa kupambana na tazama umekuwa mtu wa chini hadi kuwa mtumwa hapa Siria.
"Nilitafakari maneno yake makali na kufikiria maneno ya kumjibu kumuonyesha kwamba mimi sina roho ya utumwa lakini sikuweza kusema chochote. Siku tatu baadaye kijakazi wake alinifuata na kuniambia kuwa ninaitwa na Sira.

'''Mama yangu ni mgonjwa tena,' aliniambia Sira. 'Andaa ngamia wawili wenye afya bora. Wapakie maji na mahitaji mengine kwaajili ya safari ya siku nyingi. Kijakazi wangu atakuandalia mahitaji yote kwaajili ya safari.'

"Nilipakia vitu kwenye ngamia nikistaajabu jinsi vilivyokuwa vingi. Mama yake Sira aliishi umbali wa siku moja tu lakini kijakazi aliandaa vitu vingi sana. Wakati wa safari kijakazi alipanda ngamia wa nyuma nami nilikuwa mbele nikiongoza ngamia wa Sira. Tulipofika nyumbani kwa mama yake tayari usiku ulikuwa umeingia. Baada ya kumuondoa kijakazi wake Sira aliniambia.

'''Dabasir wewe una roho ya mtu huru au roho ya utumwa?"
'''Nina roho ya mtu huru,' nilijibu kwa msisitizo.

'''Sasa ndiyo nafasi yako ya kuthibitisha hilo. Bwana wako amelewa na machifu wake hawajitambui. Chukua hawa ngamia na utoroke. Chukua na hizi nguo za bwana wako ili usijulikane. Nitasema kuwa uliiba ngamia na kutoroka nilipoenda kumuona mama,'

'''Hakika wewe una roho ya malkia,' nilimwambia. Natumaini utapata furaha maishani mwako.

"'Furaha,' alijibu, 'furaha haimsubiri mke mtoro anayeitafuta kwenye nchi ya mbali katikati ya watu wageni. Nenda zako na Miungu ya jangwani ikulinde. Safari yako ni ndefu na huko utakopita hakuna chakula wala maji.'
"Sikuhitaji kuhimizwa zaidi. Nilimshukuru sana na nikatokomea gizani.
 
Sikuijua vizuri hii nchi hivyo nilikisia tu upande ambao mji wa Babiloni ulikuwako. Nilisonga kwa kujiamini kukatiza jangwani kuelekea kwenye vilima vya mbali. Nilipanda ngamia mmoja na mwingine nilimfunga akifuata nyuma. Nilisafiri usiku kucha na kesho yake yote bila kusimama. Hofu ya juu ya kinachowapata watumwa wanaoiba mali za wamiliki wao na kutoroka ilinisukuma mbele.

"Mchana wa siku ya pili nilifika kwenye nchi ya mawe mengi na kame sana. Mawe makali yaliwaumiza ngamia miguu hivyo walianza kutembea polepole na kwa taabu. Sikukutana na watu wala wanyama, lilikuwa ni eneo pweke sana.

"Ilikuwa safari ngumu sana, ni watu wachache wanaoweza kupona safari kama ile. Siku baada ya siku tulisonga mbele. Chakula na maji vilituishia na jua katili lilitupiga. Katika siku ya tisa ya safari nilidondoka kutoka juu ya ngamia na sikuwa na nguvu ya kupanda tena. Nilijua kuwa mwisho wangu unefika, kifo katika nchi ya ukiwa.

"Nilijinyoosha na kulala mpaka kulipopambazuka, ngamia wangu walikuwa wamekaa mbali kidogo wakionekana kama wenye huzuni sana. Eneo lililonizunguka lilikuwa ni miamba na jangwa tupu. Vichaka vya miiba vilionekana hapa na pale lakini hakukuwa na kitu cha kula wala maji ya kunywa. Hakuna cha kufaa binadamu wala ngamia.

"Inamaana huu ndiyo mwisho wangu, kicho cha kimya na amani!" Niliwaza.

"Niliangalia lile jangwa katili lililokuwa mbele yangu kisha nikajiuliza tena, 'Nina moyo wa mtumwa au moyo wa mtu huru?' Hapo nikagundua kuwa, iwapo nina moyo wa mtumwa basi nitakata tamaa, nitajilaza na kufa. Kifo kimfaacho mtumwa mtoro.

"Lakini iwapo nina moyo wa mtu huru natakiwa kufanya nini? Hakika nitapambana kurudi Babiloni. Nitalipa wote wanaonidai, nitarudisha furaha ya mke wangu anayenipenda kwa dhati. Pia nitafanya wazazi wangu wajivune kuwa na mtoto kama mimi.

