Ummy Mwalimu na fursa ya kukamilisha bima ya afya kwa wote!

Ummy Mwalimu na fursa ya kukamilisha bima ya afya kwa wote!

funaku

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Posts
39,468
Reaction score
31,952
Watanzania wengi wameshangilia ujio wa Mhe.Ummy Mwalimu a.k.a ODO hivi sasa akiwa mtumishi mwandamizi kumsaidia Rais Samia.

Ni ukweli usiopingika kuwa mwanasheria huyu na mbunge mstaafu anao uzoefu mkubwa katika sekta ya afya na pia uzoefu wa kipekee katika kutambua changamoto za afya hususani afya ya msingi ambayo kwa sasa bado inaleta changamoto na malalamiko mengi.

Uteuzi wake ni fursa ya kipekee katika kutatua changamoto muhimu ya sekta ya afya.
Sera ya afya 2007 inapaswa kurejewa kwa kiasi kikubwa ili kuondoa sintofahamu ya aina gani ya sera inayotakiwa kufuatwa kati ya huduma bure dhidi ya uchangiaji wa huduma.

Kupitia Waziri Ummy Mwalimu tulishuhudia kupitishwa kwa sheria ya bima ya afya kwa wote japo hadi leo utekelezaji wake umeenda kwa mwendo wa kobe.

Ni muda sasa wa ku-fast track utekekezaji wa Bima ya afya kwa wote lakini pia kuhuisha Sera kongwe ya afya.
Ushauri wangu kwake afanye mapitio ya haraka ya kutambua kwa nini wataalamu wa afya hususani ngazi ya msingi walialika uanzishwaji wa bima ya afya kwa wote ,na hivyo apate maoni sahihi kutoka kwa watu sahihi juu ya utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote.

Karibu tena mhe.Ummy Mwalimu katik ujenzi endelevu wa sekta ya afya.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA!
 
Hatimaye kazi inaanza
 
Back
Top Bottom