lulu za uru
JF-Expert Member
- Aug 7, 2015
- 2,557
- 3,221
Madini .
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kuwa mtumishi wa Mungu sio lazima uwe na kanisa Kama kina Masanja!! hata kwa kazi hii unayoifanya ni utumushi mkubwa sana!! Kwanza huhitaji sadaka Kama akina Masanja waganga njaa!! wewe unafanya utumishi ulioko moyoni mwako!! sio utumishi was kulazimisha Kama wafanyavyo wengine!!'''Lakini hakuna magumu yasiyo na mwisho. Nilipata kazi ya kusimamia watumwa waliokuwa wakijenga ukuta wa jiji.
'''Kwa kufuata sheria ya kwanza ya pesa nilitunza pesa kutoka kwenye pato langu. Niliendelea kutunza kadri nilivyopata hadi nilipofikisha kipande kimoja cha fedha. Nilipata shida kwa sababu kuna matumizi mengi ya maisha na niliishi kibahili sana. Nilipanga kuwa kabla miaka kumi haijaisha niwe nimepata kiasi cha dhahabu kama kile ulichonipatia.
'''Siku moja mmiliki wa wale watumwa ambaye sasa alikuwa rafiki yangu aliniambia. "Wewe ni kijana bahili sana, hutumii kabisa pesa zako, inamaana pesa zako umetunza tu, hazizalishi?"
'''Ndiyo,' nilimjibu, 'mpango wangu ni kutunza hadi kifike kiasi kama kile alichonipatia baba yangu nami nikakipoteza,'
'''Ni mpango mzuri, lakini unafahamu kuwa pesa unayoitunza inaweza kukuzalishia pesa nyingi zaidi?"
'''Nafahamu lakini naogopa kupoteza pesa zangu kama nilivyopoteza zile alizonipatia baba yangu.'
'''Kama unaniamini basi ninaweza kukufundisha jinsi ya kuwekeza pesa kwa faida,' aliniambia. "Ndani ya mwaka mmoja ukuta huu utakuwa umemalizika kujengwa. Utahitaji shaba kwaajili ya kutengenezea milango kwenye kila lango ili kulinda jiji dhidi ya maadui. Huu ndiyo mpango wangu: tujikusanye na tuchange pesa, kisha tukanunue shaba na tini kutoka migodini na kuileta hapa Ninawi kwaajili ya milango. Mfalme atakaposema 'milango itengenezwe,' basi sisi pekee ndiyo tutakuwa na shaba na tini na tutamuuzia kwa bei nzuri. Hata kama mfalme hatanunua kutoka kwetu tutaweza kuuza kwa watu wengine na kwa bei nzuri.
'''Kwa jinsi alivyonieleza nilikumbuka sheria ya tatu ya pesa. Sheria inayoshauri kuwekeza chini ya uongozi wa watu wenye ujuzi na uzoefu. Sikujutia uamuzi wangu, uwekezaji wetu ulikuwa wa mafanikio makubwa na pesa zangu chache ziliongezeka sana.
'''Baada ya hapo nikakaribishwa kuwa mshirika wa lile kundi na nilishiriki kwenye uwekezaji mwingine mwingi sana. Lilikuwa ni kundi la watu wanaojua jinsi ya kuwekeza pesa kwa faida. Kila mpango wa uwekezaji ulijadiliwa kwa kina kabla ya kuanza. Hawakuwekeza kwenye miradi ambayo kulikuwa na hatari ya kupoteza mtaji wala hawakuwekeza kwenye miradi ambayo haileti faida na ambayo ni ngumu kurejesha mtaji.
'''Vitu vya kipumbavu kama mashindano ya farasi au biashara yangu ya ushirika na yule tapeli hata visingefikiriwa na watu hawa. Mara moja wangejua ubaya wa miradi ile.
