Umewahi kutapeliwa/umekutana na changamoto gani ya utapeli na ukatapeliwa kirahisi?

Umewahi kutapeliwa/umekutana na changamoto gani ya utapeli na ukatapeliwa kirahisi?

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2014
Posts
530
Reaction score
1,446

Biashara ya Mtandaoni: Ushuhuda, Mafanikio, na Changamoto za Matapeli

Mimi ni mdau mkubwa wa biashara za mtandaoni, na jambo linalonivutia zaidi ni pale tunapoweza kuzungumza na kufanya biashara kwa njia rahisi. Watu wengi wamefaidika na biashara hii, wengine wakitengeneza mtandao mkubwa wa wateja hadi kufikia mauzo makubwa kuliko hata wale wanaotegemea wateja wa ofisini.

Leo nataka kushiriki ushuhuda wa mtu ninayemfahamu ambaye amepata mafanikio makubwa kupitia biashara ya mtandaoni.

Safari ya Mafanikio ya Biashara ya Mtandaoni
Screenshot_20250214_174705_Instagram.jpg

Mtu huyu alianza kutumia mitandao ya kijamii kufanya biashara, na hadi sasa bado anaitumia ipasavyo kupata wateja. Wateja wake wengi, na karibu wote, amewapata kupitia mtandao.

Kwa sasa anaagiza bidhaa kutoka China, na hivi karibuni alisafiri Dubai kwa ajili ya kutafuta fursa zaidi za biashara. Ingawa alisema alikuwa anaenda kusherehekea siku yake ya kuzaliwa, ukweli wa mambo ni kwamba alikuwa akitafuta ‘machimbo’ mapya ya biashara.
Screenshot_20250214_174709_Instagram.jpg

Watu wengi wanadhani alianza na mtaji mkubwa, lakini ukweli ni kwamba alijenga biashara yake kwa kuanza na mtaji mdogo mtandaoni, akajenga uaminifu na kuhakikisha kuwa kila pesa anayopokea kutoka kwa wateja wake inatumika kwa uaminifu.
Screenshot_20250214_174946_Instagram.jpg

Mpaka alipofikia sasa ni juhudi zake za biashara ya mtandaoni zilizomfikisha hapo. Ni mtu ninayemjua vyema; tumepambana pamoja kwenye safari ya maisha.

Changamoto ya Matapeli wa Mtandaoni

Biashara mtandaoni inakumbwa na changamoto nyingi, mojawapo ikiwa ni tabia ya baadhi ya wafanyabiashara kutapeli wateja wao. Unakuta mtu ameona tangazo la bidhaa, amevutiwa, amewasiliana na muuzaji, lakini baada ya kutuma pesa, muuzaji anapotea kabisa.

Hii ni tabia ambayo hata wafanyabiashara wakubwa wanayo, na matokeo yake ni kupoteza wateja. Mfano, mteja wa Sumbawanga anaweza kuagiza bidhaa, akipigwa, hatosema kwa watu wengine kwa aibu, lakini ndani yake atajenga hofu ya kufanya biashara ya mtandaoni tena.

Mimi binafsi ninajitahidi kuwa mfano wa uaminifu katika biashara mtandaoni.

Uaminifu Katika Biashara: Ushuhuda Wangu

Nimewahi kupewa pesa na dada mmoja tuliyekuwa tunafanya naye kazi. Alikuwa amenunua kiwanja lakini hakuwa na muda wa kwenda site kutokana na majukumu yake. Aliniamini, akanitumia pesa, nami nikasimamia kazi ya ujenzi.
20230903_173446.jpg

Kazi ilianza mara moja, na hatua kwa hatua, tulifika kwenye hatua ya upauaji. Akanitumia pesa tena, nikafanya manunuzi kutoka kiwandani Dar es Salaam. Kila hatua nilikuwa narekodi matumizi kwa kumbukumbu.
20230919_162416.jpg

Baada ya kazi kukamilika, nilimkabidhi kazi na gharama zilizotumika zote.
Screenshot_20230915-141820_Drive.jpg


Ni muhimu kuelewa kuwa hiyo siyo gharama za ujenzi wote, bali ni sehemu tu ya matumizi niliyoyasimamia. Hata hivyo, dada huyu hakuweza kufika site hata mara moja, pamoja na nyumba ilipofika hatua hiyo, ameiuza bila hata kwenda kuiona kwa macho yake.

Kama angekutana na mtu asiye mwaminifu, leo hii angekuwa analilia moyoni kwa sababu fedha zake zingepotea.

Nimewahi Kupigwa Lakini Sikuacha Kuendelea

Pamoja na uaminifu wangu, nimewahi pia kupigwa na matapeli. Mwaka 2023, nilifanya biashara na jamaa mmoja aliyekuwa akiuza bidhaa mtandaoni.
Screenshot_20250214_182536_Facebook.jpg
Pamoja na uaminifu wangu, nimewahi pia kupigwa na matapeli. Mwaka 2023, nilifanya biashara na jamaa mmoja aliyekuwa akiuza bidhaa mtandaoni.
Niliona tangazo lake na nikachukua hatua ya kumcheki. Baada ya mazungumzo, nilimtumia pesa.
20230912_115615.jpg

Kwa bahati nzuri, mzigo akanitumia kama tulivyokubaliana.
20230920_081543.jpg

Sababu ya kuagiza hili betri la solar nilikuwa na N75 baada ya kulitumia miaka 3 likawa limechoka nikakutana na huyo jamaa ndio akaniulzia hili la N150 kampuni ya Pro Solar. Kwa sasa umeme ni 24 mvua inyeshe isinyeshe mimi ni burudani
Screenshot_20250214_185433_Photos.jpg

Kunatukio nimewahi kupigwa mpaka nikaliweka hapa, hawa watu wanarudisha nyuma sana wengine. Yaani watu wapo town kuiba na kutapeli na maisha yanaenda vizuri tu.

Hitimisho: Tafuteni Pesa ya Halali

Kuna watu wengi wanaoendesha maisha yao kwa utapeli na ujanja, lakini ukweli ni kwamba pesa isiyo ya halali haiwezi kukuletea maendeleo ya kweli. Wapo matapeli wengi mjini wanaoishi kwa udanganyifu, lakini mwisho wa siku maisha yao hayabadiliki.

Ukiwa mwaminifu katika biashara yako, utafanikiwa na wateja wako watarudi mara kwa mara. Lakini ukianza utapeli, utajijengea sifa mbaya na mwisho wa siku hutaweza kupiga hatua yoyote ya maana.

Jamani, tafuteni pesa ya halali. Hapo ndipo utakapopata maendeleo ya kweli!
 
Huyu dada pichani kama namfahamu!! Hajawai fanya kazi halmashauri moja hivi mbeya?
 
Back
Top Bottom