Albinoomweusi
JF-Expert Member
- Oct 28, 2016
- 3,433
- 8,585
UMEWAHI KUZIELEWA PICHA ZA CEO WA SIMBA, BARBRA?
Tuliwahi kuziona picha akiwa Al Ahly nchini Misri, Jijini Cairo akiwa na Mwenyekiti wa Al Ahly ilikuwa ni ziara ya kujifunza, baadae tukaziona picha akiwa na Rais wa Mamelodi Sundowns pale Pretoria.
Rais yule wa Mamelodi Sundowns kwasasa ndie Rais wa Shirikisho la soka Afrika, sitii neno bali naweka nukta! Al Ahly wale ndio washindi wa tatu klabu Bingwa duniani, sitii neno naweka nukta.
Tukaziona picha za baadae akiwa na Rais wa Shirikisho la soka duniani, Gianni Infantino hapa sitii neno naweka nukta tena, kisha tukaziona picha akiwa na Samuel Etoo ambaye ni Nyota wa zamani na anatajwa kula shavu kubwa CAF, sitii neno naweka nukta.
Kwa taswira ya Kiswahili zaidi, tunaweza kutafsiri huenda ni majivuno, huenda ni kutaka kujionesha (show offs) au mwingine atasema ni uvimbaji tu, na watu wakikasirika kabisa watasema hakuna maana yoyote juu ya yeye kupiga picha hizo.
UNASEMAJE JUU YA PICHA HIZO? Binafsi nataka niwaambie kuna kitu kinaitwa INTERNALISATION OF THE CLUB! Hapa tunahitaji elimu kidogo ya Darasani, huyu CEO pale hapigi picha kama yeye bali ana image ameibeba nayo inaitwa SIMBA, yeye akiwa Mtendaji.
Nini maana ya Internalisation kwa hoja ya kusupport anachofanya CEO wa SIMBA? Maana yake ni kuwa anaitoa klabu kwenye level zetu za ndani na Afrika Mashariki na kuipeleka duniani, unadhani hivi sasa Motsepe haifahamu Simba?, Infantino haifahamu Simba au Etoo? Anaisukuma image kwa njia ya kidiplomasia.
Ina faida gani kwa Simba na kwake? Kwa Simba inatengeneza sura nzuri ya Taasisi kama brand, itafika muda hata mikataba itazungumzwa kwa ukubwa wa Simba na Maofisa wake, itafika muda hata macho ya Maskauti na Mawakala yataimulika Simba.
Ipi faida kwa CEO? ujanja ujanja wake ni kujiwekea nafasi kwa watu wa mpira, ujanja huu aliutumia Andrea Agnelli na sasa ni Mwenyekiti wa vilabu Ulaya, ujanja huu anautumia Steve Zhang wa Inter Milan ni Makamu na hata Perez hizi ndio karata zake, hata Barbra sasa hivi kwa Afrika anakuwa kwenye spotlight ni faida kwake na Simba.
Mbona anatumia sana Mtandao? Jibu rahisi ni CIVIL JOURNALISM, Tutajadili siku nyingine
moodykabwe
View attachment 1726447View attachment 1726453View attachment 1726454