Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

TAJIRI WA BABELI

Muandishi: George S. Clason's, 1926.
Mtafsiri: Pictuss.

Email: pictuspublishers@gmail.com.

©Pictuss2021.

Haki zote zimehifadhiwa. Hakuna sehemu yoyote ya tafsiri hii inayoweza kunakiliwa, kutolewa kivuli(photocopy), kuhamishwa, kurekodiwa au kutolewa kwa namna yeyote bila ya taarifa ya awali ya kimaandishi ya mtafsiri.


UTANGULIZI

YALIYOMO

Mtu aliyetamani dhahabu
Tajiri wa Babiloni
Tiba saba za pochi tupu
Kutana na Mungu wa bahati
Sheria tano za pesa
Mkopesha pesa wa Babiloni
Kuta za Babiloni
Mfanyabiashara ya ngamia wa Babiloni
Mabamba ya vigae
Mtu mwenye bahati zaidi katika Babiloni

MTU ALIYETAMANI DHAHABU
Bansir alikuwa ni mtengenezaji wa magari ya kukokotwa na farasi huko Babiloni. Alikuwa ni mtu ambaye hakuridhika na hali ya maisha yake. Siku hii alikuwa amekaa juu ya ukuta mfupi unaozunguka nyumba yake. Aliangalia kwa huzuni kajumba kake na eneo analofanyia kazi ambapo kulikuwa na gari la farasi ambalo halijaisha kutengenezwa.

Mara kwa mara mke wake alionekana mlangoni. Kwa jinsi alivyokuwa akimuangalia ilimkumbusha kuwa unga ulikuwa unakaribia kuisha hivyo anatakiwa kufanya kazi gari lile liishe. Agongelee, akate, apige msasa, apige rangi aweke matairi na kupamba kisha alipeleke kwa mteja wake ili apate pesa.

Hata hivyo mwili wake mnene na uliojengeka uliendelea kukaa kizembe juu ya ukuta. Akili yake nzito ilikuwa inahangaika kutatua tatizo ambalo hakuweza kupata jibu lake.

Joto na jua kali la kwenye bonde la mto Efrati lilikuwa likimpiga bila huruma. Matone ya jasho kama shanga yalimtoka kwenye paji la uso. Yalimtiririka mpaka kwenye kifua chake chenye vinyweleo vingi bila yeye mwenyewe kujua wala kutilia maanani.

Mbali na nyumba yake kulikuwa na jumba kubwa la mfalme lililokuwa limezungukwa na ukuta. Pembeni yake kulikuwa na jengo refu lililopakwa rangi, hekalu la Bel(bwana, Marduki). Katikati ya majengo makubwa na ya kifahari namna hiyo, kulikuwa na kajumba kake na tujumba tungine tuchafu zaidi.

Babiloni ulikuwa ni mji wa namna hiyo, mchanganyiko wa ufahari na uchafu. Utajiri mkubwa na umaskini wa kutupwa. Vilichanganyika na kujazana pamoja bila mpango ndani ya ukuta wa jiji.

Nyuma yake, japo hakuangalia kulikuwa na kelele za magari ya kukokotwa na farasi ya watu matajiri yakipita sambamba na wafanyabiashara waliovaa makubazi na ombaomba waliokuwa peku.

Matajiri walilazimika kupaki pembeni kupisha msafara mrefu wa watumwa waliobeba maji kwaajili ya kazi za mfalme. Kila mmoja wao alibeba mfuko mzito wa maji uliokuwa umetengenezwa kwa ngozi ya mbuzi. Walikuwa wanayapeleka kwenye bustani zinazoelea za Babiloni.

Bansir alikuwa amezama kwenye mawazo kuhusu shida zake wala hakukazia akili vurugu za mji. Alishtushwa na mlio wa kinubi ambao haukuwa mgeni kwake. Aligeuka na kukutana na uso unaotabasamu wa rafiki yake kipenzi, Kobbi, mwanamuziki.

"Baraka za Miungu ziwe nawe rafiki yangu" alisalimia Kobbi

"Inaonekana Miungu ni wema sana kwako hadi huna haja ya kufanya kazi! Nafurahia bahati yako maana na mimi naweza kufaidika nayo. Bila shaka mifuko yako imetuna, vinginevyo ungekuwa unapiga kazi saa hizi. Nikopeshe shekeli mbili, nitakulipa jioni baada ya karamu ya matajiri"

"Yaani ningekuwa na shekeli mbili nisingekukopesha" akajibu Bansir kwa unyonge. "Nisingekopesha mtu yeyote, hata wewe nisingekukopesha. Hizo ndizo zingekuwa kila kitu kwangu na mtu hawezi kukopesha kila kitu alichonacho, hata kwa rafiki yake kipenzi"
"Unasema!" Akashangaa Kobbi. "Inamaana hauna hata shekeli moja mfukoni lakini umekaa juu ya ukuta kama sanamu. Kwanini usimalizie hilo gari? Sasa utapataje mahitaji yako? Siyo kwa mtindo huo rafiki yangu. Nguvu zako za siku zote ziko wapi? Kuna kitu kimekukwaza, Miungu imekuletea matatizo?"