Sira alisema "'Madeni yako ndiyo adui zako waliokufanya ukimbie Babiloni,' maneno yake yalikuwa kweli tupu. Kwanini sikubaki na kupambana kiume na adui huyo? Kwanini niliruhusu mke wangu kurudi kwao?

"Ghafla kitu cha ajabu kikanitokea dunia yote ilionekana kama ina rangi tofauti kabisa. Ni kama siku zote nilikuwa naiangalia kupitia kioo chenye rangi na sasa kimeondolewa. Niliona thamani halisi ya maisha.

"'Siwezi kufa jangwani,' nikapata mwanga mpya, nikatambua ninalotakiwa kufanya. Kwanza natakiwa kurudi Babiloni na kuonana na kila anayenidai. Nitawaambia kuwa nimerudi kuwalipa baada ya miaka mingi ya kutangatanga na taabu. Nitawalipa haraka kadri miungu itakavyonijalia. Baada ya hapo nitatafuta nyumba kwaajili yangu na mke wangu, nitakuwa raia mwema ambaye wazazi wangu watajivunia.

"Madeni yangu ndiyo yalikuwa adui zangu lakini wale walionikopesha walikuwa ni rafiki zangu. Waliniamini na walikuwa hawana shaka nami.

"Nilijikaza na kusimama. Sikujali njaa wala kiu, hayo yalikuwa ni mapito tu katika safari ya kurudi Babiloni. Roho ya mtu huru ikanijaa, mtu anayeenda kushinda adui zake na kurudisha furaha ya rafiki zake. Nilipandwa na mori mkubwa sana.

"Baada ya ngamia wangu kujitahidi kwa mara kadhaa waliweza kusimama. Kwa uvumilivu wakaanza kusonga kuelekea kaskazini, nilikuwa nina hisia huo ndiyo uelekeo wa Babiloni.
 
Sijaelewa kidogo hapo anaposema inatakiwa ujilipe 10% ya mapato yako. Je ansmaanisha ndani ya hiyohiyo 10% ndio uweze kumudu matumizi ya kila siku? Na nyingine uwekeze izalishe ndani ya hiyohiyo 10%?. Na vipi kuhusu 90% inayobaki?. Mlioelewa tafadhali mtueleweshe sisi wa Std 4.
Mfano kama ujira wako ni tsh 100'000/= kwa mwezi, amua kuweka let say 10'000/= hiyo utabakiwa na 90. Hiyo tisini ndo kama umejilipa na nduo ya mahitaji yako mengine na kadhalika ila never ever usiiguse ile asilimia 10 kwa maana ya tsh 10'000/= uliyojiwekea akiba ukaitumia tena kwa matumizi.
 
Mfano kama ujira wako ni tsh 100'000/= kwa mwezi, amua kuweka let say 10'000/= hiyo utabakiwa na 90. Hiyo tisini ndo kama umejilipa na nduo ya mahitaji yako mengine na kadhalika ila never ever usiiguse ile asilimia 10 kwa maana ya tsh 10'000/= uliyojiwekea akiba ukaitumia tena kwa matumizi.
Ni sawa ila ile 10,000 ndiyo umejilipa. Ile tisini unawalipa wauza chakula, wenye usafiri, Tanesco, maji, Tbl nk.
 
Baada ya kusafiri kwa muda tukafika nchi tuliyopata maji, nyasi na matunda. Mwishowe tukaikuta barabara inayoelekea Babiloni. Moyo wa mtu huru huona maisha ni kama msururu wa changamoto ambazo zinatakiwa kutatuliwa, lakini moyo wa mtumwa huishia kunung'unika, 'sina la kufanya mimi ni mtumwa tu!"

"Vipi kuhusu wewe Tarkad, njaa yako haifanyi kichwa chako kifanye kazi zaidi? Je, upo tayari kuanza safari ya kurudi kwenye maisha ya kujiheshimu? Unaweza kuiona dunia kwa rangi yake halisi? Je una nia ya dhati ya kulipa madeni yako hata kama ni makubwa kiasi gani? Unataka kuwa mtu unayeheshimika tena?

Machozi yakamlengalenga Tarkad. Akapiga magoti na kusema. "Umenionyesha mwanga mpya, tayari nahisi roho ya mtu huru ikiwa ndani yangu."

"Uliporudi Babiloni maisha yalikuwaje?" Aliuliza msikilizaji mmoja.

"Penye nia pana njia," alijibu Dabasir. "Nilikuwa na nia hivyo nikaanza kutafuta njia. Kwanza nilimtafuta kila aliyekuwa akinidai na kumuomba anivumilie mpaka nitakapoweza kumlipa. Wengi wao walinipokea kwa furaha sana na wachache walinishutumu. Lakini pia kati yao walitokea waliokuwa tayari kunisaidia.

