Umewahi kuzielewa picha za CEO wa Simba, Barbra?

Umewahi kuzielewa picha za CEO wa Simba, Barbra?

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
UMEWAHI KUZIELEWA PICHA ZA CEO WA SIMBA, BARBRA?

Tuliwahi kuziona picha akiwa Al Ahly nchini Misri, Jijini Cairo akiwa na Mwenyekiti wa Al Ahly ilikuwa ni ziara ya kujifunza, baadae tukaziona picha akiwa na Rais wa Mamelodi Sundowns pale Pretoria.

Rais yule wa Mamelodi Sundowns kwasasa ndie Rais wa Shirikisho la soka Afrika, sitii neno bali naweka nukta! Al Ahly wale ndio washindi wa tatu klabu Bingwa duniani, sitii neno naweka nukta.

Tukaziona picha za baadae akiwa na Rais wa Shirikisho la soka duniani, Gianni Infantino hapa sitii neno naweka nukta tena, kisha tukaziona picha akiwa na Samuel Etoo ambaye ni Nyota wa zamani na anatajwa kula shavu kubwa CAF, sitii neno naweka nukta.

Kwa taswira ya Kiswahili zaidi, tunaweza kutafsiri huenda ni majivuno, huenda ni kutaka kujionesha (show offs) au mwingine atasema ni uvimbaji tu, na watu wakikasirika kabisa watasema hakuna maana yoyote juu ya yeye kupiga picha hizo.

UNASEMAJE JUU YA PICHA HIZO? Binafsi nataka niwaambie kuna kitu kinaitwa INTERNALISATION OF THE CLUB! Hapa tunahitaji elimu kidogo ya Darasani, huyu CEO pale hapigi picha kama yeye bali ana image ameibeba nayo inaitwa SIMBA, yeye akiwa Mtendaji.

Nini maana ya Internalisation kwa hoja ya kusupport anachofanya CEO wa SIMBA? Maana yake ni kuwa anaitoa klabu kwenye level zetu za ndani na Afrika Mashariki na kuipeleka duniani, unadhani hivi sasa Motsepe haifahamu Simba?, Infantino haifahamu Simba au Etoo? Anaisukuma image kwa njia ya kidiplomasia.

Ina faida gani kwa Simba na kwake? Kwa Simba inatengeneza sura nzuri ya Taasisi kama brand, itafika muda hata mikataba itazungumzwa kwa ukubwa wa Simba na Maofisa wake, itafika muda hata macho ya Maskauti na Mawakala yataimulika Simba.

Ipi faida kwa CEO? ujanja ujanja wake ni kujiwekea nafasi kwa watu wa mpira, ujanja huu aliutumia Andrea Agnelli na sasa ni Mwenyekiti wa vilabu Ulaya, ujanja huu anautumia Steve Zhang wa Inter Milan ni Makamu na hata Perez hizi ndio karata zake, hata Barbra sasa hivi kwa Afrika anakuwa kwenye spotlight ni faida kwake na Simba.

Mbona anatumia sana Mtandao? Jibu rahisi ni CIVIL JOURNALISM, Tutajadili siku nyingine

moodykabwe
View attachment 1726447View attachment 1726453View attachment 1726454
 
Huu uzi bila picha ni kama pombe bila hamila!!
 
Zile ni photo-op, nyingi zinapigwa baada ya kupiga ma deal.

Uongozi ni muhimu si tu ufanyike, bali pia uonekane kufanyika.

Sio kiongozi anakuwa haonekani wiki tatu nchi inakuwa katika mtafaruku.
Ana mafua.
 
Mkuu umemaliza,asie elewa basi atoelewa jambo llolote lile Duniani.
 
Club inajengwa kwa matokeo ya uwanjani. Ndivyo itafahamika kwa wachezaji na wadhamini.
Hilo la kupiga picha ni yeye kama yeye anajiweka karibu.
Endeleeni kujidanganya Motsepe akiijua simba ndio ataleta wazamini.
 
Kaka umetumia nguvu nyingi sanaaa kuelimisha kitu simple nafahamu una lengo la kuwaelimisha mambumbumbu

Ila kiukweli itoshe kusema CV inatengenezwa kwa vitu vingi ikiwemo education background + experience+conference /seminar /training attendance sasa so far iwekw ivi embu compare Barbra Vs Haji (acting secretary wa yanga) kwa vigezo kama ivyo vya Cv then ww ndio una ajiri let say Secretary waa klabu yako ...ww uta opt kumchagua yupi kqti ya hao ?
 
Yule Haji akienda sehemu za kimataifa naona hata Kiingereza tu kitamtoa jasho.
 
English sio issue mkuu
Kwanza tazama tu izo scenario
Binafsi mm nita opt kwa yule dada frankly
Ukishawahi kutupwa kikao cha kimataifa wenzako wanakata jokes na kucheka kwa Kiingereza halafu wewe hujui Kiingereza ndiyo utajua English ni issue au si issue.
 