"Itakuwa ni mateso toka kwa Miungu" alikubali Bansir. "Ilianza kama ndoto, ndoto isiyo na maana. Ndani ya ndoto nilikuwa ni mtu wa maana. Kwenye mkanda wangu wa kiunoni ilining'inia pochi nzuri iliyojaa pesa. Kulikuwa na pesa nyingi kiasi kwamba ningeweza kugawia ombaomba bila kujali kuishiwa; nilikuwa na dhahabu zilizonifanya nijihisi salama hata kwa siku za usoni na wala sikuogopa kutumia pesa. Nilikuwa ni mtu niliyeridhika sana. Usingenijua kama ni mtu mwenye bidii ya kazi wala mke wangu usingemtambua. Uso wake haukuwa na makunyanzi na uling'ara kwa furaha, alikuwa mwanamwali tena, kama alivyokuwa mwanzo nilipomuoa."

"Ndoto tamu kweli" akasema Kobbi. "Lakini kwanini ndoto tamu hivyo ikufanye ukae juu ya ukuta kama sanamu?"

"Hilo ndilo swali! Nilipoamka na kukumbuka jinsi mifuko yangu ilivyo mitupu, hisia za uasi na kutojali zikaniingia. Ngoja tuongelee hilo suala pamoja. Kama mabaharia wasemavyo, mimi na wewe tupo ndani ya mtumbwi mmoja. Wakati tukiwa wavulana tulijifunza pamoja kwa kuhani. Tulipokuwa vijana tulifurahia maisha pamoja. Na katika utu uzima tumekuwa marafiki wa karibu.

Tumekuwa watu wa kuridhika. Tumeridhika kufanya kazi kwa masaa mengi na tunatumia mapato yetu kwa uhuru. Tumepata pesa nyingi kwa miaka yote tuliyofanya kazi lakini furaha ya utajiri tunaipata ndotoni tu. Bah! Tunatofauti gani na kondoo wasioelewa kitu? Tunaishi kwenye mji tajiri zaidi duniani. Wasafiri wanasema hakuna mji unaofanana nao kwa utajiri lakini sisi hatuna kitu. Baada ya kufanya kazi ngumu kwa nusu ya maisha yangu, mimi, wewe na rafiki zetu wengine, hatuna kitu,'

"Naweza kuazima shekeli mbili na nitakulipa jioni? Nilijibuje? Nilisema kuwa hii hapa? Hapana, nilikubali kuwa mifuko yangu haina kitu kama yako tu."

"Shida yetu nini? Kwanini hatuwezi kuwa na fedha na dhahabu zaidi ya zinazotosha nguo na chakula tu?"

"Fikiria kuhusu wana wetu" aliendelea Bansir. "Je, hawafuati hatua zetu? Si kwamba wao, familia zao, na familia za watoto wao wataishi katikati ya dhahabu na utajiri kama sisi lakini wataridhika na kunywa maziwa mgando ya mbuzi na uji tu?"
Mdau hii ngoma hard copy inapatikana wapi?
 
Alipomaliza kuongea mmoja wa rafiki zake akasema, "Ulikuwa na bahati sana kwa Algamisha kukufanya mrithi wake."

"Nilikuwa na bahati kwa sababu nilikuwa na matamanio ya kufanikiwa hata kabla hatujaonanana naye. Je, sikuonyesha uwezo wangu kwa kutunza sehemu ya kumi ya pato langu kwa miaka minne? Unawezaje kumuita mvuvi ambaye kwa miaka mingi amesoma tabia za samaki na anajua majira mazuri ya kushusha nyavu ana bahati?

Bahati ni Mungu katili ambaye ambaye hapotezi muda na wale ambso hawako tayari."

"Ila Arkad una moyo mgumu sana. Maana baada ya kupoteza akiba yako ya mwaka wa kwanza bado hukukata tamaa. Upekee wako upo hapo," alisema rafiki yake mwingine.

"Moyo mgumu!" Alisema Arkad akishangaa. Upuuzi! Unafikiri moyo mgumu unaweza kumpa mtu nguvu za kunyanyua mzigo ambao ngamia hawezi, au kukokota kitu ambacho ng'ombe wa kukokota hawezi hata kukitikisa? Si moyo mgumu bali nia ya kufanya jambo ulilolipanga mpaka likamilike. Kama nimejiwekea lengo, hata liwe gumu kiasi gani nitahakikisha nalikamilisha. Vinginevyo nawezaje kujiamini kutimiza mambo muhimu?

"Nikijiambia, 'kwa siku miamoja, nikipita kwenye daraja la kuelekea mjini nitaokota jiwe dogo barabarani na kulitupa kwenye maji, nitafanya hivyo. Iwapo siku ya saba ikifika na nikasahau kutupia jiwe nitajiambia, 'haina shida kesho nitatupia mawili?' Si ni kitu kile kile? Hapana, nitarudi na kutupia jiwe mtoni. Wala ikifika siku ya ishirini siwezi sema, 'Arkad, hili ni jambo la kijinga, inakusaidia nini kurusha jiwe mtoni kila siku? Tupia yote kwa wakati mmoja na uwe umemalizana na hili jambo. Hapana, sitasema wala kufanya hivyo. Nikijiwekea lengo lazima nilikamilishe. Kwa sababu hiyo, nipo makini sana kutoanzisha vitu vigumu na visivyowezekana kwa sababu sipendi kujitesa."

