Umezuka Ugonjwa wa Kusahau Kulipa Madeni!

Mtu anakuja kwako analia, kilio cha msibani. Anapiga magoti umkopeshe pesa. Unamkopesha kwa moyo safi kabisa. Anaondoka kwa shangwe utafikiri bwana arusi kaoa. Muda mliopatana wa kulipa deni ukifika, ghafla anapatwa na "ugonjwa wa kusahau kulipa madeni."

Ugonjwa usiotibiwa hospitali, ambao dawa yake ni "kidonge" kimoja tu - kulipa deni.😂 Cha ajabu ni kwamba, anasahau madeni tu, lakini nyama choma hasahau kula. Hasahau kuhonga wanawake. Hasahau “kilauri”

Ukimkumbusha deni, anakutazama kama vile umemkosea adabu; anashika kifua utafikiri ana shambulio la moyo. Anaanza hotuba ya maisha magumu, yenye maudhui kuliko mihadhara ya chuo kikuu.

Wakopaji wengine wakimuona kwa mbali aliyewakopesha, wanabadilisha “ruti.” Wengine wanabadili namba zao za simu. Mkopaji anayejiona mjanja zaidi kuliko sungura, atakuambia yuko safarini, akishuka atakupigia! Utasubiri wee, simu hupigiwi mpaka jogoo anawika! Asubuhi ukimuuliza vipi kulikoni, anakujibu: "Ooh samahani nilisahau." Wanaojifanya wamezaliwa na “simu janja,” wao “wanakupiga tofali” kabisa.

Biblia inasema wazi: "Asiye haki hukopa wala halipi" (Zaburi 37:21). I dare to talk openly:🗣️ ukikopa benki, ukikopa kwenye taasisi za kifedha, ukikopa kwa mtu, usiwe miongoni mwa wasio haki – lipa deni. Vinginevyo moto mkali wa jehanamu unakuhusu.😆
Kopesha mtu kiasi ambacho huwezi kuumia ata akiingia mitini 🤣🤣🤣🤣
 
Hichi kirusi cha alaghai hususa katika mambo ya fedha ni hatari sana hapa Tanzania na hasa watu wanaotoka nyanda za juu kusini sio mchungaji, sio muinjilisti ,sio múumini wakawaida tena unaweza diriki kusema bora na mtu asiye sali maana unaweza chukua tahadhari lakini hawa wanaojidai wanamtumikia muumba alafu bahati mbaya zaidi muwe mnasali kanisa moja anajua huwezi mfanya chochote katika vyombo vya kisheria ,dawa kama mtu anataka mkopeshe mkatalie mtaendelea kupendana na kuheshimiana.
 
NJIA SALAMA, NI KUACHA KUMKOPESHA MTU HATA KAMA ATAKUJA NA SBB ZA KUTIA SIMANZI NAMNA GANI.
TENA NJIA NZURI UKISHAONA KUNA DALILI ZA MTU KUKOPA, ANZA KUMKOPA WEWE.

AU KAMA ANAOMBA KUKOPA 500,000, MPE 50,000 YA KUMSAIDIA, URAFIKI, UNDUGU WENU UENDELEE. KULIKO KUJA KUJAZA HASIRA KIFUANI KWA DADA DANA ZA KILA SIKU
 
Mtu anakuja kwako analia, kilio cha msibani. Anapiga magoti umkopeshe pesa. Unamkopesha kwa moyo safi kabisa. Anaondoka kwa shangwe utafikiri bwana arusi kaoa. Muda mliopatana wa kulipa deni ukifika, ghafla anapatwa na "ugonjwa wa kusahau kulipa madeni."

Ugonjwa usiotibiwa hospitali, ambao dawa yake ni "kidonge" kimoja tu - kulipa deni.😂 Cha ajabu ni kwamba, anasahau madeni tu, lakini nyama choma hasahau kula. Hasahau kuhonga wanawake. Hasahau “kilauri”

Ukimkumbusha deni, anakutazama kama vile umemkosea adabu; anashika kifua utafikiri ana shambulio la moyo. Anaanza hotuba ya maisha magumu, yenye maudhui kuliko mihadhara ya chuo kikuu.

Wakopaji wengine wakimuona kwa mbali aliyewakopesha, wanabadilisha “ruti.” Wengine wanabadili namba zao za simu. Mkopaji anayejiona mjanja zaidi kuliko sungura, atakuambia yuko safarini, akishuka atakupigia! Utasubiri wee, simu hupigiwi mpaka jogoo anawika! Asubuhi ukimuuliza vipi kulikoni, anakujibu: "Ooh samahani nilisahau." Wanaojifanya wamezaliwa na “simu janja,” wao “wanakupiga tofali” kabisa.

Biblia inasema wazi: "Asiye haki hukopa wala halipi" (Zaburi 37:21). I dare to talk openly:🗣️ ukikopa benki, ukikopa kwenye taasisi za kifedha, ukikopa kwa mtu, usiwe miongoni mwa wasio haki – lipa deni. Vinginevyo moto mkali wa jehanamu unakuhusu.😆
Mkuu sio usahaulifu, watu wengi Kwa sasa ni matapeli wanaokuja Kwa mwamvuli wa mkopo, lkn kiuhalisia anakutapeli.
 
Dah! Watu hatuombeani magonjwa, lakini mimi naomba huu ugonjwa nami unipate!
 
Back
Top Bottom