Ummy Mwalimu apiga marufuku kulazimisha watu kuchanja, Watanzania waliochanja wamefika milioni 8.5

Ummy Mwalimu apiga marufuku kulazimisha watu kuchanja, Watanzania waliochanja wamefika milioni 8.5

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Ummy.JPG
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameendelea kupiga marufuku tabia za Watoa huduma kulazimisha wananchi wanaoenda kupata huduma za afya kulazimishwa kuchanja, ameeleza kuwa tabia hiyo ni kinyume cha miongozo na maadili ya taaluma za Watoa huduma.

Ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kujitokeza kupata Chanjo ya UVIKO-19, hasa watu walio katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huo kama vile wenye magonjwa sugu (Shinikizo la damu, kisukari, magonjwa, saratani, UKIMWI n.k) na wazee.

Amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya imelenga kufikia asilimia 70 ya watu waliochanja ikiwa ni sehemu ya mkakati wa Dunia wa kupambana dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19.

Ameyasema hayo wakati akiwa na Waziri wa TAMISEMI na Mwakilishi kutoka Wizara ya fedha katika Mkutano na Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Umoja wa Mataifa Dkt. Ted Chaiban aliyeambatana na wajumbe kutoka WHO na UNICEF.

Ameongeza kuwa mpaka kufikia Aprili 5, 2022 tayari watu milioni 8.5 wameshapatiwa Chanjo ya kupambana dhidi ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kuweka wazi kuwa, bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuweza kuchanja watu waliobaki ili kuweza kuishi na ugonjwa huo kama magonjwa mengine.

Source: Voice of Bongo
 
yaani we Mama mi nakuelewaga toka enzi za Magufuli endelea kupambana Mungu atalusimamia.

mi nilishasema mtanichanja nikiwa maiti ila nikiwa hai hio itakua ngumu sana walahi
 
yaani we Mama mi nakuelewaga toka enzi za Magufuli endelea kupambana Mungu atalusimamia.

mi nilishasema mtanichanja nikiwa maiti ila nikiwa hai hio itakua ngumu sana walahi
Wakati huo huo ukiugua kichwa unakunywa Panadol ya Beberu? 😂😂

Nyie mnao kejeli chanjo mnawashauri nini wanaougua Covid 19 hadi kulazwa ICU ama ambao Wana kisukari! Wajilinde vipi dhidi ya Covid 19?
 
Je huu msimamo ni kwa Covid 19 pekee ama kwa magonjwa yote huwa hauendi hospitali?
Niwe muwazi kwenye huu mpango wa kukataa chanjo Magu alifanikiwa kwa asilimia kubwa sana, ila maswali yangu alisema chanjo sio nzuri je ni covid pekee au chanjo zote?
 
Niwe muwazi kwenye huu mpango wa kukataa chanjo Magu alifanikiwa kwa asilimia kubwa sana, ila maswali yangu alisema chanjo sio nzuri je ni covid pekee au chanjo zote?
Aliiita kuwa ni vita ya kiuchumi, hivyo ali-refer kwenye hilo tu.

Kwa asilimia karibu zote alikuwa sahihi. Wanakupa mkopo wa kupunguza makali ya Covid19, unaenda kujenga madarasa?

Kama kweli ni ugonjwa hatari, kwanini wasijenge hospitali na kununua zile mashine za kupumilia? Wakaongeza uwezo wa ICU kupokea wengi zaidi na kuokoa maisha?
 
Wakati huo huo ukiugua kichwa unakunywa Panadol ya Beberu? 😂😂

Nyie mnao kejeli chanjo mnawashauri nini wanaougua Covid 19 hadi kulazwa ICU ama ambao Wana kisukari! Wajilinde vipi dhidi ya Covid 19?
ukichanja ww na ukoo wenu si inatosha kwani lazima sote tuishi milele wengine si inabidi tusepe ?

kaa kwa kutulia wewe ...
 
Aliiita kuwa ni vita ya kiuchumi, hivyo ali-refer kwenye hilo tu.

Kwa asilimia karibu zote alikuwa sahihi. Wanakupa mkopo wa kupunguza makali ya Covid19, unaenda kujenga madarasa?

Kama kweli ni ugonjwa hatari, kwanini wasijenge hospitali na kununua zile mashine za kupumilia? Wakaongeza uwezo wa ICU kupokea wengi zaidi na kuokoa maisha?
Ni nchi zote pesa ya covid wamejengea madarasa? Au unatumia mfano Tanzania kugenaralize?
 
Waache kuwashukia watumishi wa idara ya afya wanapopeleka zero report ya chanjo yq UVIKO-19
 
Back
Top Bottom