Uchaguzi 2020 Ummy Mwalimu ndio Mbunge Anaetufaa Tanga Mjini 2020

Uchaguzi 2020 Ummy Mwalimu ndio Mbunge Anaetufaa Tanga Mjini 2020

Habari wana JF.

Katika makosa waliofanya wananchi wa tanga mjini mwaka 2015 n kumpa ubunge mtu ambae haguswi ata na kero za wananchi wake, kumekuwa na mbunge jina tuu, mbunge anashindwa ata kuchangia hoja za msingi bungeni kwa maslah ya wananchi wake, leo hii ni aibu unaweza kuta mkazi wa tanga mjini lakini hamjui ata jina mbunge wake... Wana tanga tumekuwa nyuma zaidi kimaendeleo miaka 5 mfululizo.


Wana Tanga sasa imetosha ni wakati wa kutofanya makosa tena 2020, tunataka mtu atakaeguswa na changamoto za wananchi wake, tunataka mtu shupavu, mwajibikaji, mwenye roho ya huruma, mwenye weledi wa hali ya juu haya yote anayo dada etu UMMY MWALIMU.

Katika ubunge tu wa viti maalum alokuwa nao keshafanya mambo makubwa kutoa sapoti kubwa katik timu yetu ya coastal union, kutoa vifaa mbalimbal ikiwemo kompyuta kwa wakuu wa shule, kufadhili wadada waliofeli wasome tena QT, ni mtu anaeguswa na changamoto mbalimbali za kijamiii na kiuchumi., ni miongoni mwa kiongoz aliekaa kwenye wizara bila kutumbuliwa kutokana na uadilifu wake na uwajibikaji.

2020 ni wakati sasa wa kumpa rasmi jimbo la tanga mjini mana ana uthubutu na hari ya kuwaletea maendeleo wana Tanga Mjini, huu sio wakati wa kupepesa macho lazma tupate mtu sahiihi kwa mustakabali wa wananchi wa tanga mjini.


Sisi wananchi tuko tayar ata kumchukulia fomu kwa gharama yoyote ile.

#UmyyIsOurNextMP#TangaMjiniNaUmmy #2020HatufanyiMakosaTena#UmmyAnatutoshaaaaView attachment 1343112

Sent using Jamii Forums mobile app
Amewahi kufanya nini na wapi ?
 
Hapa ndio wananchi tunapokosea, tusipende sana eti watu wakutusemea kero ambazo kila mtu anaziona...

Ni wakati sasa wa kuchagua watu wenye mbinu na uwezo direct wa kutatua shida kama ajira kwa vijana, kuhamasisha na kutoa elimu watu wasomeshe watoto, kuwatengenezea wananchi connection na mataifa yaliyoendelea vijana wapate ujuzi mbalimbali, kuyatumia maeneo yetu ya ardhi vizuri kwa kuwajengea wananchi uwezo wa kulima na kuuza mazao yao...
 
Kuwasemea wananchi kero zao kwa serikali yenye organs lukuki za kutambua na kutatua kero za wananchi sio kigezo cha kusema fulani anafaa kuwa Mbunge..
 
Tuambie huyo mama kwa kutumia akili na uwezo wake kifedha amesaidia nini wakazi wa Tanga kwa kujitolea na si kwasababu anautaka ubunge..

Amekuwa Mbunge kwa zaidi ya 5yrs, ameleta mfumo gani madhubuti ambao umeongeza kitu kwenye mkoa wa Tanga??
Kutumia akili yake na uwezo wake ametengeneza ajira ngapi kwa mkoa wa Tanga wenye wakazi wengi masikini..??

Atuambie pia atatumia strategies gani yeye kama yeye bila kuihusisha Serikali na maelfu ya wananchi wa Tanga hasa madada wengi wasio na uelekeo wakanufaika??
 
Mtu sahihi wa kukata kiu ya maendeleo ya wana Tanga Mjini 2020 ni Dada @ummymwalimu ... Wana Tanga wenzangu amkeni amkeni amkeni jamani 2020 si kipindi cha kufanya makosa Tena Tambueni kuwa ukitandika Pazuri Utalala Pazuri UmmyMwalimu kwa hakika amethubutu, ametenda na ameweza, ummy ni Jembe linalolima hadi majani yasiyoonekana, ummy ni Daraja la kutuvusha, ummy ni Taa pekee ya kuangazia Matatizo yetu wana Tanga.
Ng'ara dada ummy nga'ra, tembea kifua mbele huku ukijua kamwe wana Tanga hatuwezi kukuangusha tuko Bega kwa bega nawe, tambua upendo tulionao kwako hauna pazia.

#2020TangaYaUmmyMwalim
#2020HatufanyiMakosaTena
#IstandwithUmmyMwalim
#BegaKwaBegaNaUmmy
#JimboTunampaUmmy
#2020TunatembeaNaUmmy
#UmyyAnatoshaaa
3.jpeg
 
Sio Tanga tu Bali sehemu zote zenye waislamu wengi lazima CCM ishinde kwa kishindo maana sisi waislamu wengi wetu ni darasa la saba na tunatoka kwenye jamii za kimasikini hadi Leo watoto wetu bado wanasoma chini ya miti maji shida miundo mbinu hakuna zahanati zipo mbali lakini sisi sote CCM oyeee
Jamani tusomeshe watoto wasije Wakawa kama sisi
 
Tanga Ccm imekufa kitambo kinachofanyika sasa ni mabavu tu, kuanzia ile issue ya madiwani wa upinzani kununuliwa kwa nguvu na vitisho kisha kurudishwa kwenye baraza la madiwani.kama ndugai na mwambe bungeni, vichekesho tupu.
 
Hujaweka sifa yake moja kuwa ni chakula cha.......since jamaa anavyoshobokea wanawake weupe hivyo teuzi zake zenye sura nyeupe huwa nina mashaka nazo
 
Back
Top Bottom