Hapo rafiki yake mwingine akasema. "Kama unayosema ni kweli, na kwa jinsi ulivyoeleza inaonekana ni kweli, sasa ni rahisi namna hiyo, na kila mtu akifanya hayo, kutakuwa na utajiri wa kutosha wote?"

"Utajiri hukua pale watu wanapofanya kazi," akajibu Arkad. "Iwapo tajiri amejenga jumba kubwa, pesa alizotumia zinapotea? Hapana, mfyatua matofali anapata kidogo na vibarua nao wanapata kidogo. Wasanifu nao hupata kidogo na kila mtu aliyefanya kazi kwenye ujenzi wa nyumba hiyo hupata kidogo. Lakini je, nyumba iliyojengwa haiwi na thamani sawa na dhahabu iliyotumika? Na ardhi ambamo imejengwa haipandi thamani kwa sababu sana ina nyumba? Na ardhi inayopakana nayo haiongezeki thamani kwa sababu inapakana na jumba kubwa? Utajiri hukua kimaajabu sana. Hakuna anayeweza kutabiri mwisho wake. Je, wafoenike hawajajenga majiji makubwa kwenye pwani za jangwani kutokana na utajiri unaoletwa na meli zao za biashara?

"Kwa hiyo unatupa ushauri gani ju ya cha kufanya ili nasi tuwe matajiri? Maana miaka inaenda na uzee unaingia lakini hatuna tulichowekeza." Alisema rafiki mwingine tena.

"Nawashauri kuchukua ushauri wa Algamish na kujiambia, 'sehemu fulani ya pato langu ni yangu.' Sema hivyo asubuhi unapoamka, sema mchana, sema na usiku. Sema kila saa ya siku. Jiambie hivyo hadi maneno hayo yatokee kama herufi za moto angani.
 
Jaza wazo hili ndani yako na tunza kiasi unachoona kinafaa ila isiwe chini ya moja ya kumi ya pato lako. Ikiwa kuna ulazima, badili matumizi yako ili kufanikisha hili. Baada ya muda utaanza kuhisi hisia za utajiri. Akiba inayokua itakuletea furaha, furaha ya kumiliki kitu chako mwenyewe. Kadri hazina yako inavyokuwa ndivyo utakavyochochewa kuweka zaidi. Utapata furaha maishani na nguvu ya kutafuta zaidi itakuingia. Je, kadri unavyopata zaidi si na kiasi unachotunza kitaongezeka?

"Baada ya hapo jifunze jinsi ya kufanya akiba yako ikutumikie. Ifanye mtumwa wako. Wafanye watoto wake na watoto wa watoto wake wakutumikie.

"Hakikisha una kipato kwaajili ya siku zijazo. Waangalie wazee na kumbuka kuwa siku zijazo nawe utakuwa mzee. Hivyo wekeza kwa tahadhari ili hazina yako isipotee. Biashara zenye kudai zina faida kubwa ni mtego na udanganyifu. Ni nyimbo zinazoimbwa ili kumvuta mtu asiye makini kwenye hasara na majuto.

Hakikisha familia yako haitateseka iwapo Miungu wakikuita. Unaweza fanya hivyo kirahisi kwa kutunza pesa kidogokidogo mara kwa mara. Mtu mwenye fikra za mbele hasubiri kupata kiasi kikubwa ndiyo akitunze au akiwekeze kwa wakati ujao.

"Jadiliana na watu wenye hekima. Tafuta ushauri kutoka kwa wale wanaofanya kazi zihusuzo pesa kila siku. Hao watakusaidia kuepuka makosa kama niliyofanya mimi kwa kumpa pesa zangu Azmur, mfyatua matofali. Faida ndogo penye usalama ni bora kuliko faida kubwa lakini penye hatari ya kupoteza mali zako.

"Furahia maisha ungali bado upo duniani. Usijibane kupita kiasi ili kutunza pesa, na usijaribu kutunza kiasi kikubwa kuliko uwezo wako. Kama sehemu ya kumi ndiyo unayoweza kutunza bila kupata taabu basi ridhika na kutunza kiwango hicho tu. Ishi kulingana na kipato chako ila usiwe bahili na kuogopa kufanya matumizi. Maisha ni matamu na yana vitu vingi vya kufurahia."

Rafiki zake wakamshukuru na kwenda zao. Wengine walikuwa kimya kwa sababu haikuwaingia akilini na hawakuweza kuelewa. Wengine walidhihaki kwa kusema "mtu tajiri hivyo alitakiwa kugawana utajiri wake na rafiki zake wasio na kitu." Lakini wengine walikuwa wamepata mwanga mpya. Walielewa kuwa, Algamish alirudi kwa Arkad mara nyingi sababu alikuwa anataka kumuona mtu akitoka gizani hadi kwenye mwanga. Mtu huyo alipopata mwanga fursa zilimsubiria, hakuna anayeweza kutumia fursa hizo mpaka afanye bidii kupata uelewa kwanza.

