Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Umewahi kusoma kitabu, The Richest Man In Babylon? Ulijifunza nini? Kinasaidia?

Nitaendelea kesho, lazima nimalize kitabu hiki na niki-apply kwenye maisha yangu.
 
"Siku moja, Aligamishi, tajiri mkopesha pesa, alikuja kwa msimamizi wa mji na kuomba apate nakala ya sheria ya tisa. Alisema kuwa anataka kazi yake ikamilike ndani ya siku mbili. Niliambiwa nikifanikiwa kufanya kazi hiyo kwa siku mbili nitapewa zawadi ya sarafu mbili za shaba."

"Nilifanya kazi kwa bidii lakini sheria ya tisa ilikuwa ndefu sana. Algamishi alipokuja na kukuta kazi yake haijaisha alikasirika sana. Kama ningekuwa mtumwa wake hakika angenipiga. Lakini kwa kujua kuwa msimamizi wa mji asingemruhusu anipige, sikuogopa, nikamwambia "'Aligamishi wewe ni tajiri sana. Niambie jinsi ya kuwa tajiri nami nitafanya kazi yako usiku kucha, asubuhi itakuwa tayari.'

"Akatabasamu na kusema, 'we mjanja sana, basi na iwe hivyo'

"'Usiku kucha nilikesha nikiandika, japo mgongo uliuma na harufu ya utambi iliniumiza kichwa na hadi macho yakawa hayaoni vizuri. Alipofika asubuhi kazi yake ikawa tayari."

"Hapo nikamwambia, 'niambie ulichoniahidi'

"Kijana wangu umefanya sehemu yako kwa ukamili,' aliniambia kwa upole. 'Sasa ngoja nami nitimize sehemu yangu. Nitakwaambia ujuzi huo kwasababu nimezeeka na ulimi wa wazee hupenda kuongea Vijana wanapoomba ushauri kutoka kwa wazee, hupata hekima ya miaka mingi. Lakini mara nyingi vijana hufikiri kuwa hekima ya wazee imepitwa na wakati, hilo linafanya wakose kufaidika.

"Kumbuka hili jambo, jua lililowaka wakati wa baba yangu ndilo hilo hilo litakalokuwa linawaka mjukuu wangu wa mwisho atakapokufa.

"Mawazo ya ujana,' akaendelea kusema, 'ni kama mwanga mkali wa kimondo kinachopita angani kwa kasi. Lakini hekima za wazee ni kama nyota inayoangaza siku zote kiasi kwamba mabaharia huitegemea kuwaongoza.

"Nisikilize kwa makini nitayokueleza na uelewe, vinginevyo kazi yako ya usiku kucha itakuwa ni kazi bure.

"Hapo aliniangalia kwa makini kwa macho yake yaliyokuwa yamefunikwa na makunyanzi, kwa sauti ya chini lakini thabiti, akaniambia.

'''Niliipata njia ya kwenda kwenye utajiri nilipoamua kwamba sehemu ya kumi ya kipato changu ni yangu, na wewe unatakiwa ufanye namna hiyo."

"Hapo akaendelea kuniangalia kwa macho ambayo nilihisi kuchomwa lakini hakuendelea kuongea.

"Ni hilo tu?' nikamuuliza.
"Hilo liliweza kubadilisha mchunga kondoo kuwa mkopesha pesa,' akanijibu.

"Lakini mbona kila ninachopata ni changu mwenyewe?' nikahoji'

"Unajidanganya,' akasema, 'je humlipi mshona nguo? Humlipi mtengeneza makubazi? Haulipii vitu unavyokula? Unaweza kuishi Babiloni bila kutumia pesa? Una nini cha kuonyesha kutokana na kipato chako cha mwezi uliopita? Vipi mwaka uliopita? Unalipa watu wote, kasoro wewe mwenyewe. Usiye na akili! Unafanyia wengine kazi. Ni sawa tu na kuwa mtumwa na kufanya kazi kwa yule anayekupa chakula na mavazi.

"Iwapo ungetunza sehemu ya kumi ya pato lako, ungekuwa na kiasi gani kwa miaka kumi?'
"Hesabu bado zilikuwa zinachaji kichwani mwangu, 'itakuwa sawa na pato langu la mwaka mmoja', nikajibu

"Kwa kiasi fulani upo sahihi' akasema. 'Kila kipande cha dhahabu ulichojilipa ni mtumwa wa kukufanyia kazi. Kila senti unayopata ni mtoto anayetakiwa kukuzalishia. Ili kuwa tajiri, kile unachotunza kinatakiwa kikuzalishie, na watoto wake wakuzalishie pia. Hilo ndilo linaweza kukufanya ufikie matamanio yako ya kuwa na mali.'

