Umewahi kuweka akiba kwenye kibubu

Umewahi kuweka akiba kwenye kibubu

Sitasahau nilikuwa naweka za 1k,2k,5k na 10k kwenye kibubu akaja dogo toka school likizo kukaa kwangu akakiona akawa ananichora tu.​

Siku wamefungua dogo akaenda sokoni akakinunua kibubu kinafanana kinoma akabeba chenye hela akaniacha kitupu,​

Sikugundua mapema Kama kimebadilishwa nikaendelea kutupia noti huku nakadiria kuwa kitakuwa na 500k.​

Siku moja nikakishika nikasema mbona kibubu hakiwi kizito na ni miezi mitano.​

Nikakivunja we nilikuta kuna 52k.​

Ilibidi nicheke kwanza nikajua chuma ulete kuja kukiangalia vizuri kumbe kilibadilishwa daah we dogo sitakusahau aisee.​
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] alijua kukukomesha lol
 
Back
Top Bottom