Hawa ndiyo ambao baadaye walikuwa wakimtembelea Arkad kila mwaka. Aliwashauri na kuwapa maarifa yake bure kama ambavyo watu wenye maarifa na busara nyingi hufanya. Pia aliwasaidia kuwekeza akiba zao ili wapate faida nzuri bila ya kuingia katika hatari ya kupoteza pesa zao wala kuingia kwenye uwekezaji usioleta faida. Maisha ya watu hawa yalibadilika siku ile walipogundua ukweli uliotoka kwa Algamish kwenda kwa Arkad. Kutoka kwa Arkad hadi kwao.

Sehemu fulani ya pato unalopata ni yako.

Mwisho wa sura ya pili.
 
TIBA SABA DHIDI YA POCHI TUPU

Ufahari wa Babiloni umesifika kwa vizazi vingi sana. Sifa zake za kuwa jiji tajiri kuliko yote na utajiri wake usio na kipimo zimesimuliwa vizazi na vizazi.

Hata hivyo, jiji hili halikuibuka tu na kuwa tajiri. Utajiri wa Babiloni ulitokana na maarifa ya watu wake. Kwanza kabisa walijifunza jinsi ya kupata utajiri.

Mfalme Sargon wa Babiloni aliporudi baada ya kuwashinda waelami alikuta jiji lipo kwenye hali mbaya sana. Mshauri wa mfalme alimuelezea hali hiyo, alisema:
"Kwa miaka mingi kumekuwa na ukuaji wa uchumi na watu wamekuwa matajiri sababu ya wewe kujenga mifereji ya unwagiliaji na mahekalu makubwa ya Miungu. Sasa baada ya miradi hiyo kukamilika watu hawana kazi za kuwaingizia kipato.

"Wafanyakazi wamekaa tu. Wafanyabiashara hawana wateja. Wakulima hawana wa kumuuzia mazao yao na raia hawana pesa za kutosha kununua chakula."

"Lakini pesa zote tulizotumia kwenye miradi ya serikali zimekwenda wapi?" Akahoji mfalme.

"Nina wasiwasi zimeishia mikononi mwa matajiri wachache. Zimepita mikononi mwa watu haraka kama vile maziwa ya mbuzi yanavyopita kwenye chujio. Sasa mzunguko wa pesa umekuwa chini na watu wetu hawana cha kuonyesha kutokana na mapato yao."

Mfalme alifikiria kwa muda kidogo na kisha akasema. "Imekuwaje watu wachache wameweza kumiliki pesa nyingi kiasi hicho?"

"Kwa sababu wanajua jinsi ya kupata pesa," akajibu yule mshauri.

"Mtu anayejua jinsi ya kufanikiwa hawezi kulaumiwa akifanikiwa, na wala si haki kuchukua mali ya mtu aliyeipata kihalali na kuwapa wazembe."

"Lakini kwanini iko hivi," akahoji mfalme. "Kwanini watu wote hawajifunzi mbinu za kufanikiwa ili na wao wawe matajiri na kufanikiwa?"

"Mtukufu mfalme, hilo linawezekana, lakini ni nani atawafundisha? Hawawezi kuwa makuhani, hawajui chochote kuhusu mbinu za kutengeneza pesa."

"Sasa kwenye mji wetu ni nani anafahamu namna ya kuwa tajiri?" Akauliza mfalme.

"Hilo linajijibu lenyewe mtukufu mfalme, ni nani aliye tajiri kuliko wote hapa Babiloni?"
"Umenena vema mshauri wangu, ni Arkad. Ndiye mtu tajiri kuliko wote. Kesho mlete nionane naye."

Kesho ilipofika Arkad alifika mbele ya mfalme. "Arkad ni kweli kuwa wewe ndiye tajiri kuliko wote hapa Babiloni?"

"Na mimi nimesikia hivyo mtukufu mfalme na sijaona mtu wa kubisha."
"Umewezaje kuwa tajiri namna hiyo?"
"Kwa kutumia vizuri fursa zilizopo wazi kwa watu wote kwenye mji wetu huu."
"Kwa hiyo hapo mwanzo hukuwa na utajiri wowote?"
"Sikuwa na chochote zaidi nia ya kuwa tajiri, sikuwa na kingine zaidi ya hicho."

"Sikiliza Arkad" akasema mfalme. "Mji wetu hauna furaha. Sababu kuu ni kuwa watu wachache ndiyo wanajua namna ya kuwa na utajiri na hawa wameuhodhi. Walio wengi hawana ujuzi wa kutunza pesa wanazopata. Ni nia yangu kufanya Babiloni kuwa mji tajiri zaidi duniani, unatakiwa kuwa mji wa matajiri. Kwa hiyo tunatakiwa kuwafundisha watu namna ya kupata utajiri.

Hebu niambie Arkad, kuna siri ya namna ya kuwa tajiri? Watu wanaweza kufundishwa siri hiyo?"

