Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

ebhana nakumbuka siku moja natoka zangu ferry naelekea home kujificha basi nikaamua nipitie njia ya mji mwema niendelee kubariz ka usiku naweza pata hata chura wa kwenda kula mbususu mdogo mdogo na ka Tvs kangu wakanipita watoto wa mbagala wamepakizana mshikaki watu 5 vijana wa saiz ya kati na pikipiki nyingine yupo dereva na mademu watatu jumla wanne ziko speed sana walinipita chadibwa wao kufika kona ya malaika pikipiki moja ikapasuka tairi ya mbele na aliekua kabeba madem akakosa uelekeo akawapanda wa mbele waliokua wameshaanguka hivyo ikawa ajali ya pikipiki mbili majeruhi 6 waliokufa 3 nilikua nyuma yao hivyo nikawa wakwanza kufika alooo inasikitisha walio majeruhi wote wamevunjika madem wawili wamekufa na men mmoja ile siku sitaisahau kwakua madogo walikua wanalia kwa maumivu wengne wananyanyuka kwa wenge wanaanguka nilichoweza ni kusimamisha magari na bajaji na kutoa taarifa kituoni ila tuchunge sana watoto wetu wadogo zetu mdugu jamaa na marafiki kuna michezo inafanyika usiku hasa wale wanaotoka beach kurudi makwako ebhana weee hizo pikipiki zinageuka ndege za ardhini
 
Pole sana mdogo wangu.Usichukie kukuita mdogo wangu maana ungekuwa na umri mkubwa ungekuwa umeshakutana na mengi sana.Mfano baba yako unamuuguza anakufa mbele yako wakati mmeongea naye dakika 20 kabla.
Kufiwa na mwanao.Kufiwa na ndugu zako wote ubaki peke yako.
Usijali ndio maisha.
 
Mimi naye sikai dirishani, huwa nakaa siti ya mwisho kati kati
Hii ilitokea mwaka 1984 Morogoro wakati ule gari zinasafiri usiku.Dereva alipita sehemu kumbe kuna kijiko au teseme grader la kuchimba barabara kimeegeshwa meno yamegukia barabarani basi abiri wote walikuwa upande wa kushoto walicharangwa kama wembe.
Situ nzuri za kukaa dirishani ni kwenye train na ndege tu gari hapana aise.
 
Mkuu, inawezekana unachokisema ni sahihi ila tatizo hizo first aid zipo nyingi saaaana na ni rahisi mtu kuzisahau baada ya muda fulani kupita. Vilevile unakuta mtu tangu afundishwe hajawahi kuzifanyia mazoezi pahala popote.
 
Daah hatari sanaa....
 
CPR hizi naonaga ni kushuhudia kifo tu mkuu.. Kuna mgonjwa alikuwa na vidonda vya tumbo mwana tu alitoka kweye surgery akaja ICU aisee hakuchuki hata dak 2 nkaona anaanz akugeuza macho katika vifo vyote kile sitakisahau kifo kinaumiza sana[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Aisee achaeni haya maishaa tupo hai kwa neema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…