Sina hakika kama huyo amepitia maisha magumu kuliko wengine ila nakumbuka mimi baada ya kumaliza shule ya msingi sikuwa na mtu wa kuniendeleza kielemu miaka hiyo nikaingia mashimoni kugonga kokoto huku nalala kwenye machimbo nikiwa na umri wa miaka 14 natafuta hela ya ada kujisomesha ila baada ya kupata ada nikaona nifungue genge la nyanya nikaanza na mtaji wa elfu 20 ebu fikiria nikiwa kwenye umri huo natoka maeneo ya kipunguni b kule nakuja kupanda gari mombasa hapo lerini unakutana na maiti ya mtu kachomwa kisu huku mwanamke kabakwa mida ya saa tisa na katika hiyo biashala nilikuwa najinyima kula nakula mlo mmoja tu mpk nilipofanikiwa maisha ila yote kwa yote kila mtu ana siri yake na usije ukasema mtu ni mtakatifu machoni pako ila nyuma ya pazia kuna mengine