Ukishawahi kutupwa kikao cha kimataifa wenzako wanakata jokes na kucheka kwa Kiingereza halafu wewe hujui Kiingereza ndiyo utajua English ni issue au si issue.
Ktk vikao vyenye status ya kimataifa basi lzm viwepo vifaa saidizi vya lugha. Mfano pale Caf kuna mijitu ina mwaga french tupu kwa iyo lzm kuwepo vifaa saidizi vya lugha
 
Ktk vikao vyenye status ya kimataifa basi lzm viwepo vifaa saidizi vya lugha. Mfano pale Caf kuna mijitu ina mwaga french tupu kwa iyo lzm kuwepo vifaa saidizi vya lugha
Kwanza kabisa, ukishaanza kusaidiwa lugha, kwa mfano na mkalimani, huwezi kwenda kasi sawa maongezi na watu ambao wanaipiga lugha bila kusaidiwa.

Kuna kipindi Fidel Castro alikuwa anaweka ngumu kuongea Kiingereza, alikuwa anataka kuongea Kihispania tu katika mahojiano na mtangazaji wa Marekani. Halafu kati kuna mkalimani anatafsiri Kiingereza na Kihispania kati yao.

Mtangazaji akampatia Castro. Alijua Castro anajua Kiingereza ila anakataa tu kuongea Kiingereza. Basi badala ya Mtangazaji kuongea siasa, akaanza kuongea habari za mchezo wa baseball, akijua Castro anapenda sana baseball.

Castro akaingia mtegoni, alivyosikia mtangazaji anaongea baseball, Castro akasahau mpango wake wa kuongea Kihispania na kutafsiriwa na mkalimani, akaongea Kiingereza moja kwa moja na mtangazaji. Ikawa mtangazaji kavunja barrier ya mkalimani.

Mtangazaji huyu mjanja alielewa kwamba mkalimani tayari ni barrier!

Pili, kusaidiwa lugha kunaweza kuwa na maana kwenye formal communication, ambapo pengine kuna mpaka wakalimani. Kwenye informal chitchat, ambapo personal connections kubwa sana zinakuwa developed, kuwa na mkalimani kati ni awkward.

Tatu, usilinganishe mtu ambaye hajui Kiingereza anajua Kifaransa na mtu ambaye hajui Kiingereza wala Kifaransa, anayejua Kifaransa anaweza kuongea na watu wa nchi nyingi sana za Afrika bila kujua Kiingereza. Asiyejua Kiingereza wala Kifaransa hata Waganda tu wa East Africa atapata tabu kuongea nao.

Bottom line.

Mtanzania anayetaka kujichanganya kimataifa kujua Kiingereza ni jambo muhimu sana.
 
Kwanza kabisa, ukishaanza kusaidiwa lugha, kwa mfano na mkalimani, huwezi kwenda kasi sawa maongezi na watu ambao wanaipiga lugha bila kusaidiwa.

Kuna kipindi Fidel Castro alikuwa anaweka ngumu kuongea Kiingereza, alikuwa anataka kuongea Kihispania tu katika mahojiano na mtangazaji wa Marekani. Halafu kati kuna mkalimqni anatafsiri Kiingereza na Kihispania kati yao.

Mtangazaji akampatia Castro. Alijua Castro anajua Kiingereza ila anakataa tu kuongea Kiingereza. Basi badala ya Mtangazaji kuongea siasa, akaanza kuongea habari za mchezo wa baseball, akijua Castro anapenda sana baseball.

Castro akaingia mtegoni, alivyosikia mtangazaji anaongea baseball, Castro akasahau mpango wake wa kuongea Kihispania na kutafsiriwa na mkalimani, akaongea Kiingereza moja kwa moja na mtangazaji. Ikawa mtangazaji kavunja barrier ya mkalimani.

Mtangazaji huyu mjanja alielewa kwamba mkalimani tayari ni barrier!

Pili, kusaidiwa lugha kunaweza kuwa na maana kwenye formal communication, ambapo pengine kuna mpaka wakalimani. Kwenye informal chitchat, ambapo personal connections kubwa sana zinakuwa developed, kuwa na mkalimani kati ni awkward.

Tatu, usilinganishe mtu ambaye hajui Kiingereza anajua Kifaransa na mtu ambaye hajui Kiingereza wala Kifaransa, anayejua Kifaransa anaweza kuongea na watu wa nchi nyingi sana za Afrika bila kujua Kiingereza. Asiyejua Kiingereza wala Kifaransa hata Waganda tu wa East Africa atapata tabu kuongea nao.

Bottom line.

Mtanzania anayetaka kujichanganya kimataifa kujua Kiingereza ni jambo muhimu sana.
Sawa kwa hiyo baba jesca atuhimize pia matumizi ya english
 
Back
Top Bottom