'''Kutokana na kushirikiana na watu hawa nilijifunza jinsi ya kuwekeza pesa kwenye miradi yenye faida na salama. Miaka ilivyokwenda ndivyo hazina yangu ilivyozidi kuongezeka kwa kasi. Nilifikisha kile kiasi nilichopoteza mwanzo na kupata na ziada.
'''kutokana na magumu niliyopitia na hatimaye mafanikio nilikuwa nimeona ukweli wa busara zilizokuwepo kwenye zile sheria tano za pesa, na ukweli wa busara ya baba yangu. Zilifanya kazi kila nilipozitumia.
'''Kwa asiyefahamu sheria hizi tano, pesa kwake haiji kirahisi na huondoka haraka. Lakini kwa yule anayezifahamu, pesa huja kirahisi na kumfanyia kazi kama mtumwa muaminifu.
"Nomasir alisimama na kumuonyeshea ishara mtumwa aliyekuwa amesimama nyuma ya kile chumba. Mtumwa alileta mifuko mitatu mizito ya ngozi, akibeba mmoja mmoja. Nomasir aliuchukua mmoja na kuuweka mbele ya baba yake na kusema:
'''Ulinipatia mfuko mmoja wa dhahabu, dhahabu ya Babiloni. Tazama, narudisha kwako dhahabu ya Ninawi yenye uzito uleule. Wote watakubaliana nami kuwa ni mabadilishano sawa.
'''Pia ulinipatia bamba la kigae lililokuwa limeandikwa mambo ya busara juu yake. Tazama! Narudisha mifuko miwili ya dhahabu,' baada ya kusema hayo, alichukua ile mifuko miwili na kuiweka mbele ya baba yake.
'''Nimefanya hivi ili kukuthibitishia ni jinsi gani nathamini hekima na busara zako kuliko dhahabu zako. Ni nani anaweza kupima thamani ya hekima? Bila hekima pesa hupotea haraka lakini mtu mwenye hekima hata kama hana pesa anaweza kuzipata. Mifuko hii mitatu ya dhahabu ni ushahidi kuhusu hilo.
Baada ya karamu, baba yake na mama yake wakaketi vitini kama vile ni mfalme na malkia. Nomasir akasimama mbele yao ili kueleza yale aliyotimiza kwa kipindi cha miaka kumi.
"Mke wa Nomasir, wana wake wawili, rafiki zake na ndugu zake wengine wa ukoo walikaa kwenye zuria nyuma yake, wakisubiri kwa hamu kumsikiliza.
'''Baba yangu,' alianza kusema, ninainama kwa heshima ya busara zako. Miaka kumi iliyopita nilipoanza kuingia utu uzima, uliniagiza niende na nikapambane kuwa mwanaume kati ya wanaume badala ya kuwa mshirika na mrithi tu wa mali yako.
'''Ulinipatia dhahabu na hekima yako. Nikiri kuwa dhahabu uliyonipa sikuweza kuitumia vizuri, ilipukutika yote. Ilikimbia kama vile sungura hukimbia kutoka katika mikono ya mwindaji asiye na uzoefu.
"Baba yake akatabasamu na kusema,' endelea kusimulia, napenda kusikia kwa undani zaidi.'
'''Nilipotoka hapa nikaamua kwenda Ninawi. Kwa sababu ni mji uliokuwa unakua nilitumaini kutakuwa na fursa nyingi. Nilijiunga na msafara wa wafanyabiashara waliokuwa wakielekea huko. Njiani nilipata rafiki wengi na kati yao walikuwapo mabwana wawili wachangamfu. Walikuwa na farasi mweupe mzuri sana.
'''Tulipokuwa safarini, walinisimulia kuwa huko Ninawi kuna tajiri ambaye alikuwa na farasi ambaye hajawahi shindwa mashindanoni. Mmiliki wake alikuwa akijigamba kuwa hakuna farasi mwenye kasi kama wake. Alikuwa tayari kuweka kiasi chochote cha pesa dhidi ya farasi mwingine yoyote wa Babiloni. Rafiki zangu wale waliniambia kuwa, ukilinganisha na farasi waliyekuwa naye, farasi anayesifiwa ni kama punda tu na anaweza kushindwa kirahisi sana.