"Inawezekana mtukufu mfalme. Kile mtu mmoja anachokijua inawezekana kufundishwa kwa wengine."
"Arkad umeongea vitu nilivyotaka kusikia. Je unaweza kufanya hiyo kazi? Unaweza kufundisha hiyo elimu kwa wakufunzi, ambao nao watafundisha wengine mpaka kuwe na walimu wa kutosha kumfundisha kila raia wangu maarifa hayo?"

"Arkad akainama kwa heshima na kusema, "mimi ni mtunishi wako, nitafanya kama ulivyoagiza. Maarifa yote niliyonayo nitayafundisha kwa ajili ya usitawi wa raia wenzangu na utukufu wa mfalme wangu. Ninaomba mshauri wako aniandalie darasa la watu mia moja nami nitawafundisha tiba saba zilizofanya niwe na pochi iliyotuna, pochi ambayo ilikuwa tupu kuliko zote katika Babiloni.
 
Baada ya siku arobaini, na kama mfalme alivyoagiza, wale wateule mia moja walikuwa wamekusanyika kwenye ukumbi mkubwa ulio ndani ya Hekalu la Elimu. Walikuwa wamekaa kwenye nusu duara wakipendeza kwa mavazi yao ya rangi mbalimbali. Arkad likaa pembeni ya kiti kidogo ambacho juu yake chetezo cha kuabudia kilikuwa kikitoa moshi wenye harufu nzuri sana.

"Tazama mtu tajiri zaidi katika Babiloni," alinong'ona mwanafunzi mmoja huku akimgusa mwenzake Arkad alipokuwa anasimama. "Ni mtu kama sisi tu!"

"Nikiwa kama mtumishi mtiifu wa mfalme wetu," alianza kuongea Arkad. "Ninasimama mbele yenu kufanya kazi yake. Kwa sababu zamani nilikuwa kijana aliyetamani kuwa tajiri, na kwa sababu nilipata maarifa yaliyoniwezesha kuupata, ameniagiza niwafundishe maarifa niliyonayo.

"Utajiri wangu ulianzia chini sana. Sikuwa na cha ziada, nilikuwa kama ninyi au raia wengine wa Babiloni."
"Sehemu kuu ya kutunza hazina yangu ilikuwa ni pochi yangu. Nilichukia jinsi ilivyokuwa tupu bila kazi yoyote. Nilitamani ijae na itune, ikilia kwa sauti za dhahabu zilizogongana ndani yake. hivyo nikatafuta tiba zote dhidi ya pochi tupu, nikapata tiba saba.

"Kwa nyinyi mliokusanyika hapa mbele yangu. Nitawafundisha tiba hizo saba na, hizo zinatakiwa kujulikana na watu wote wanaotaka utajiri. Kila siku, kwa siku saba nitawafundisha moja ya tiba hizo.

"Msikilize kwa makini yale nitakayowafundisha. Mjadiliane kati yenu. Jifunzeni mambo haya kikamilifu ili hata nyinyi yaweze kuweka mbegu ya utajiri kwenye pochi zenu. Mwanzo, kila mmoja wenu atatakiwa kuanza kujenga utajiri wake. Mkiweza kufanikiwa hilo ndipo mtaweza kufundisha wengine.

"Nitawafundisha jinsi ya kutunisha pochi zenu kwa njia rahisi. Hii ndiyo ngazi ya kwanza kuelekea hekalu la utajiri. Hakuna mtu anaweza kupanda ngazi iwapo hawezi kuweka mguu wake kwenye ngazi ya kwanza.
"Sasa na tuone tiba ya kwanza.

TIBA YA KWANZA - Anza kutunisha pochi yako.

Arkad akaongea na mtu aliyekaa mstari wa pili, aliyeonekana yuko makini sana.
"Rafiki yangu, unafanya kazi gani?"

"Mimi ni muandishi wa kumbukumbu kwenye mabamba ya vigae." Alijibu mtu yule.
"Hata mimi kazi hiyo ndiyo iliyonipatia pesa zangu za kwanza. Una fursa kama yangu ya kujenga utajiri."
Kisha akaongea na mtu aliyekuwa na uso mwekundumwekundu aliyekuwa amekaa siti ya nyuma.
"Ndugu tuambie, unapataje mkate wako wa kila siku?"
"Mimi nauza nyama. Nanunua mbuzi toka kwa wafugaji, nawachinja na kuuza nyama. Ngozi huwa nawauzia watengeneza viatu."
"Sababu na wewe una kazi na kipato, nawe pia una fursa ya kufanikiwa kama mimi."
Arkad aliuliza kazi ya kila mmoja wao. Alipomaliza alisema:

"Mnaweza kuona kuwa, kuna kazi nyingi za kufanya ili kujipatia kipato. Kila njia ya kujipatia kipato ni kijito cha dhahabu ambacho kinaingia kwenye pochi.
Kwahiyo, kwenye kila pochi ya mmoja wenu kuna kijito cha pesa kinachotiririka. Wengine kwa wingi na wengine kwa uchache kulingana na uwezo wa kila mtu, si ndivyo ilivyo?

