Umewahi kuuziwa maji ya Bomba dukani?

Umewahi kuuziwa maji ya Bomba dukani?

Basi Nenda

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2017
Posts
20,774
Reaction score
47,866
Hii tabia kuna mtu ameshakutana nayo? Unaenda dukani kununua maji makubwa unapewa ila ukifika nyumbani wakati wa kufungua unagundua hakuna seal

1. Nikiwa Mgahawa fulani nje ya mji niliagiza maji makubwa ya baridi,nikaletewa ila yana ladha ya ajabu japo yalikuwa na seal (

2. Nilinunua duka la mtaani kwangu maji makubwa (mimi ni mteja wa kila siku) nikayaweka chumbani alafu nikafunga mlango na kuondoka (naishi mwenyewe) nimerudi usiku huu nimegundua yale maji hayana seal, nimejiuliza muuzaji kafanya makusudi au bahati mbaya tu amenipa maji yake yeye ya bombani lakini nimegundua ni makusudi kwa sababu hata ujazo ulikuwa kama ya dukani mapya
 
Nimewahi sio mara moja.
Kwenye maduka yanayofanya hivyo wengi huuza maji ya bomba ujazo wa 1 L to 1.6 L kwa tsh 200/= na wanayapack kwenye machupa ya kampuni zinazouza sana.

Tatizo ni kuuziwa ukidhani ni maji halisi ya kampuni fulani kwa bei ile ile ila ukishtuka wanasema bei ya hayo ni mia 2, hii kisheria ipoje maana ni kuharibiana biashara na pia kiafya si salama.
 
Kiafya sio nzuri asubuhi nimepata matatizo ya tumbo. Bora hata wangekuwa wanachemsha
 
Kuna kaujanja ka kufunika kile kizibo ili kionekane kama kipo sealed. Tunakunywa uchafu pasipo kujua, ndio maana ya jina "bongo" tumia bongo ili uishi. Hata mavi uza.
 
Back
Top Bottom