"Unaweza dhani nakudanganya na umekesha bure, lakini ninachokupa kina thamani mara elfu ya kazi uliyofanya. Unatakiwa tu kuwa na akili ya kuelewa.'

'''Lazima ujilipe sehemu fulani ya pato lako. Haitakiwi kuwa chini ya sehemu ya kumi ya pato lako hata kama pato lako ni dogo kiasi gani. Lakini inaweza kuwa zaidi ya hapo kulingana na uwezo wako. Lazima ujilipe kwanza na panga matumizi yako vizuri, usinunue nguo na viatu kwa pesa nyingi hadi ukakosa pesa ya kutoa misaada na sadaka.

"Utajiri ni kama mti, unakua kutoka kwenye mbegu ndogo sana. Pesa kidogo unayoanza kutunza ndiyo mbegu ya mti wa utajiri wako. Unavyopanda mapema ndivyo na mti utakua mapema. Na kadri unavyotunza mti wako kwa kuumwagilia kwa kutunza pesa ndivyo utakavyokaa na kufurahia kivuli chake mapema,'

"Baada ya kusema hayo, alichukua mabamba yake na kuondoka."

"Nilifikiria kwa makini kile alichokuwa ameniambia na nikaona kinapatana na akili, nikaazimia kukifanyia kazi. Kila mara nilipolipwa, nilichukua sehemu ya kumi ya pato na kuitunza. Jambo la ajabu ni kwamba sikupata shida yoyote ya mahitaji yangu. Tofauti ilikuwa ndogo sana na baadaye nikazoea.

Akiba yangu ilipoanza kukua nikaanza kupata kishawishi cha kuitumia. Nilitamani kununua vitu vizuri vilivyoletwa na meli na ngamia kutoka kwa wafoenike lakini nikajizuia'

"Baada ya miezi 12 toka Algamish aondoke, akarudi tena. Akaniuliza 'kijana, ulifanikiwa kujilipa sehemu ya kumi ya pato lako kwa mwaka uliopita?'

"Ndiyo mkuu, niliweza," nilijibu kwa kujidai.

'''vema sana,' akajibu akiwa kafurahi, 'umefanyia nini?'

'''Nimempatia Azmur, mfyatua matofali. Aliniambia atafanya safari kwenda nchi za mbali na akifika Tiro ataninunulia vito adimu kutoka kwa wafoenike. Akirudi tutauza kwa bei kubwa na kugawana faida,'

'''Kila mpumbavu anatakiwa kujifunza,' alifoka Algamish, 'kwanini umemuamini mfyatua matofali kwa jambo linalohusu vito? Unaweza kwenda kwa muoka mikate kuuliza kuhusu mambo ya nyota? Hapana! Utaenda kwa mnajimu iwapo una akili. Akiba yako imeshapotea, umeng'oa mti wako wa utajiri. Lakini unaweza panda upya. Jaribu tena na wakati mwingine ukitaka habari za vito nenda kwa sonara. Ukitaka kujua kuhusu kondoo, nenda kwa mfuga kondoo.

Ushauri mara nyingi ni kitu ambacho hutolewa bure lakini kuwa makini na hakikisha unachukua ule unaofaa tu. Anayechukua ushauri kuhusu akiba yake kutoka kwa mtu ambaye hana uzoefu ataipoteza kwanza ndipo atajua kuwa haufanyi kazi'. Baada ya kusema hayo akaondoka.
Duuuh.......kitabu kina MADINI ya kutosha.....
 
Jaza wazo hili ndani yako na tunza kiasi unachoona kinafaa ila isiwe chini ya moja ya kumi ya pato lako. Ikiwa kuna ulazima, badili matumizi yako ili kufanikisha hili. Baada ya muda utaanza kuhisi hisia za utajiri. Akiba inayokua itakuletea furaha, furaha ya kumiliki kitu chako mwenyewe. Kadri hazina yako inavyokuwa ndivyo utakavyochochewa kuweka zaidi. Utapata furaha maishani na nguvu ya kutafuta zaidi itakuingia. Je, kadri unavyopata zaidi si na kiasi unachotunza kitaongezeka?

"Baada ya hapo jifunze jinsi ya kufanya akiba yako ikutumikie. Ifanye mtumwa wako. Wafanye watoto wake na watoto wa watoto wake wakutumikie.

"Hakikisha una kipato kwaajili ya siku zijazo. Waangalie wazee na kumbuka kuwa siku zijazo nawe utakuwa mzee. Hivyo wekeza kwa tahadhari ili hazina yako isipotee. Biashara zenye kudai zina faida kubwa ni mtego na udanganyifu. Ni nyimbo zinazoimbwa ili kumvuta mtu asiye makini kwenye hasara na majuto.

