Asante sana. Nimeshapoa maisha yanaendeleaPole sana mkuu, imeniuma kama mimi ndio mzazi!!
Asante sana. Nimeshapoa sasa
Mwenzako ana uhakika wa kwenda mbinguni maana hamlaumu MunguThat is the weakest point of any living organism, especially human being the most weakest oneView attachment 2380253
Duh may he rest in peaceView attachment 2380690
Hi gari nliomba nafasi nkaambiwa imejaa
Ikaenda ya nyuma yake nkaomba ikawa imejaa pia
Inayofuata nkapanda!
Hivyo tulikua hatujapishana sana
Kufika nyang’oro nkakuta imepata ajali
Watu woote walitoka nje(wa hi buss) kasoro dereva tu!
Sababu alikandamizwa na dashboard ya buss
Kadri wanavyoendelea kufanya jitihada za kuvuta buss nyuma ndivyo jamaa alivyokua anaendelea kupoteza nguvu
Ila wakati nafika alikua yuko fit
Kiasi kua alikua anageuka na kuongea vizuri
Baadae nkaona kama hata nguvu imemuishia
Bahati nzuri ambulance ikawa imefika
Hivyo walimuanzishia hiduma ya kwanza pale pale ndani
Huku jitihada za kumtoa zinaendelea[emoji34]
Dah nlihisi maumivu anayoyapata yule dereva sikua na majibu
Baadae wakafanikisha kumtuoa jamaa nje
Dah ile miguu nahisi ilikua imekatika kabisa[emoji17][emoji17]
Wakampeleka hospital akiwa mzima
Baadae nmefika home napewa taarifa na mdogo wangu (mnazi wa magari) kua jamaa amekufa
Aaah it was si bad bad bad
Hadi sasahivi siwezi kusema kua ni kweli ila nadhan ni kweli
Yule jamaa anaitwa shomali
Afu nasikia kuna watu wakipelekwa mochwari wanafufuka wahudumu wanawamalizia huko huko yaani nyie!!!Ndio kaka
Nyingi ni story za vijiweni [emoji23]Afu nasikia kuna watu wakipelekwa mochwari wanafufuka wahudumu wanawamalizia huko huko yaani nyie!!!
Mchawi huyoUmenikumbusha jambo moja lililotokea nikiwa na demu geto, ndani ya sekunde 5 nishapagawa.
Mwezi wa 7 nilikuwa na demu geto, baada ya kunyanduana tukawa tumelala. Sasa USIKU wa manane nilivyoshtuka, kumwangalia demu katulia tiiiii. Kumgusa kwenye mbavu akawa kama hapumui hivi! Oyaa, nilidata, nikajua ashavuta.
Basi nikamtikisa kwa nguvu sana ndo akashtuka anauliza NINI????
Nilivuta pumzi ndefu halafu nikalala Hata sikumsemesha
Kutoa lift ovyo ovyo ni hatari kwa maisha yako.Kuna mama niliwahi kumpa lifti ilikua maeneo ya njia ya kahama geita ile njia ya vumbi watu wengi wanaifahamu.
Kutokana na mazingira niliyomkuta yalikua magum nilijua kwa muda ule hawez kupata msaada ilikua ni jion
Nilivyombeba niligundua ni mtu anae amini sana ushirikina alikua ananisimulia ni jinsi gan ndugu zake wamemloga na watoto wake huwa wanakufa kabla ya kufikisha miaka 10, hata yeye nilivyomuona alikua ni mgonjwa kakonda sana hivyo akasema hata yeye pia kalogwa na ndugu zake, baada ya safari kidogo aliacha kunisimulia akajifunika kanga yake usoni Basi mi nikajua kalala
Tulivyofika sehem natakiwa kumshusha namuamsha haamki, kila nikimuamsha haamki ghafla nikaona gari ya polisi nikawasimamisha wakaniambia tuongozane had hospita kufikisha hospital tu nikaambiwa kashakufa huyu, ikabd uchunguz uanze kama amelishwa sumu au nn bahat nzuri iligundulika kafa na maradhi ingekua vinginevyo ningewajibishwa hata ndugu zake wangeniiona ni Mimi ndo nimefanya
Watu wengi waliowahi kupata ajali huwa hawapendi siti za dirishani na zile siti za mbele upande wa kushoto wa dereva huwa hawazitaki kabisa hizo sitiNakumbuka tarehe 12 Jan 2011 siku ya Mapinduzi, Bus la Sumry kutoka Dar kwenda Iringa tulivyopata ajali kugongana uso kwa uso na Lori la mizigo mbele ya mikumi ukiwa unaanza kuitafuta Kitonga..11 au 13 people walipoteza maisha siku ile..Hii safari ni kama ilikuwa ina ishara ila kiubinadamu ni ngumu kujua what kingekuja mbele yetu..Maana Ubungo pale watu hadi dakika za mwisho Dereva anataka kuondoa gari wasindikizaji zaidi ya 10 wanaagana na wapendwa wao hadi Dereva akagomba kiwa imetosha sasa wasiosafiri washuke ili tuanze safari.
Ila ninachokikumbuka zaidi ni Mama aliyekaa pembeni yangu maana toka mwanzo wa Safari alikuwa kama hayupo sawa..Salamu alikuwa anaitikia kwa uzito..Soda na Pipi alikataa vyote hakuchukua...Nilitamani nihame kabisa siti maana nilikuwa naona kama ana kisirani hivii..Mara nyingi huwaga nalala sana kwenye gari so tulivyofika tuu Moro Mjini nikalala zangu nikaachana nae...Kufika kwenye eneo la tukio Dereva wa lori alisinzia inavyosemekana kwenye kona ya mlima akakatia kona upande wetu so dereva kuona hivyo akakwepesha na kumpa ubavu kuanzia siti ya 3 kutoka kwake..Hivyo basi Lile lori likaanza kupiga siti hizo hadi mwisho na gari zote zikapinduka finally..
Kwa kuwa nilikuwa usingizini kushtuka sikuelewa kilichotokea haswaa nikakuta tuu abiria wenzangu kama wamelala hivii ila baada ya muda akili ikanirudia kuwa wameshafariki baada ya kuona ubongo,utumbo na vitu vingine..Kumbe ndiyo walikuwa washafariki including Mama wa pembeni yangu..Good enough niliumia lakini si sana compared to wengine..Niliona watu wawili wakija kufia nje kutokana na kutokwa sana na damu na msaada kuchelewa..Pia I still remember kuna Mzee alikuwa anamlilia Mke wake walikuwa wanapiga story ila ghafla tuu akawa hayupo nae tena.
Very bad expirience ambayo hadi leo imenifanya niwe na phobia ya kukaa dirishani kwenye safari ndefu..hata unipe milioni sikai siti ya dirishani..
Ebola hiyoLeo nimeona mtu akifa kama utani na mbele yangu.
Wakati nikivuka barabara ghafla mtu mwanaume aliyekuwa mbele yangu akaanguka kama kapigwa shoti ya umeme.
Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili.
Sababu ya butwaa nilikosa cha kusaidia ila wakaja wadau hapo wakasema ni kifafa huyo, jamaa keshameza ulimi n.k yaani kuna mzee akamgusa akasema huyo tayari kafa.
Basi ikawa ndio hata hatujui nini kifanyike
Ila ndio ikawa tayari amekufa. Nikaahirisha na safari nikarudi zangu nyumbani.
Umewahi shuhudia mtu kufa ghafla?