Hapo walikubaliana naye kuwa asemayo ni kweli. Hivyo Arkad akaendelea "iwapo kila mmoja wenu atakuwa na nia ya kuwa tajiri, je, si busara kutumia chanzo cha utajiri ambacho tayari anacho?
Hili nalo wakakubaliana naye.
Hapo Arkad akamgeukia mtu mmoja mnyenyekevu aliyejitambulisha kuwa anafanya biashara ya mayai. "Mfano ukichukua kikapu kimoja na kuweka humo mayai kumi kila siku asubuhi na kila jioni ukatoa mayai tisa nini kitatokea?"
"Baada ya muda kikapu kitajaa kupita kiasi." Akajibu muuza mayai.
"Kwa nini?"
"Kwa sababu kila siku naweka yai moja zaidi ya ninayotoa."
Arkad aliligeukia darasa huku akitabasamu. "Kuna mtu hapa ana pochi tupu?"
Kwanza wanafunzi walionyeshwa kushangazwa kisha wakacheka na mwishowe wakapunga pochi zao hewani kwa pamoja.
"Sawa!" Akaendelea Arkad, "sasa nitawaambia tiba ya kwanza ya pochi tupu. Fanyeni kama nilivyo mshauri muuza mayai. Kila ukiweka sarafu kumi kwenye pochi basi chukua tisa tu kwa matumizi yako. Pochi yako itaanza kutuna mara moja. Uzito wa pochi yako utakuwa mzuri mikononi mwako utakuburudisha moyoni.

"Usidharau kitu nisemacho kwa sababu kinaonekana ni rahisi. Mara zote ukweli huwa rahisi. Niliwaambia kuwa nitawaeleza niliwezaje kuwa tajiri, hivyo ndivyo nilivyoanza. Mimi mwenyewe nilikuwa na pochi tupu na niliichukia kwa sababu haikuwa na kitu chochote cha maana. Lakini nilivyoanza kuweka kumi na kutoa tisa, ilianza kutuna. Nanyi itakuwa hivyohivyo.

"Sasa niwaambie kitu cha ajabu kilichonitokea na mpaka sasa sikielewi. Nilipoacha kutumia zaidi ya tisa ya kumi ya pato langu niliishi kama zamani tu, sikupungukiwa chochote. Pia cha kushangaza zaidi, nikaanza kupata pesa kirahisi kuliko mwanzo.
Bila shaka ni sheria za Miungu kumpa pesa kirahisi yule anayetunza sehemu ya pato lake. Yule mwenye mifuko mitupu pesa humuepuka.

"Ni kitu gani unatamani sana? Kutimiza matamanio ya kila siku. Vito, nguo nzuri, chakula kingi, vitu ambavyo vinakuja na kupita. Au vitu vya kudumu, dhahabu, ardhi, mifugo au uwekezaji wenye kuingiza pesa? Pesa unayotoa kwenye pochi yako huleta hivyo vitu vya kwanza. Pesa unayoiacha kwenye pochi huleta hivyo vitu vya pili.

"Hii ndiyo tiba niliyoigundua: 'kwa kila sarafu kumi nilizoweka kwenye pochi, nilitumia tisa tu' jadilianeni kuhusu hili, kama kuna mtu anaona halina ukweli basi kesho tukionana tena aniambie."
 
TIBA YA PILI - Pangilia matumizi yako.

"Wengine kati yenu wameuliza: mtu anawezaje kutunza moja ya kumi ya pato lake wakati pato lote analopata halitoshi kwaajili ya matumizi yake ya lazima?" Arkad alianza kuongea kwenye siku ya pili.
"Jana ni wangapi kati yenu walikuwa na pochi tupu?"
"Wote" darasa lilijibu.
" Lakini si kwamba wote mnapata kipato sawa. Wengine hupata zaidi na wengine wana familia kubwa. Lakini wote pochi zenu zilikuwa tupu. Sasa nitawaambia jambo la kushangaza kuhusu watu. Ni hivi, kile ambacho tunaita 'matumizi ya lazima' mara zote hukua kulingana na kipato chetu kinavyokuwa isipokua tukijizuia.

"Usichanganye matumizi ya lazima na matamanio. Wote hapa na familia zenu mna matamanio mengi kuliko mnayoweza kutimiza. Kwa hiyo, mnaendelea kuyatimiza kadri kipato chenu kinavyoongezeka. Lakini bado mengi yanabaki bila kutimizwa.
"Watu wote wameelemewa na matamanio mengi kuliko wanayoweza kuyatimiza.

Mnafikiri sababu ya utajiri wangu naweza kutimiza matamanio yangu yote? Si kweli. Kuna kikomo cha nguvu zangu. Kikomo cha umbali ninaoweza kusafiri. Kikomo cha ninachoweza kula na kikomo cha mambo ninayoweza kufurahia.
"Kama ambavyo magugu hukua sehemu ambazo mkulima kaacha nafasi kwa mizizi yake kushika ndivyo matamanio hukua kwa mtu anayetamani kuyatimiza.
Matamanio yenu ni mengi lakini mnayoweza kuyatimiza ni machache.

