Ummy Mwalimu: Hospitali maalum ya watoto inayoitwa Rainbow kujengwa Tanzania

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 12 Oktoba, 2023.

Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Tanzania imepata faida kwenye ziara ya Rais nchini India ikiwemo kuingia makubaliano na baadhi ya Hospitali za huko kuanzisha huduma zao nchini.

Waziri Ummy amesema mojawapo ya Hospitali hizo ni Rainbow ambayo itashughulikia masuala yote ya watoto kuanzia siku ya 1 hadi miaka 17.

"La mwisho ambalo kwangu tunaona kama ushindi mkubwa kwenye sekta ya afya, kupata hospitali yeye wakiamka ni watoto tu, Rainbow children hospital, wao ni watoto tu. Kama ni upasuaji wa moyo ni upasuaji wa koyo wa watoto, kama ni upasuaji wa mifupa, upasuaji wa mifupa wa watoto. Yeye kazi yake akiamka, ICU yake ni ya watoto, kila kitu chake ni cha watoto, ambulance yake ni ya watoto kuanzia siku 1 mpaka miaka 17. Hayo tunaamini ni mafanikio makubwa" amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo, amewaomba watanzania kutokutishika na jina hilo kwani halina maana mbaya.

Aidha, Serikali imepata kampuni itakayoanza kutengeneza dawa nchini ili kupunguza mzigo wa zaidi ya 80% zinazoagizwa nje ya nchi ambapo 60% kati yake huagizwa India.

Mambo haya kwa pamoja yataongeza ubora wa huduma za afya nchini pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji na uagizaji wa madawa kutoka nje ya nchi.

Rainbow - Ndugu wananchi mna maswali yoyote? 😀
 
"La mwisho ambalo kwangu tunaona kama ushindi mkubwa kwenye sekta ya afya, kupata hospitali yeye wakiamka ni watoto tu, Rainbow children hospital, wao ni watoto tu. Kama ni upasuaji wa moyo ni upasuaji wa koyo wa watoto, kama ni upasuaji wa mifupa, upasuaji wa mifupa wa watoto. Yeye kazi yake akiamka, ICU yake ni ya watoto, kila kitu chake ni cha watoto, ambulance yake ni ya watoto kuanzia siku 1 mpaka miaka 17. Hayo tunaamini ni mafanikio makubwa" amesema Waziri Ummy
Jambo jema lakini tuna kawaida ya kuanzisha vitu vipya vingi na uendelezaji wake unaishia kuwa maonesho, imagine Mloganzila ianenda kuwa hospitali ya kuongeza maumbile badala ya kujikita kwenye changamoto zinazowakabili watanzania wengi
 
Leo wameanza na Rainbow kesho likajengwa Tawi la Rainbow la wakubwa mtalalamika Kweli ? Au mimi ndo Sioni Mbali.

Ushetani unaanzaga kidog kidog mwshoe mnajikuta mmeingia Mazima.
 
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus akizungumza na Waandishi wa Habari leo tarehe 12 Oktoba, 2023.

Akizungumza kwenye Mkutano na waandishi wa Habari ulioandaliwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema Tanzania imepata faida kwenye ziara ya Rais nchini India ikiwemo kuingia makubaliano na baadhi ya Hospitali za huko kuanzisha huduma zao nchini.

Waziri Ummy amesema mojawapo ya Hospitali hizo ni Rainbow ambayo itashughulikia masuala yote ya watoto kuanzia siku ya 1 hadi miaka 17.

"La mwisho ambalo kwangu tunaona kama ushindi mkubwa kwenye sekta ya afya, kupata hospitali yeye wakiamka ni watoto tu, Rainbow children hospital, wao ni watoto tu. Kama ni upasuaji wa moyo ni upasuaji wa koyo wa watoto, kama ni upasuaji wa mifupa, upasuaji wa mifupa wa watoto. Yeye kazi yake akiamka, ICU yake ni ya watoto, kila kitu chake ni cha watoto, ambulance yake ni ya watoto kuanzia siku 1 mpaka miaka 17. Hayo tunaamini ni mafanikio makubwa" amesema Waziri Ummy.

Hata hivyo, amewaomba watanzania kutokutishika na jina hilo kwani halina maana mbaya.

Aidha, Serikali imepata kampuni itakayoanza kutengeneza dawa nchini ili kupunguza mzigo wa zaidi ya 80% zinazoagizwa nje ya nchi ambapo 60% kati yake huagizwa India.

Mambo haya kwa pamoja yataongeza ubora wa huduma za afya nchini pamoja na kupunguza gharama za uzalishaji na uagizaji wa madawa kutoka nje ya nchi.

Hongera Sana JMT... Hii ni Hatua kubwa sana Siemple
 
Duuu haya ndio madhara ya kuomba omba aiseee hii kali sana
 
''hata hivyo, amewaomba watanzania kutokutishika na jina hilo kwani halina maana mbaya''.
Hili nalo litapita tu
 
Wewe usijifanye uelewi watu wanasema nini hata hao wafiraji na wafirwaji tunajua wameumbwa na Mungu kwa hiyo bado sio sababu ya kutumia jina hilo …hakuna ulazima!

Hii hospitali itakosa wateja lazima serikali ichukue hatua!
Kwani usipoenda hospitali nani ataathirika 😀😀😀 au utakuwa unamkomoa nani..
Tanzania tuache mindset za Kitoto
 
Mradi wa bomba la mafuta ulikuwa uishie jimboni kwako umefikia wapi?
Wizara nyeti zimepewa watu wa ajabu kupita kiasi.
1. Afya
2. Maliasili
4. Ulinzi
5. Bunge
6. Kazi na ajira
Hili kundi kazi yao ni kusema mama, mama
Unataka wizara 1 na 4 zifanyaje ujue zinafanya kazi
 
Wewe usijifanye uelewi watu wanasema nini hata hao wafiraji na wafirwaji tunajua wameumbwa na Mungu kwa hiyo bado sio sababu ya kutumia jina hilo …hakuna ulazima!

Hii hospitali itakosa wateja lazima serikali ichukue hatua!

Sio lazima uende, wenye akili timamu and who can see through the bullshit will go. Kama wewe hiyo ndo tafsiri yako, more power to you, usiende. Wengine hata neno Mungu ni tusi kwao na hawaendi kabisa kwenye nyumba za ibada wakati wengine wanaenda kuabudu huko. To each their own.
 
Mradi wa bomba la mafuta ulikuwa uishie jimboni kwako umefikia wapi?
Wizara nyeti zimepewa watu wa ajabu kupita kiasi.
1. Afya
2. Maliasili
4. Ulinzi
5. Bunge
6. Kazi na ajira
Hili kundi kazi yao ni kusema mama, mama
Watu wana piga kazi... kama una marafiki
Igunga
Nzega
Na Tanga

Wata kupa majibu ya kinacho endelea maeneo hayo...

Bomba la mafuta lipo kazini, ni kazi kazi
 
Back
Top Bottom