'''Wakaniambia kuwa kama nitapenda niungane nao katika kuweka pesa juu ya farasi wao dhidi ya farasi wa yule tajiri. Nilivutiwa sana na mpango ule.
'''Farasi wetu alishindwa vibaya na nilipoteza dhahabu nyingi sana.'
Baba yake akacheka baada ya kusikia hivyo.
'''Baadaye nikaja kugundua kuwa ulikuwa ni mpango wa kitapeli. Wale watu walikuwa wakisafiri na misafara ya wafanyabiashara wakitafuta watu wa kuwatapeli. Yule aliyedaiwa kuwa ni tajiri wa Ninawi alikuwa ni mshirika wao na waligawana pesa baada ya kushinda. Utapeli huu wa kijanja ulinifundisha somo la kuwa makini.
'''Baada ya muda mfupi nilipata funzo lingine lakini kwa uchungu vilevile. Kwenye ule msafara kulikuwa na kijana ambaye tulitokea kuwa marafiki wazuri sana. Alionekana kuwa ni mtoto wa kitajiri, alikuwa anaenda Ninawi kuangalia fursa, kama mimi tu. Muda mfupi baada ya kufika Ninawi akaniambia kuwa kuna mfanyabiashara amefariki na duka lake pamoja na bidhaa zake vinaweza kununuliwa kwa bei nafuu sana. Akaniambia tuwe washirika lakini kwanza inampasa kurudi Babiloni kuchukua pesa zake. Akanishawishi kununua biashara ile kwa pesa zangu na kuniambia pesa zake zitatumika kuongezea mtaji hapo baadaye.
'''Siku zilikwenda lakini hakurudi Babiloni kufuata pesa zake na mbaya zaidi alikuwa hajui biashara na ni mtu mwenye matumizi mabaya. Nilimfukuza kwenye biashara lakini tayari hali ya biashara ilikuwa mbaya sana. Bidhaa zilizobaki zilikuwa hazifai kuuzwa na sikuwa na pesa ya kununulia zingine. Niliamua kuuza ile biashara kwa muisraeli mmoja kwa bei ya hasara.
'''Baada ya hapo maisha yalikuwa magumu sana. Nilitafuta kazi lakini sikupata kwa sababu sikuwa na ujuzi wowote. Nililazimika kumuuza mtumwa wangu na baadhi ya nguo zangu ili nipate kula na sehemu ya kulala. Siku zilivyosonga ndivyo maisha yalivyozidi kuwa magumu.
'''Katika siku hizo ngumu nilikumbuka jinsi unavyiniamini. Ulinituma nikawe mtu wa maana na hilo ndilo nililopanga kutimiza.' Baada ya kusikia hayo mama yake alijiziba uso na kulia.
'''Muda huo ndipo nilipokumbuka kuhusu lile bamba ulilonipatia. Nikasoma maneno yake kwa umakini mkubwa, iwapo ningepata busara iliyokuwepo mule kabla ya kuanza kuwekeza basi nisingeweza kupoteza pesa zangu. Nilijifunza sheria zote na kuziweka akilini. Nikajiapisha kuwa iwapo Mungu wa bahati akinibariki tena nitaongozwa na busara iliyojengwa kwa miaka mingi badala ya kufanya mambo bila uzoefu kama ilivyo kawaida ya vijana.
'''Kwa faida ya nyote mliokusanyika hapa usiku wa leo, nitasoma hekima aliyonipa baba yangu kama ilivyoandikwa kwenye bamba alilonipa miaka kumi iliyopita.
Sheria tano za pesa
1. Pesa huja kwa wingi kwa yule ambaye huweka akiba moja ya kumi ya kipato chake. Na kuitumia kuwekeza kwa ajili ya wakati ujao.