"Mtu mmoja alinipa msaada niliouhitaji sana, alikuwa ni Mathon, mkopesha pesa. Alipofahamu kuwa nilipokuwa Siria nilifanya kazi ya kutunza Ngamia akaniagiza kwenda kwa mfanyabiashara wa ngamia aliyeitwa Nebaturi. Nebaturi alikuwa amepewa kazi na mfalme ya kununua ngamia bora kwa ajili ya safari za uvumbuzi. Nilitumia ujuzi wangu kumsaidia kupata ngamia bora. Polepole nikaanza kulipa madeni yangu. Mwishowe nikaweza kuinua kichwa na kujiona mtu kati ya watu.

Baada ya kusema hayo Dabasir akageukia chakula chake na kuita kwa sauti kubwa ambayo ilisikika hadi jikoni. "Kauskori, konokono mkubwa wewe! Chakula kimepoa, niletee nyama nyingine ya moto. Pia mletee na Tarkad kipande kikubwa cha nyama. Huyu ni mwana wa rafiki yangu, nitakula naye"

Hivyo ndivyo hadithi ya Dabasir ilivyoisha, hadithi ya mfanyabiashara wa ngamia wa Babeli. Alijitambua mara alipoona ukweli wa mambo. Ukweli ambao watu wenye hekima waliujua zamani za kale kabla yake.

Ukweli huo uliwaongoza watu wa vizazi vyote kutoka kwenye taabu hadi kwenye mafanikio. Utaendelea kufanya hivyo kwa wale wenye hekima ya kutambua nguvu zake za ajabu. Mtu yeyote anayesoma maneno yafuatayo anaweza kuyatumia.

Penye nia pana njia.

Mwisho wa sura ya nane.
 
TAJIRI WA BABELI

Muandishi: George S. Clason's, 1926.
Mtafsiri: Pictuss.

Email: pictuspublishers@gmail.com.

[emoji2398]Pictuss2021.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.


UTANGULIZI

YALIYOMO

Mtu aliyetamani dhahabu
Tajiri wa Babiloni
Tiba saba za pochi tupu
Kutana na Mungu wa bahati
Sheria tano za pesa
Mkopesha pesa wa Babiloni
Kuta za Babiloni
Mfanyabiashara ya ngamia wa Babiloni
Mabamba ya vigae
Mtu mwenye bahati zaidi katika Babiloni

MTU ALIYETAMANI DHAHABU
Bansir alikuwa ni mtengenezaji wa magari ya kukokotwa na farasi huko Babiloni. Alikuwa ni mtu ambaye hakuridhika na hali ya maisha yake. Siku hii alikuwa amekaa juu ya ukuta mfupi unaozunguka nyumba yake. Aliangalia kwa huzuni kajumba kake na eneo analofanyia kazi ambapo kulikuwa na gari la farasi ambalo halijaisha kutengenezwa.

Mara kwa mara mke wake alionekana mlangoni. Kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia ilimkumbusha kuwa unga ulikuwa unakaribia kuisha hivyo anatakiwa kufanya kazi gari lile liishe. Agongelee, akate, apige msasa, apige rangi aweke matairi na kupamba kisha alipeleke kwa mteja wake ili apate pesa.

Hata hivyo mwili wake mnene na uliojengeka uliendelea kukaa kizembe juu ya ukuta. Akili yake nzito ilikuwa inahangaika kutatua tatizo ambalo hakuweza kupata jibu lake.

Joto na jua kali la kwenye bonde la mto Efrati lilikuwa likimpiga bila huruma. Matone ya jasho kama shanga yalimtoka kwenye paji la uso. Yalimtiririka mpaka kwenye kifua chake chenye vinyweleo vingi bila yeye mwenyewe kujua wala kutilia maanani.

Mbali na nyumba yake kulikuwa na jumba kubwa la mfalme lililokuwa limezungukwa na ukuta. Pembeni yake kulikuwa na jengo refu lililopakwa rangi, hekalu la Bel(bwana, Marduki). Katikati ya majengo makubwa na ya kifahari namna hiyo, kulikuwa na kajumba kake na tujumba tungine tuchafu zaidi.

Babiloni ulikuwa ni mji wa namna hiyo, mchanganyiko wa ufahari na uchafu. Utajiri mkubwa na umaskini wa kutupwa. Vilichanganyika na kujazana pamoja bila mpango ndani ya ukuta wa jiji.

Nyuma yake, japo hakuangalia kulikuwa na kelele za magari ya kukokotwa na farasi ya watu matajiri yakipita sambamba na wafanyabiashara waliovaa makubazi na ombaomba waliokuwa peku.