"Chunguzeni kwa makini namna mnavyoishi. Mtakuta mnamatumizi mengi yasiyo ya lazima ambayo mnaweza kuyapunguza au kuyaacha kabisa. Acha kaulimbiu yenu iwe kupata asilimia mia moja ya thamani mnapofanya matumizi.
"Kila mmoja aandike vitu alivyopanga kutumia pesa. Kisha chagua yale matumizi ya muhimu na yale yanayowezekana kwa kutumia tisa ya kumi ya pato lako. Tupilia mbali mengine yote na yaone ni kama matamanio ambayo hayana umuhimu wa kuyatimiza.
"Panga matumizi yako. Usiguse ile moja ya kumi ya kutunishia pochi yako. Kutunza pesa liwe ndiyo tamanio lako kuu. Panga bajeti yako kwa uangalifu mkubwa. Acha ikusaidie katika kutunisha pochi yako.

Hapo mwanafunzi mmoja aliyekuwa na vazi la rangi nyekundu na dhahabu akasimama na kusema, "mimi ni mtu huru. Nafikiri kuwa nina haki ya kufurahia vitu vizuri maishani. Naona kama kupanga matumizi na kuishi kwa bajeti inayonipangia kiasi cha kutumia na kwa matumizi gani ni utumwa. Naona hilo litaharibu furaha yangu maishani na kunifanya niishi kama punda mbeba mizigo tu."

Arkad akamjibu, "rafiki, ni nani atapanga bajeti yako?"

"Nitapanga mimi mwenyewe," akajibu yule bwana.

"Kama ni hivyo, unafikiri punda mbeba mizigo akiambiwa apange pajeti ya mizigo yake atabeba vito, mazuria na dhahabu? Hapana, ataweka nyasi, nafaka na mfuko wa maji kwaajili ya safari ya jangwani.
"Lengo la bajeti ni kutunisha pochi yako. Inakusaidia kupata mahitaji yako ya muhimu na kutimiza matamanio mengine iwapo inawezekana. Inakusaidia kutofautisha mahitaji ya muhimu na matamanio tu. Kama mwanga ndani ya pango lenye giza totoro. Bajeti inakusaidia kuona tobo kwenye pochi yako. Inakusaidia pia kuliziba na kupanga vizuri matumizi kwa mambo ya msingi na starehe.

"Hii ndiyo tiba ya pili kwa pochi iliyo tupu. Panga matumizi yako hadi uwe na pesa ya matumizi ya lazima na pesa ya starehe bila kutumia zaidi ya tisa ya kumi ya pato lako.

TIBA YA TATU - Fanya dhahabu zako ziongezeke.

"Tazama pochi yako imeanza kutuna! Umekuwa na nidhamu ya kutunza moja ya kumi ya pato lako. Umepanga matumizi yako vizuri na umelinda akiba yako. Hatua inayofuata tutajifunza namna ya kufanya hazina yako kufanya kazi na kukua zaidi.

Pesa kwenye pochi ni kitu cha kuridhisha lakini haizalishi kitu chochote. Pesa tuliyopata kwa kutunza ni mwanzo tu. Mapato itakayozalisha ndiyo yatayojenga utajiri wetu. " Hivyo ndivyo alivyoanza Arkad kwenye siku ya tatu.

"Jinsi gani tunaweza fanya pesa zetu zifanye kazi? Uwekezaji wangu wa kwanza haukuwa mzuri. Nilipoteza pesa zote. Nitasimulia hilo baadaye. Uwekezaji wangu wa kwanza ulioleta faida ulikuwa ni mkopo niliompa Agger, mtengeneza ngao. Alikuwa akinunua shaba kwaajili ya kutengeneza ngao, lakini alikuwa hana mtaji wa kutosha hivyo alikuwa akikopa kwa wenye pesa. Alikuwa ni mtu muaminifu, alilipa mikopo yake na riba vizuri mara tu alipouza ngao.

"Kila mara nilipomkopesha, nilimkopesha na ile riba aliyonilipa. Kwa hiyo mtaji wangu uliongezeka na mapato yangu yakaongezeka pia. Lilikuwa jambo la kuburudisha sana kuona pesa zile zikiingia kwenye pochi yangu.

"Nisikilizeni kwa makini'

''Utajiri wa mtu haupo kwenye fedha zilizopo kwenye pochi yake bali kwenye kijito cha dhahabu kinachotiririka kwenda kwenye pochi yake na kuitunisha. Kipato kinachoingia hata akisafiri au asipofanya kazi.

"Nimeweza pata pesa nyingi sana hadi kufikia kuitwa mtu tajiri zaidi. Mkopo wangu kwa Aggar ulikuwa ni somo langu la kwanza juu ya uwekezaji wenye faida. Kutokana na uzoefu nilioupata hapa nikatanua uwekezaji wangu kadri mtaji ulivyokuwa ukiongezeka. Nilianza na kidogo lakini baada ya muda kikawa kikubwa. Utajiri ulimiminika kwenye pochi yangu.