2. Pesa hufanya kazi kwa bidii na kwa uaminifu iwapo itampata mtu anayeipatia kazi yenye faida. Hapo itaongezeka kama wanyama wa kufungwa.
3. Pesa hung'ang'ania kukaa kwa mtu mtu anayeilinda na mwenye tahadhari. Mtu anayeomba ushauri kutoka kwa watu wenye ujuzi na uzoefu wa kuitunza.
4. Pesa haikai na hupotea kwa mtu ambaye anawekeza kwenye biashara au mradi ambao haijui vizuri, au kwa mtu ambaye hapati ushauri kutoka kwa wale wenye uzoefu na ujuzi wa kuitunza.
5. Pesa haikai kwa mtu anayeiwekeza kwenye miradi inayodai kutoa faida kubwa kuliko kawaida, wala kwa wale wanaodanganywa na matapeli na watu wajanja wajanja na wale ambao wanawekeza bila kupata ushauri kutoka kwa wale wenye uzoefu, au wale wanaowekeza kwa sababu wanapenda tu miradi ya aina hiyo.
'''Hizi ndizo sheria tano za pesa kama zilivyoandikwa na baba yangu. Ninaweza kusema kuwa zina thamani kuliko pesa yenyewe, kama tu mtakavyoona kwenye kisa changu.
"Hapo Nomasir alimuangalia tena baba yake. 'Nimekusimulia jinsi kutokuwa na uzoefu kulivyonitumbukiza kwenye umaskini na taabu.
HahahahaYaani wengine tumeanza kusoma vitabu muda umekwenda ndio tunashtuka kuhusu formula za fedha
Mkuu tunashukuru sana hakika Mungu akubariki. Binafsi naomba uendelee na huduma hii hata kwa kutuwekea vitabu vingine zaidi ili tuendelee kupata madini ambayo hatukuyapata katika mfumo wetu wa elimu."Hiki hapa," aliendelea kusema Mathon huku akifungua kamba moja, 'Hii ni mali ya Nebaturi, mfanyabiashara ya ngamia. Kila atakapo kununua ngamia wengi kuliko pesa alizonazo huniletea kamba hii nami humkopesha kulingana na mahitaji yake. Ni mtu ninayemuamini sana. Ni mfanyabiashara mzuri na muaminifu hivyo hata bila dhamana mimi humkopesha. Ninawaamini wafanyabiashara wengi hapa Babiloni sababu ya uaminifu wao. Huweka mali zao kama dhamana na kuzikomboa mara tu wakamilishapo biashara. Wafanyabiashara wazuri ni hazina ya mji wetu na ni faida kwangu kuwasaidia kuendelea kufanya biashara na kuzidi kuneemesha mji wetu."
Mathon alichukua kito cha rangi ya ubluu na ukijani na kukitupa chini kwa dharau. "Mdudu kutoka Misri. Aliyekuwa anamiliki hiki hajali kabisa kunilipa. Nikimfuata kumdai anajibu, "nitakulipaje nami nimeandamwa na majanga kila leo? Hata hivyo wewe unapesa za kutosha! Unafikiri nitafanya nini?'
Dhamana ni ya baba yake. Baba yake si mtu tajiri lakini alijinyima na kuweka shamba na mifugo yake kama dhamana ili mwanae afanye biashara. Kijana wake alianza vizuri biashara zake na alikuwa akipata faida lakini akaingiwa na tamaa ya kutaka utajiri wa haraka. Kwa kuwa hakuwa na ujuzi mwingi, biashara yake ikafa.
"Vijana wana malengo makubwa sana. Mara zote wanatafuta njia ya mkato ya kuwa matajiri. Ili kupata utajiri haraka mara nyingi hukopa bila kufikiri.
Kwa kukosa kwao uzoefu hawatambui kuwa deni baya ni shimo refu ambalo unaweza kutumbukia kirahisi lakini ukahangaika kwa siku nyingi ili kutoka. Ni shimo la majuto na huzuni. Ni shimo ambalo jua la mchana huzibwa na mawingu na usiku hufanywa mchungu kwa usingizi wa mang'amung'amu.
