Sitasahau nilikuwa naweka za 1k,2k,5k na 10k kwenye kibubu akaja dogo toka school likizo kukaa kwangu akakiona akawa ananichora tu.
Siku wamefungua dogo akaenda sokoni akakinunua kibubu kinafanana kinoma akabeba chenye hela akaniacha kitupu,
Sikugundua mapema Kama kimebadilishwa nikaendelea kutupia noti huku nakadiria kuwa kitakuwa na 500k.
Siku moja nikakishika nikasema mbona kibubu hakiwi kizito na ni miezi mitano.
Nikakivunja we nilikuta kuna 52k.
Ilibidi nicheke kwanza nikajua chuma ulete kuja kukiangalia vizuri kumbe kilibadilishwa daah we dogo sitakusahau aisee.