Afrikasana
JF-Expert Member
- Oct 27, 2021
- 320
- 288
Jana kupitia vyombo vya habari waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu amewataka wakurugenzi kufanya alichokiita msawazo wa watumishi katika halmashauri zao akilenga zaidi kwa walimu.
Amedai kwamba katika halmashauri nyingine sio kwamba walimu hawatoshi bali tatizo ni watumishi kulundikwa sehemu moja kwa wingi na kwingine ndani ya halmashauri hiyohiyo hakuna nguvukazi ya kutosha.
Ninamwambia Ummy aache kuwahadaa watanzania akiwafanya ni mazuzu yasiyoona. Mfano mzuri nikatika halmashauri yake ya Tanga jiji ambapo ndani ya ofisi ya Afisa elimu sekondari kuna kiini macho. Wapo maafisa elimu taaluma watatu na jamaa mmoja ambaye alikuja na afisa elimu sekondari kutoka huko aliko kua.
Mtu huyo aliyekuja na afisa elimu hajulikani kama anacheo gani kwenye hiyo ofisi. Je wale waliojazana pale sio walimu? Je wanafanya kazi gani pale zaidi ya majungu pale ofisini?
Kwataarifa yako Ummy nikwamba huyo jamaa aliyehama na huyo afisa elimu ndio anatumwa na afisa elimu huyo kwenda kuchukua bahasha za chochote kitu kwa wakuu wa shule. Pamoja na afisa elimu taaluma mmoja pale ambae naye anatumwa kukusanya posho kutoka kwa wakuu wa shule.
Pamoja na kuwapo kwa maafisa elimu taaluma wawili haitoshi Ummy kamuweka rafiki na kada mwenzake akawe afisa elimu taaluma ndani ya ofisi hiyo hivyo kuna maafisa elimu taaluma watatu kwenye ofisi moja. Je huo msawazo kwanini usianzie maofisini? Ummy ameamua kulipa fadhila kupitia ofisi ya umma hata kama hakuna uhitaji. Je wewe Ummy huo ndio msawazo au mvurugo?
Ummy unaiharibu Tanga kwakulea marafiki zako huku ukitaka watanzania watende haki.Nakuuliza je wewe kama haki huiwezi utawashurutisha vipi wenzako watende haki?
Kaondoe yule rafiki yako kwenye ofisi ya afisa elimu sekondari ambaye alikua mkuu wa shule ya sekondari Toledo kisha ndio utangaze msawazo.
Ukiongea uongo utakumbushwa. Ummy badilika ofisi ya umma sio kijiwe cha kubwabwaja pasipo kumaanisha. Tenda kwa usahihi ndio uwaongoze wengine kutenda kwa usahihi