Matajiri walilazimika kupaki pembeni kupisha msafara mrefu wa watumwa waliobeba maji kwaajili ya kazi za mfalme. Kila mmoja wao alibeba mfuko mzito wa maji uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya mbuzi. Walikuwa wanayapeleka kwenye bustani zinazoelea za Babiloni.

Bansir alikuwa amezama kwenye mawazo kuhusu shida zake wala hakukazia akili vurugu za mji. Alishtushwa na mlio wa kinubi ambao haukuwa mgeni kwake. Aligeuka na kukutana na uso unaotabasamu wa rafiki yake kipenzi, Kobbi, mwanamuziki.

"Baraka za Miungu ziwe nawe rafiki yangu" alisalimia Kobbi

"Inaonekana Miungu ni wema sana kwako hadi huna haja ya kufanya kazi! Nafurahia bahati yako maana na mimi naweza kufaidika nayo. Bila shaka mifuko yako imetuna, vinginevyo ungekuwa unapiga kazi saa hizi. Nikopeshe shekeli mbili, nitakulipa jioni baada ya karamu ya matajiri"

"Yaani ningekuwa na shekeli mbili nisingekukopesha" akajibu Bansir kwa unyonge. "Nisingekopesha mtu yeyote, hata wewe nisingekukopesha. Hizo ndizo zingekuwa kila kitu kwangu na mtu hawezi kukopesha kila kitu alichonacho, hata kwa rafiki yake kipenzi"
"Unasema!" Akashangaa Kobbi. "Inamaana hauna hata shekeli moja mfukoni lakini umekaa juu ya ukuta kama sanamu. Kwanini usimalizie hilo gari? Sasa utapataje mahitaji yako? Siyo kwa mtindo huo rafiki yangu. Nguvu zako za siku zote ziko wapi? Kuna kitu kimekukwaza, Miungu imekuletea matatizo?"

"Itakuwa ni mateso toka kwa Miungu" alikubali Bansir. "Ilianza kama ndoto, ndoto isiyo na maana. Ndani ya ndoto nilikuwa ni mtu wa maana. Kwenye mkanda wangu wa kiunoni ilining'inia pochi nzuri iliyojaa pesa. Kulikuwa na pesa nyingi kiasi kwamba ningeweza kugawia ombaomba bila kujali kuishiwa; nilikuwa na dhahabu zilizonifanya nijihisi salama hata kwa siku za usoni na wala sikuogopa kutumia pesa. Nilikuwa ni mtu niliyeridhika sana. Usingenijua kama ni mtu mwenye bidii ya kazi wala mke wangu usingemtambua. Uso wake haukuwa na makunyanzi na uling'ara kwa furaha, alikuwa mwanamwali tena, kama alivyokuwa mwanzo nilipomuoa."

"Ndoto tamu kweli" akasema Kobbi. "Lakini kwanini ndoto tamu hivyo ikufanye ukae juu ya ukuta kama sanamu?"

"Hilo ndilo swali! Nilipoamka na kukumbuka jinsi mifuko yangu ilivyo mitupu, hisia za uasi na kutojali zikaniingia. Ngoja tuongelee hilo suala pamoja. Kama mabaharia wasemavyo, mimi na wewe tupo ndani ya mtumbwi mmoja. Wakati tukiwa wavulana tulijifunza pamoja kwa kuhani. Tulipokuwa vijana tulifurahia maisha pamoja. Na katika utu uzima tumekuwa marafiki wa karibu.

Tumekuwa watu wa kuridhika. Tumeridhika kufanya kazi kwa masaa mengi na tunatumia mapato yetu kwa uhuru. Tumepata pesa nyingi kwa miaka yote tuliyofanya kazi lakini furaha ya utajiri tunaipata ndotoni tu. Bah! Tunatofauti gani na kondoo wasioelewa kitu? Tunaishi kwenye mji tajiri zaidi duniani. Wasafiri wanasema hakuna mji unaofanana nao kwa utajiri lakini sisi hatuna kitu. Baada ya kufanya kazi ngumu kwa nusu ya maisha yangu, mimi, wewe na rafiki zetu wengine, hatuna kitu,'

"Naweza kuazima shekeli mbili na nitakulipa jioni? Nilijibuje? Nilisema kuwa hii hapa? Hapana, nilikubali kuwa mifuko yangu haina kitu kama yako tu."

"Shida yetu nini? Kwanini hatuwezi kuwa na fedha na dhahabu zaidi ya zinazotosha nguo na chakula tu?"

"Fikiria kuhusu wana wetu" aliendelea Bansir. "Je, hawafuati hatua zetu? Si kwamba wao, familia zao, na familia za watoto wao wataishi katikati ya dhahabu na utajiri kama sisi lakini wataridhika na kunywa maziwa mgando ya mbuzi na uji tu?"
[emoji419][emoji419]
 
Back
Top Bottom