Umewahi kuswekwa lockup(selo), Unakumbuka nini?

Umewahi kuswekwa lockup(selo), Unakumbuka nini?

Candyscorpion
Daby
espy


mnaonaje mtafutane pm...maana mnajaza uzi kwa maongezi binafsi
 
Niliingia siku fulani hivi.

Askari waliokuja kunikamata niliwaona ni wadogo kiumbo na kiumri (nilikua na mwili wa mazoezi) wakawa wanaondoka na mimi mmoja akaniuliza "Sasa unaenda selo wakati unakaribia mitihani hauoni unajiharibia?" Mimi kimya.
Akili yangu inaniambia hapa nimeonewa, nina hasira vibaya vibaya hata kuongea sitaki. Nikaingizwa kwenye gari mpaka kituoni.

Nikafatishwa taratibu zote, naona lango linafunguliwa (halafu kufika kosa likaandikwa nimevunja na kuiba hasira zikazidi kunishika), namuuliza jamaa "Mbona hamnihoji?" Akacheka akasema "Hebu ingia huko"

Muda wote nilikua sihofii kuingia kwa kuamini kwanza sina kesi lakini pia nina mwili wa mazoezi (na sura mbaya nikazidi kuikunja) hakuna atakayenisumbua, nikaingia mule selo. Nilikuta washkaji kama wawili wana miili imekomaaa (Harmo rapa haoni ndani) halafu kuna washkaj kama kikundi wanaonekana wanajiamini balaa.
Kuna dogo katoka kupigwa virungu vya ugoko kapasuka hivyo katika kila kijichumba tukajibana ili anyooshe miguu. Surprisingly jamaa walikua peace vibaya mno nikajikuta nalegeza sura wakauliza ishu yangu ilianzaje nikawaelezea wakasema mbona hauna kesi hayo ni madai ukitoka kama vipi katembeze kipigo kwa huyo jamaa.

Joto, mbu, harufu ya mikojo, njaa na kujihis umepuuzwa na walio nje n.k.

Hata hivyo sikumaliza siku mbili nikatoka.
 
Back
Top Bottom