Si kwamba nashauri watu wasikope, hapana! Nasisitiza watu wakope lakini iwe kwa jambo la maana. Mimi mwenyewe nilianza kufanya biashara kwa pesa za mkopo.
"Lakini mkopeshaji anapaswa kufanya nini kwa jambo kama la huyu kijana? Kijana mwenyewe amekata tamaa, hafanyi chochote wala hafanyi bidii yoyote kulipa deni. Moyo wangu unakuwa mzito kuchukua shamba na mifugo ya baba yake."
"Umeniambia habari nyingi na nimezifurahia ," alisema Rodan. "Lakini hujajibu swali langu iwapo nimkopeshe vipande vyangu hamsini vya dhahabu mume wa dada yangu? Kumbuka hawa ni ndugu zangu wa karibu sana.
"Dada yako ni mtu anayejitambua nami namheshimu kwa hilo. Lakini kama mume wake angekuja kwangu kuomba nimkopeshe vipande hamsini vya dhahabu lazima ningemuuliza anataka kufanyia nini?
"Kama akisema anataka kuwa mfanyabiashara kama mimi na kuuza vito na samani za gharama nitamuuliza. Unaujuzi gani kuhusiana na biashara? Unajua unakoweza kununua kwa bei rahisi ? Unajua unakoweza kuuza kwa bei nzuri?
Je, shemeji yako anafahamu vitu hivyo?
"Kwakweli hafahamu," akajibu Rodan. "Alikuwa msaidizi wangu kwenye kutengeneza mikuki na amewahi kuwa msaidizi wa dukani."
"Kama ni hivyo nitamwambia kuwa hajachagua kazi yake kwa busara. Mfanyabiashara anatakiwa kuwa na ujuzi wa kazi hiyo. Ana malengo mazuri lakini hayatimiziki, nisingeweza mkopesha pesa zangu.
"Tuseme angejibu kuwa, 'ninafahamu sababu nimekuwa msaidizi wa wafanyabiashara kwa muda mrefu. Ninajua jinsi ya kufika Smyrna na kununua mazuria yaliyoshonwa na wakinamama kwa bei ya chini. Pia nawajua matajiri wengi wa Babiloni ninaoweza kuwauzia kwa faida kubwa,' hapo ningemwambia kuwa 'lengo lako ni zuri na mpango wako unatekelezeka. Kwa hiyo ningekuwa tayari kumkopesha vipande hamsini vya dhahabu iwapo atakuwa na dhamana."
"Iwapo angesema 'sina dhamana yoyote lakini mimi ni muaminifu, nitalipa pesa yako vizuri,' ningemwambia; 'ninathamini kila kipande cha dhahabu nilichonacho. Inaweza tokea wanyang'anyi wakakupora pesa unapoenda Smyrna au kukupora mazuria unaporudi. Si unakuwa huna jinsi ya kunilipa na pesa yangu inakuwa imepotea?'
Asante Mtumishi wa Mungu!!"Hiki hapa," aliendelea kusema Mathon huku akifungua kamba moja, 'Hii ni mali ya Nebaturi, mfanyabiashara ya ngamia. Kila atakapo kununua ngamia wengi kuliko pesa alizonazo huniletea kamba hii nami humkopesha kulingana na mahitaji yake. Ni mtu ninayemuamini sana. Ni mfanyabiashara mzuri na muaminifu hivyo hata bila dhamana mimi humkopesha. Ninawaamini wafanyabiashara wengi hapa Babiloni sababu ya uaminifu wao. Huweka mali zao kama dhamana na kuzikomboa mara tu wakamilishapo biashara. Wafanyabiashara wazuri ni hazina ya mji wetu na ni faida kwangu kuwasaidia kuendelea kufanya biashara na kuzidi kuneemesha mji wetu."