Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

ebhana nakumbuka siku moja natoka zangu ferry naelekea home kujificha basi nikaamua nipitie njia ya mji mwema niendelee kubariz ka usiku naweza pata hata chura wa kwenda kula mbususu mdogo mdogo na ka Tvs kangu wakanipita watoto wa mbagala wamepakizana mshikaki watu 5 vijana wa saiz ya kati na pikipiki nyingine yupo dereva na mademu watatu jumla wanne ziko speed sana walinipita chadibwa wao kufika kona ya malaika pikipiki moja ikapasuka tairi ya mbele na aliekua kabeba madem akakosa uelekeo akawapanda wa mbele waliokua wameshaanguka hivyo ikawa ajali ya pikipiki mbili majeruhi 6 waliokufa 3 nilikua nyuma yao hivyo nikawa wakwanza kufika alooo inasikitisha walio majeruhi wote wamevunjika madem wawili wamekufa na men mmoja ile siku sitaisahau kwakua madogo walikua wanalia kwa maumivu wengne wananyanyuka kwa wenge wanaanguka nilichoweza ni kusimamisha magari na bajaji na kutoa taarifa kituoni ila tuchunge sana watoto wetu wadogo zetu mdugu jamaa na marafiki kuna michezo inafanyika usiku hasa wale wanaotoka beach kurudi makwako ebhana weee hizo pikipiki zinageuka ndege za ardhini
 
Leo nimeona mtu akifa kama utani na mbele yangu.

Wakati nikivuka barabara ghafla mtu mwanaume aliyekuwa mbele yangu akaanguka kama kapigwa shoti ya umeme.

Akajibamiza vibaya sana chini na pote pakaanza kutapakaa damu, inatoka kila eneo la wazi la mwili.

Sababu ya butwaa nilikosa cha kusaidia ila wakaja wadau hapo wakasema ni kifafa huyo, jamaa keshameza ulimi n.k yaani kuna mzee akamgusa akasema huyo tayari kafa.

Basi ikawa ndio hata hatujui nini kifanyike

Ila ndio ikawa tayari amekufa. Nikaahirisha na safari nikarudi zangu nyumbani.

Umewahi shuhudia mtu kufa ghafla?
Pole sana mdogo wangu.Usichukie kukuita mdogo wangu maana ungekuwa na umri mkubwa ungekuwa umeshakutana na mengi sana.Mfano baba yako unamuuguza anakufa mbele yako wakati mmeongea naye dakika 20 kabla.
Kufiwa na mwanao.Kufiwa na ndugu zako wote ubaki peke yako.
Usijali ndio maisha.
 
Mimi naye sikai dirishani, huwa nakaa siti ya mwisho kati kati
Hii ilitokea mwaka 1984 Morogoro wakati ule gari zinasafiri usiku.Dereva alipita sehemu kumbe kuna kijiko au teseme grader la kuchimba barabara kimeegeshwa meno yamegukia barabarani basi abiri wote walikuwa upande wa kushoto walicharangwa kama wembe.
Situ nzuri za kukaa dirishani ni kwenye train na ndege tu gari hapana aise.
 
Watu wengi wanakufa kwa sababu ya kukosa huduma ya kwanza.. Kuna uwezekano huyo jamaa angepata mtoa huduma wa kwanza angeishi

Watu wengi hawajui kufanya ABC's (Airways, breathing and circulation )na Cadio pulmonary resuscitation (CPR) pindi kunapotokea dharura za kiafya mitaani

Kwa wenzetu FIRST AID Ni kitu kinachofundwa mashuleni tangu chekechea
Mkuu, inawezekana unachokisema ni sahihi ila tatizo hizo first aid zipo nyingi saaaana na ni rahisi mtu kuzisahau baada ya muda fulani kupita. Vilevile unakuta mtu tangu afundishwe hajawahi kuzifanyia mazoezi pahala popote.
 
Kuna dogo alikuwa anavuka barabara....lilikuwa kundi la watoto chokoraa...wenzie wakasita kidogo Yeye akawa ashaingia barabarani tayari....alipigwa na gari IT alirushwa juu mkojo ukawa unamiminika anavyoshuka kutua chini...yaan alivyotua ni kama limetupwa furushi...dogo alishakufa kitambo maana alipasuka kichwa....nilikuwa kwenye bodaboda nishuka na kuanza kurudi Kwa mguu nimeshika viatu mkononi[emoji24][emoji120]
Daah hatari sanaa....
 
Wafanyakazi wa afya tupewenl ulinzi maalumu maana daily ndugu zenu tunakuwa nao katika nyakati zao za mwisho hapa duniani..

Sema kuna mambo tumeyazoea lakini kiuhalisia ni mazito kwa mtu wa kawaida, mfano kutoa taarifa ya kifo kwa ndugu tunaonaga ni kawaida lakini ni jambo zito sana kwa wanaopata hizo taarifa.
CPR hizi naonaga ni kushuhudia kifo tu mkuu.. Kuna mgonjwa alikuwa na vidonda vya tumbo mwana tu alitoka kweye surgery akaja ICU aisee hakuchuki hata dak 2 nkaona anaanz akugeuza macho katika vifo vyote kile sitakisahau kifo kinaumiza sana[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Hii ilitokea mwaka 1984 Morogoro wakati ule gari zinasafiri usiku.Dereva alipita sehemu kumbe kuna kijiko au teseme grader la kuchimba barabara kimeegeshwa meno yamegukia barabarani basi abiri wote walikuwa upande wa kushoto walicharangwa kama wembe.
Situ nzuri za kukaa dirishani ni kwenye train na ndege tu gari hapana aise.
Aisee achaeni haya maishaa tupo hai kwa neema.
 
Back
Top Bottom