Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

Umewahi shuhudia mtu akifa mbele yako ghafla na hukuamini?

CPR hizi naonaga ni kushuhudia kifo tu mkuu.. Kuna mgonjwa alikuwa na vidonda vya tumbo mwana tu alitoka kweye surgery akaja ICU aisee hakuchuki hata dak 2 nkaona anaanz akugeuza macho katika vifo vyote kile sitakisahau kifo kinaumiza sana[emoji24][emoji24][emoji24]
Pole sana mkuu, ukiwa health work inabidi usiwe na sympathy kabisa maana unaweza ukakimbia clinical area, utaonea huruma wangapi? Utalilia wangapi?
 
Kuna mama niliwahi kumpa lifti ilikua maeneo ya njia ya kahama geita ile njia ya vumbi watu wengi wanaifahamu.
Kutokana na mazingira niliyomkuta yalikua magum nilijua kwa muda ule hawez kupata msaada ilikua ni jion

Nilivyombeba niligundua ni mtu anae amini sana ushirikina alikua ananisimulia ni jinsi gan ndugu zake wamemloga na watoto wake huwa wanakufa kabla ya kufikisha miaka 10, hata yeye nilivyomuona alikua ni mgonjwa kakonda sana hivyo akasema hata yeye pia kalogwa na ndugu zake, baada ya safari kidogo aliacha kunisimulia akajifunika kanga yake usoni Basi mi nikajua kalala

Tulivyofika sehem natakiwa kumshusha namuamsha haamki, kila nikimuamsha haamki ghafla nikaona gari ya polisi nikawasimamisha wakaniambia tuongozane had hospita kufikisha hospital tu nikaambiwa kashakufa huyu, ikabd uchunguz uanze kama amelishwa sumu au nn bahat nzuri iligundulika kafa na maradhi ingekua vinginevyo ningewajibishwa hata ndugu zake wangeniiona ni Mimi ndo nimefanya
Duuh angekua amekunywa sumu ungeozea jela mkuu
 
Nakumbuka tarehe 12 Jan 2011 siku ya Mapinduzi, Bus la Sumry kutoka Dar kwenda Iringa tulivyopata ajali kugongana uso kwa uso na Lori la mizigo mbele ya mikumi ukiwa unaanza kuitafuta Kitonga..11 au 13 people walipoteza maisha siku ile..Hii safari ni kama ilikuwa ina ishara ila kiubinadamu ni ngumu kujua what kingekuja mbele yetu..Maana Ubungo pale watu hadi dakika za mwisho Dereva anataka kuondoa gari wasindikizaji zaidi ya 10 wanaagana na wapendwa wao hadi Dereva akagomba kiwa imetosha sasa wasiosafiri washuke ili tuanze safari.

Ila ninachokikumbuka zaidi ni Mama aliyekaa pembeni yangu maana toka mwanzo wa Safari alikuwa kama hayupo sawa..Salamu alikuwa anaitikia kwa uzito..Soda na Pipi alikataa vyote hakuchukua...Nilitamani nihame kabisa siti maana nilikuwa naona kama ana kisirani hivii..Mara nyingi huwaga nalala sana kwenye gari so tulivyofika tuu Moro Mjini nikalala zangu nikaachana nae...Kufika kwenye eneo la tukio Dereva wa lori alisinzia inavyosemekana kwenye kona ya mlima akakatia kona upande wetu so dereva kuona hivyo akakwepesha na kumpa ubavu kuanzia siti ya 3 kutoka kwake..Hivyo basi Lile lori likaanza kupiga siti hizo hadi mwisho na gari zote zikapinduka finally..
Kwa kuwa nilikuwa usingizini kushtuka sikuelewa kilichotokea haswaa nikakuta tuu abiria wenzangu kama wamelala hivii ila baada ya muda akili ikanirudia kuwa wameshafariki baada ya kuona ubongo,utumbo na vitu vingine..Kumbe ndiyo walikuwa washafariki including Mama wa pembeni yangu..Good enough niliumia lakini si sana compared to wengine..Niliona watu wawili wakija kufia nje kutokana na kutokwa sana na damu na msaada kuchelewa..Pia I still remember kuna Mzee alikuwa anamlilia Mke wake walikuwa wanapiga story ila ghafla tuu akawa hayupo nae tena.

Very bad expirience ambayo hadi leo imenifanya niwe na phobia ya kukaa dirishani kwenye safari ndefu..hata unipe milioni sikai siti ya dirishani..
Dah experience mbaya kweli yani, huwa nahofu sana nikiwa nasafiri na basi. Akili yangu imekuwa affected kiasi kwamba huwa sitakagi kukaa upande tofauti na wa dereva tena siti za katikati kuelekea mwisho
 
I believe when we die the soul leave our bodies, therefore, the possibility of seeing such a thing does not arise, and if it does, then it will definitely not be in such a dimension, maybe utaweza kufika msibani kwako na kuona maiti yako ukiw kama mtu mwingine anavofika, hutokuwa ndani ya mwili bali hewani.
Yeap the same to me japo katofauti kangu kidogo naamini roho inakua inajua kabisa huo ni mwili wake hipo hapo kulinda mazishi ya mwili wake[emoji7]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mama yangu mzazi, ilikuwa tarehe 1/5/2020.

Majira ya saa tatu usiku, nimekaa na mama tunazungumza huku tukiwa tunatazamana machoni. Hapohapo mama alifumba macho na hakufumbuwa tena.

Nilipatwa na mshangao usio wa kawaida, RIP mama
 
Style ya Jimmy McMelle ile noma
Kama kifo cha Jimmy na hao wana ilikuwa night kali wanatoka kula bata

Mmoja pale mataa ya Lugalo njiapanda ya kwenda Kawe (alitoka Dizzy pub anarudi Kawe Beach)

Mwingine mataa ya Africana njiapanda ya kwenda White sand (mwana alikuwa anahama kiwanja anatoka Last Point Salasala anaenda Juliana Mbezi Beach)

Mwanangu mwingine mataa ya fire (huyu kitambo kidogo alikuwa anatoka Billicanas)
 
Kuna msela alifiwa na mke wa mtu chumbani kwake.

Mke alimuaga mume anakwenda kijijini lakini mke kaenda jirani tu kwa msela. Hawajakaa sawa malaria, hawajakaa sawa mama Kavuta.

Jamani Tanga Kuna watu Wana busara, ukiambiwa hiyo Soo Kuna mgosi alikwenda kumtuliza mume wa MTU mpaka maisha yanaendelea!!! Ingekuwa huko Bunda au Geita pangechimbika.
Kwa akili za kawaida ni ngumu mno mume kupokea hili jambo usikute hata kuna nguvu zilitumika kumfanya mwenye mke awe mwelewa[emoji16]

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kama kifo cha Jimmy na hao wana ilikuwa night kali wanatoka kula bata

Mmoja pale mataa ya Lugalo njiapanda ya kwenda Kawe (alitoka Dizzy pub anarudi Kawe Beach)

Mwingine mataa ya Africana njiapanda ya kwenda White sand (mwana alikuwa anahama kiwanja anatoka Last Point Salasala anaenda Juliana Mbezi Beach)

Mwanangu mwingine mataa ya fire (huyu kitambo kidogo alikuwa anatoka Billicanas)
Gari na pombe ni shida. Mungu atusaidie tu
 
Back
Top Bottom