Samwely Angelo kisinga
New Member
- Oct 30, 2023
- 2
- 0
Umewahi kuua mtu?
Juzi mwanangu Tracey aliniuliza Hilo swali,nilishtuka na kuogopa Sana. Sikutegemea kabisa Kama mwanangu anaweza kuniuliza swali la namna Hiyo. Kwa dakika kadhaa nilimtazama pasipokusema kitu.
" Hapana sijawahi." Nilijikuta nimeropoka kwa haraka na gafla baada ya kukaa kimya kwa dakika kadhaa.Na nilijibu haraka hivyo ili kuondoa utata kwenye ubongo wake. Maana bila Shaka ukimya wangu ungeweza kumfanya afikirie tofauti.
" Lakini Baba ulitufundisha tusiseme uongo." Aliniambia.
Kauli hii ilinitisha zaidi, Kimoyo moyo nilijiuliza anamaana gani. Inamaana anaamini nimewahi kuua mtu? Na Nani huyo niliyemuua? Nilijiuliza pasipokuwa na majibu.
Ili kutoutesa ubongo wangu ,niliamua kuvunja ukimya . Nilimsogelea na kumshika mkono.
" Inamaana unaamini baba yako ni muuaji? Kabisa unafikiria Mimi baba yako nimewahi kuua mtu? Hapana trace,Mimi sipo hivyo, sijawahi kuua mtu? Na kwanini nifanye hivyo?" Nilimuuliza.
" Umeua baba? Tena sio mtu mmoja,umeua watu wengi.." Aliniambia.
Looh! Nilizidi kuchoka,Macho yalinitoka mithili ya panya kabanwa na mlango. Nilitamani kuongea lakini sikuwa na uwezo wa kufanya hivyo. Nilihisi kuweuka.
"Kwanini unanishtumu hivyo mwanangu?" Kinyonge Sana nilimuuliza.
" Kitu gani kinaua watu wengi Sana? Aliniuliza swali badala ya kujibu swali langu.
" Ni uharibifu wa mazingira mwanangu. Matatizo yanayotokana na uharibifu wa mazingira yanaua watu wengi Sana. Katika kila vifo vitano,vitatu vinatokana na uharibifu wa mazingira." Nilimwambia.
" Nani anaharibu mazingira?" Aliniuliza.
" Ni sisi wanadamu."
" Wewe umewahi kuharibu mazingira?"
" Ndio mwanangu."
" Kama hivyo basi umewahi kuua ,maana uharibifu wa mazingira ndio chanzo Cha vifo vingi. Ikiwa umewahi kuchoma vitu vilivyochafua hewa na ukasikia mtu amekufa kwa matatizo ya kuvuta hewa chafu basi jua wewe umewaua. Na ukisikia watu wamekufa kwa mafuriko,na wewe uliwahi kukata miti hovyo au kufanya Jambo baya lilipelekea ongezeko la joto na baadae mafuriko yakatokea basi jua wewe ni chanzo."
" Mmmh"
" Usigune baba, waharibifu wa mazingira wote ni wauaji. Na ikiwa wewe umewahi kuharibu mazingira basi jua nawe ni muuaji." Aliniambia.
Nilichoka,kwa maelezo yake nilijikuta nakubali, ni kweli nimewahi kuua mtu! vipi kuhusu wewe kwa ufafanuzi huu wa mwanangu Trace hujawahi kuua mtu kweli?
Samwely kisinga
Msendembali ,songea
0744408606.
Tena industry.