Hakikisha familia yako haitateseka iwapo Miungu wakikuita. Unaweza fanya hivyo kirahisi kwa kutunza pesa kidogokidogo mara kwa mara. Mtu mwenye fikra za mbele hasubiri kupata kiasi kikubwa ndiyo akitunze au akiwekeze kwa wakati ujao.

"Jadiliana na watu wenye hekima. Tafuta ushauri kutoka kwa wale wanaofanya kazi zihusuzo pesa kila siku. Hao watakusaidia kuepuka makosa kama niliyofanya mimi kwa kumpa pesa zangu Azmur, mfyatua matofali. Faida ndogo penye usalama ni bora kuliko faida kubwa lakini penye hatari ya kupoteza mali zako.

"Furahia maisha ungali bado upo duniani. Usijibane kupita kiasi ili kutunza pesa, na usijaribu kutunza kiasi kikubwa kuliko uwezo wako. Kama sehemu ya kumi ndiyo unayoweza kutunza bila kupata taabu basi ridhika na kutunza kiwango hicho tu. Ishi kulingana na kipato chako ila usiwe bahili na kuogopa kufanya matumizi. Maisha ni matamu na yana vitu vingi vya kufurahia."

Rafiki zake wakamshukuru na kwenda zao. Wengine walikuwa kimya kwa sababu haikuwaingia akilini na hawakuweza kuelewa. Wengine walidhihaki kwa kusema "mtu tajiri hivyo alitakiwa kugawana utajiri wake na rafiki zake wasio na kitu." Lakini wengine walikuwa wamepata mwanga mpya. Walielewa kuwa, Algamish alirudi kwa Arkad mara nyingi sababu alikuwa anataka kumuona mtu akitoka gizani hadi kwenye mwanga. Mtu huyo alipopata mwanga fursa zilimsubiria, hakuna anayeweza kutumia fursa hizo mpaka afanye bidii kupata uelewa kwanza.

Hawa ndiyo ambao baadaye walikuwa wakimtembelea Arkad kila mwaka. Aliwashauri na kuwapa maarifa yake bure kama ambavyo watu wenye maarifa na busara nyingi hufanya. Pia aliwasaidia kuwekeza akiba zao ili wapate faida nzuri bila ya kuingia katika hatari ya kupoteza pesa zao wala kuingia kwenye uwekezaji usioleta faida. Maisha ya watu hawa yalibadilika siku ile walipogundua ukweli uliotoka kwa Algamish kwenda kwa Arkad. Kutoka kwa Arkad hadi kwao.

Sehemu fulani ya pato unalopata ni yako.

Mwisho wa sura ya pili.
Lkn sijachelewa Sana[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Boss ubarikiwe sana,hivi kufuata hizi kanuni sisi ambao tunakaribia kufika 40 tutaweza kutomboa kweli ? Make naona hii ni kwavijana wenye miaka kuanzia 25 wakiweka kidogo kidogo watatoboa.
 
Watu kama nyinyi Red Giant mnabarikiwa sana. Hiki kitabu nilikipakua huku mwaka jana nikapitia tu list of content nikaacha leo nimekisoma kupitia kwako.

Nasema mnabarikiwa kwasababu kama mimi nashindwa tu kujisomea, je kweli ningeweza kusoma na kutafsiri niandike kwa ajili ya watu?

Shukrani. Big up
Nitumie PM hicho kitabu ulichopakua.
 
Miaka 40 bado sana
Boss ubarikiwe sana,hivi kufuata hizi kanuni sisi ambao tunakaribia kufika 40 tutaweza kutomboa kweli ? Make naona hii ni kwavijana wenye miaka kuanzia 25 wakiweka kidogo kidogo watatoboa.
 
Natoa shukrani zangu Kwa mleta post,napenda kukwambia kazi yako na Muda wako haujaenda bure,umetuongezea maarifa ndugu zako ambayo yatatufanya tuwe wapya Kwa mitazamo chanya kabisa,barikiwa Sana mkuu
 
Boss ubarikiwe sana,hivi kufuata hizi kanuni sisi ambao tunakaribia kufika 40 tutaweza kutomboa kweli ? Make naona hii ni kwavijana wenye miaka kuanzia 25 wakiweka kidogo kidogo watatoboa.
Unatoboa bado mapema sana ndugu
 
Sijasoma vitabu vingi ila THINK AND GROW RICH ni miongoni mwa vitabu bora ningemshauri kila aliyekata tamaa ya maisha na huna mwangaza basi ukisoma hicho kitabu you will be fine na kama unapitia magumu kwenye mahusiano basi MEN ARE FROM MARS AND WOMEN ARE FROM VENUS japo ni nje ya mada ila hivyo ni miongoni mwa vitabu bora I recommend everyone to read one of them or all.
 
Back
Top Bottom