Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mtu anakuja kwako analia, kilio cha msibani. Anapiga magoti umkopeshe pesa. Unamkopesha kwa moyo safi kabisa. Anaondoka kwa shangwe utafikiri bwana arusi kaoa. Muda mliopatana wa kulipa deni ukifika, ghafla anapatwa na "ugonjwa wa kusahau kulipa madeni."
Ugonjwa usiotibiwa hospitali, ambao dawa yake ni "kidonge" kimoja tu - kulipa deni.😂 Cha ajabu ni kwamba, anasahau madeni tu, lakini nyama choma hasahau kula. Hasahau kuhonga wanawake. Hasahau “kilauri”
Ukimkumbusha deni, anakutazama kama vile umemkosea adabu; anashika kifua utafikiri ana shambulio la moyo. Anaanza hotuba ya maisha magumu, yenye maudhui kuliko mihadhara ya chuo kikuu.
Wakopaji wengine wakimuona kwa mbali aliyewakopesha, wanabadilisha “ruti.” Wengine wanabadili namba zao za simu. Mkopaji anayejiona mjanja zaidi kuliko sungura, atakuambia yuko safarini, akishuka atakupigia! Utasubiri wee, simu hupigiwi mpaka jogoo anawika! Asubuhi ukimuuliza vipi kulikoni, anakujibu: "Ooh samahani nilisahau." Wanaojifanya wamezaliwa na “simu janja,” wao “wanakupiga tofali” kabisa.
Biblia inasema wazi: "Asiye haki hukopa wala halipi" (Zaburi 37:21). I dare to talk openly:🗣️ ukikopa benki, ukikopa kwenye taasisi za kifedha, ukikopa kwa mtu, usiwe miongoni mwa wasio haki – lipa deni. Vinginevyo moto mkali wa jehanamu unakuhusu.😆