Ummy Mwalimu: Watoa huduma za afya wasikimbie wagonjwa, sio kila homa kali ni Corona

Ummy Mwalimu: Watoa huduma za afya wasikimbie wagonjwa, sio kila homa kali ni Corona

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Afya wa Tanzania, Ummy Mwalimu amesema watoa huduma wa sekta ya afya hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa na badala yake, wanatakiwa kuzingatia Kanuni za Udhibiti wa Maambukizi katika kutoa Huduma (IPC).

Ummy amesema sio kila homa kali au kikohozi ni CoronaVirus hivyo watoa huduma hawatakiwi kuwakimbia wagonjwa kwasababu kuna magonjwa mengine kama Kisukari, Moyo, HIV na TB.

Pia, Waziri huyo amewataka kuendelea kuwa makini kwa kuchukua tahadhari mbalimbali ikiwemo kunawa mikono pale wanapotoa huduma.

Msikilize akizungumza hapa:

 
Yaani kwani mpaka sasa hawajui hayo ?, nadhani wao ndio wapo katika better position ya ku-access the situation..., nadhani pia tujitahidi kuwapa vifaa ili kuwaondelea hofu
 
Ukitaka ushindi, lazima uwe mstari wa mbele, simama nao, pale, wakuone watie moyo, ukikaa mbali, nao watakaa mbali kuepuka unacho kiepuka wewe! Kila mtu ana haki ya kufanya kazi katika mazingira salama.
 
Natamani kusikia hawa Wauguzi wakiongezewa posho ili angalau Morali ya kufanya kazi irudi, Maana huu ugonjwa unawakumba hadi Madaktari na wauguzi.
 
Natamani kusikia hawa Wauguzi wakiongezewa posho ili angalau Morali ya kufanya kazi irudi, Maana huu ugonjwa unawakumba hadi Madaktari na wauguzi.
Tena wao ndio wako kwenye risk kubwa ya kuupata kirahisi kama hawajapewa vifaa stahiki vya kujikinga.
 
Back
Top Bottom