Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

umewahi fiwa na demu gheto ?
Kuna msela alifiwa na mke wa mtu chumbani kwake.

Mke alimuaga mume anakwenda kijijini lakini mke kaenda jirani tu kwa msela. Hawajakaa sawa malaria, hawajakaa sawa mama Kavuta.

Jamani Tanga Kuna watu Wana busara, ukiambiwa hiyo Soo Kuna mgosi alikwenda kumtuliza mume wa MTU mpaka maisha yanaendelea!!! Ingekuwa huko Bunda au Geita pangechimbika.
 
Huyo ni mwanakamati wa Mshana Jr ,hapo ulibaki mfano wa mwili tu
 
wewe ungefungwa kimasihara ohoo😂😂
 
Visa viwili vyote kwenye maji miaka fulani nikiwa naishi Tanga mzee alikuwa anafanya kazi huko, tulikuwa na mtindo wa kwenda kuogelea deep sea kipindi cha Ramadhani siku moja tuliogelea kama saa nane hivi dah!! Palikuwa na mdada anaenda maji marefu maana wanaume wanamfuata kumshika shika basi akawa anakimbia maji marefu tunashangaa kimya watu wakapiga mbizi kama Kanata chini kama dk 20 akapatikana kashakufa tayari alikuwa mnene...

Kingine kulikuwa na ziwa nyuma ya shule moja inaitwa mabawa mitaa ya komesho palisemekana Kuna chunusi, kama kawa wazee wa kupiga mbizi tulikuwa wadogo na vinguo vya shule watoto wanaosoma mabawa, majengo na Shaban Robert wako nyomi sisi tumekuja na nguo za home tukawa tunapiga mbizi.

Kuna dogo alikuwa yuko darasa la kwanza sijajua shule gani maana zipo tatu sehemu moja, alizama kiutani utani akashika kwenye tope akafariki tulimtafuta zaidi ya nusu saa yaani mpaka kiza kinaingia 12 ndio anaonekana kavimba tumbo kashakufa ila ile sehemu panahusishwa na imani za kishirikina wenyeji wanasema Kuna "chunusi" sijui ndo mdudu gani?

Vifo vingine nishaona sana kwenye misafara ya harusi wale wenye masifa ya pikipiki walikuja kugongana mmoja akafarirki hapo hapo.
 
Kama nakuona vile, swali la kwanza ulikua unajiuliza JELA WATU WANAISHI VIPI[emoji1783][emoji1783][emoji1783]
 
Kuna dogo alikuwa anavuka barabara....lilikuwa kundi la watoto chokoraa...wenzie wakasita kidogo Yeye akawa ashaingia barabarani tayari....alipigwa na gari IT alirushwa juu mkojo ukawa unamiminika anavyoshuka kutua chini...yaan alivyotua ni kama limetupwa furushi...dogo alishakufa kitambo maana alipasuka kichwa....nilikuwa kwenye bodaboda nishuka na kuanza kurudi Kwa mguu nimeshika viatu mkononi😭🙏
 
Mwezi wa tano mwaka huu mtoto wangu alikuwa kalazwa KCMC kwa shida ya moyo. Saa 7 usiku daktari akanipigia simu kuwa hali ya mtoto imebadilika ghafla. Niliwasha gari na kuelekea hospitali haraka na kufika tu dogo akanishika mkono akakata roho....

Natamani sana nisingepigiwa ile simu. Mzazi hapaswi kuzika mtoto bali mtoto ndio amzike mzazi
 
Pole sana, Mungu akupe faraja kuu na akufute machozi na maumivu yote.
 
Daaa😭😭🙏
 
Huduma ya kwanza kuokoa maisha inapaswa kuwa elimu muhimu itolewe kuanzia shule ya msingi kama wanavyofanya wenzetu ughaibuni
Kwa wenzetu mtu akifa ni hasara kubwa sana lkn kwetu ukiwa hai ni kama hasara kwa taifa, fikiria kazi ni za kugombania, maji, dawa, elimu, usafiri kila kitu ni ugonvi ili ukipate.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…