OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Anaandika katika kurasa yake Twita
Tumepokea maoni na ushauri kuhusu Kanuni za mwaka 2020 zinazosimamia usajili wa majengo ya dawa (ikiwemo maduka binafsi karibu na Hospitali/Vituo vya huduma za Afya vya Serikali.
Ni mjadala mzuri. Tumefurahi kujua kuwa watanzania wengi tunakubali kuwa lipo tatizo kubwa ktk mfumo.mfumo mzima wa ugavi, usambazaji na usimamizi wa dawa. Sisi @wizara_afyatz tutasimamia maslahi ya watanzania kwa kuhakikisha kuwa wanapata dawa ambazo ni salama, zenye ubora na kwa gharama nafuu. Hivyo tutakuchukua hatua kadri tutakavyoona inafaa ili kufikia lengo hili ikiwemo
Kwanza, tutaisimamia vyema
@MsdTanzania kutimiza wajibu wake ktk kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa nchini.
Pili, tutaboresha mifumo ya udhibiti na usimamizi wa dawa na bidhaa nyingine za Afya katika Hospitali na Vituo ya kutoa huduma za Afya vinavyomilikiwa na Serikali.
Tatu, Tutasimamia kikamilifu matumizi ya Mwongozo wa Taifa wa Matibabu (National Standard Treatment Guideline) wa mwaka 2021; cheti cha dawa sambamba na miongozo mingine ili kuwapunguzia wananchi adha ya kutafuta dawa wanazoandikiwa ambazo zipo nje ya Miongozo ya Matibabu.
Dawa ni Sayansi, Dawa ni Uhai, Dawa ni Biashara na Dawa ni Siasa. Asanteni wote kwa maoni. Tumeyapokea na tutayafanyia kazi.