"Tazama! Kutoka kwenye mapato yangu kidogo nilipata umati wa watumwa ambao walifanya kazi ya kuzalisha zaidi. Watoto wao walinitumikia na watoto wa watoto wao nao walinitumikia. Jumla ya pato walilozalisha ilikuwa kubwa sana.
"Dhahabu hukua kwa kasi iwapo inazalisha, kama tu mtakavyoona kwenye mfano ufuatao.

"Kulikuwa na mkulima ambaye mtoto wake wa kwanza alipozaliwa alichukua vipande kumi vya fedha na kwenda kwa mkopesha pesa. Akamwambia aweke ile pesa kwa riba mpaka mtoto wake atakapotimiza miaka ishirini. Mkopesha pesa akakubali na wakakubaliana kuwa riba itakuwa moja ya nne ya ile pesa kila baada ya miaka minne. Mkulima kasema, kwa sababu ile pesa ni kwaajili ya kijana wake basi hata ile riba iongezwe kwenye mtaji.

"Kijana wake alipofikisha miaka ishirini, mkulima akaenda tena kwa mkopesha pesa kuuliza kuhusu fedha alizoweka. Mkopeshaji akamwambia kuwa kwa sababu pesa ilikuwa ikiongezeka kwa riba inayobadilika kulingana na muda, vile vipande kumi vya fedha sasa vimekuwa thelathini na moja na nusu.

"Mkulima akafurahi sana na kwa sababu kwa wakati huo kijana wake hakuhitaji fedha zile akaziacha kwa mkopeshaji. Mtoto wake alipofika miaka hamsini, wakati huo mkulima yule tayari alikuwa ameshafariki mkopeshaji akamlipa mtoto wake vipande mia moja na sitini na saba vya fedha.
"Kwa miaka hamsini, uwekezaji ulikuwa umekua karibia mara kumi na saba.
"Hii ndiyo tiba ya tatu ya pochi tupu. Fanya fedha yako ifanye kazi na ijizalishe kama mnyama wa kufugwa. Ilete kipato ambacho kitatiririka kwenye pochi yako daima.


TIBA YA NNE - linda hazina yako isipotee.

"Bahati mbaya hupendelea sehemu inayong'ara. Dhahabu ndani ya pochi inatakiwa kulindwa kwa nguvu zote vinginevyo itapotea. Kwa hiyo ni busara kuanza na kiasi kidogo, tukiweza kumudu kukiendesha na kukilinda ndipo Miungu itatuamini na kutupatia kikubwa zaidi." Alisema Arkad katika siku ya nne.

"Kila mtu mwenye pesa hushawishika na fursa za kuwekeza kwenye uwekezaji unaodaiwa kuwa na faida kubwa sana. Mara nyingi hushawishiwa na ndugu na marafiki ambao tayari wamo humo.

"Kanuni ya kwanza ya uwekezaji ni usalama wa mtaji wako. Je, ni busara kufuatilia faida kubwa huku ukihatarisha mtaji wako kupotea? Hapana, adhabu ya kutochukua tahadhari ni hasara. Chunguza kwa makini kabla haujatumia hazina yako. Hakikisha hata mambo yakienda kombo bado mtaji wako utakuwa salama. Usidanganyike na ndoto za kuwa tajiri haraka.

"Kabla hujamkopesha mtu hakikisha kama anaweza kulipa na ana sifa hiyo. Usije ukatoa kama zawadi mali uliyoitafuta kwa jasho.
"Kabla hujawekeza kwenye mradi wowote hakikisha unajua mapungufu na hatari za huo mradi.
"Uwekezaji wangu wa kwanza ulikuwa hovyo sana. Pesa niliyotunza kwa mwaka mzima nilimpatia Azmur mfyatua matofali. Alisafiri nchi za mbali hadi jiji la Tiro, aliahidi kununua vito kwa wafoenike. Ilikuwa tuviuze na kugawana faida. Wafoenike walimtapeli na kumuuzia vioo. Hazina yangu ilipotea. Leo, uzoefu wangu unaniambia ubaya wa kumuamini mfyatua matofali kwenye masuala ya vito.

"Kutokana na uzoefu wangu, nimejifunza kuwa: usiamini uelewa wako kupita kiasi na ukaishia kuwekeza hazina yako kwenye mradi mbaya. Ni bora kupata ushauri wa wenye uzoefu wa kuwekeza kwa faida. Kawaida ushauri kama huo hutolewa bure kwa wanaouliza, na una thamani sawa tu na kiwango unachotaka kuwekeza sababu unakiokoa kiwango hicho kisipotee.

"Hii ndiyo tiba ya nne ya pochi tupu. Hii ni ya muhimu sababu inalinda pochi iliyotuna isiwe tupu tena. Linda hazina yako kwa kuwekeza kwenye miradi ambayo mtaji wako utakuwa salama. Wekeza kwenye Miradi ambayo inaleta faida siku zote.

Omba ushauri kwa wenye uelewa na tumia ushauri wa watu wenye uzoefu wa kuwekeza kwa faida. Acha maarifa yao yalinde hazina yako dhidi ya uwekezaji mbaya.
 
Back
Top Bottom