Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Waziri wa Afya ndugu Ummy Mwalimu amesema kuwa Katika nchi yetu ya Tanzania, watoto chini ya miaka mitano asilimia 31.8 wana utapiamlo.
Waziri akaendelea kusema kuwa, hali hiyo inahatarisha maendeleo ya ukuaji ubongo wa watoto hao kitu kinachoweza kupelekea udumavu wa akili.
Mimi binafsi nimeogopa sana kwa takwimu hizi. Hawa watoto ndiyo Taifa la kesho, Je taifa litakuwa ni taifa la namna gani kama 31.8% ya watoto wachanga leo ni wadumavu.
Hapo ndipo ninapojiuliza, Je serikali hii ambayo inajitapa kuwa tumeingia uchumi wa kati, huo uchumi wa kati unatusaidia nini kama asilimia 31.8 ya vichanga vyake vipo katika hatari ua udumavu wa akili sababu ya utapia mlo?
Watu wanapolalamika kuhusu maendeleo ya watu vs Maendeleo ya vitu wanakuwa wanamaanisha vitu kama hivi. Kiukweli, hizi takwimu zinatisha.
Serikali ianze kuwekeza kwenye maisha bora ya wananchi badala ua kuwekeza kwenye miradi ya tembo mweupe kama vile uwanja wa ndege Chato na daraja la baharini huko Dar es Salaam.
Kwa vyovyote vile Taifa inabidi litokwe na machozi kuona 31.8% ya vichanga vyake huenda vikadumaa akili sababu ya utapiamlo.
Serikali iweke priorities zake sawa